Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Alafu baada ya kufa Baba J ndio mwimbaji akawa dogo jack simela,au huyu dogo jack simela alikuwepo kitambo?
 
Ahsante mkuu,ila nimeutafuta mtandaoni sijaupata,Kama unao nauomba,mimi jagwa ndio bendi yangu pendwa so nikajua wameimba wao
Ninao ila nimejaribu ku-apload nikutumie umekataa, kama hutojali nitumie namba yako ya WhatsApp nikutumie.
 
Mimi bhana naomba kujua hawa waliokuwa wanatajwa kwenye nyimbo za jagwa walikuwa na cheo gani kwenye bend,
1.Kamongo Manja(Manjalino)
2.Jolijo
3.Saidi Misape
4.Bonge mzito
4.Baba Dullah

1. Manjarino ni mdau mkubwa wa Jagwa
2.Jolijo ndio mkurugenzi wa Jagwa
3. Bonge Mzito ambae kwa sasa ni marehemu alikuwa shabiki mkubwa wa Jagwa ila alikuwa mwizi hatari miaka hiyo maeneo ya Mwananyamala, Tandale na Manzese
4. Baba Dullah nae ni mdau wa Jagwa.
 
Ok!ahsante sana kwa kunifahamisha,maana mi nilijua ni majina wale wapiga vyombo,unaweza kunitajia majina ya wapiga vyombo?
 
Alafu baada ya kufa Baba J ndio mwimbaji akawa dogo jack simela,au huyu dogo jack simela alikuwepo kitambo?
Hapana, kwanza Baba J hakufariki akiwa uraiani alipelekwa mahabusu ambapo huko ndio umauti ulimkuta. Kwa hiyo baada ya Baba J kupelekwa Jera akaja muimbaji mwingine jina kidogo limenitoka ila kama unaujua wimbo wa Kondacta wa Chaukucha yule muimbaji ndio aliechukua nafasi ya Baba J.
Baada ya huyo jamaa kwenda Chaukucha ndio dogo Jack akachukuliwa kutoka Morogoro kuja Dar kujiunga na Jagwa Music.
 
Ahsante sana kiongozi kwa darasa unalonipa,basi ndio maana kuna wimbo ameimba dogo jack unaitwa maisha popote,kumbe katokea morogoro kuja dar
 
Wengi wao si wote walikuwa kwapukwapu yaani mnanda na uporaji kama uji na mgonjwa wengi wanakuwa watu wa maskani hawana kipato cha kueleweka so wanaongeza kipato kwa kukaba na kupora watu.
 
Jolijo sifa nyingine kwa mwananyamala kisiwani ni mpishi maarufu wa pilau kwenye shughuli za kijamii
 
Interview ya gari kubwa.
Kumbe hiyo Albam iliyotamba jamaa walilipwa 80,000/- Tu
 
Interview ya gari kubwa.
Kumbe hiyo Albam iliyotamba jamaa walilipwa 80,000/- Tu
Dah...kumbe walianza mwaka 1981 na Ali Hassan Mwinyi umeimbwa 1986
 
Mimi ninayo ila nashindwa kuapload humu, nitumie namba ya WhatsApp nitakutumia. Halafu kuna WhatsApp group la Mchiriku lipo ukitaka utaunganishwa, huko utapata kila unachotaka kuhusu Mchiriku.
Hili group bado lipo?
 
Mimi niko mbioni kufanya hivyo,kwani nina historia iliyoshiba ya mziki huu na nawajua watu wengi waliokua ni wadau wakubwa ambao wanaweza kunirekebisha nikoseapo.Halafu naupenda mziki huu.
Bob naweza pata namba yako ya simu?
 
Mimi niko mbioni kufanya hivyo,kwani nina historia iliyoshiba ya mziki huu na nawajua watu wengi waliokua ni wadau wakubwa ambao wanaweza kunirekebisha nikoseapo.Halafu naupenda mziki huu.
Kama hutojali kuna what group la Mchiriku humo kuna wakongwe na wadau wanaoujua historia za muziki huu na wasanii wa sasa pia wapo humo. Kwa vile unataka kuandaa Documentary nakushauri ujiunge huko uchukue baadhi ya "madini" ambayo yatakusaidia kwenye Documentary yako. Ukitaka kujiunga nitumie namba yako ya WhatsApp PM.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…