Mchongo gani utanifaa, nina 1,000,000 cash nina page yenye followers 60k

Shozylin

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
341
Reaction score
699
Wakuu habari zenu.

Wale wazee wa kuchungulia fulsa naombeni tafadhali mnipe mwanga.

Mm ni kijana nipo mkoa wa dodoma, Nina cash ya sh 1 million Nina miliki page zenye followers zaid ya 60k zinazo jihusisha na michezo.

Akili yangu inanituma kua kupitia hawa wafuasi active nilio nao hawa pia wanaweza kua chanzo Cha kipato. Nataka kupingana na akili yangu kwa hoja zenye mashiko lakini nakosa Kama una hoja Basi ungana nami kupinga akili yangu kwenye comment.

Akili yangu bado inajaribu kuwaza Nawezaje kuanzisha mchezo wa bahati nasibu (kubashiri) mechi kupitia page zangu za michezo.? Hapa penyewe nataka wale ma great thinker waje tujadiri.

Akili yangu pia inanambia kua, naweza kutengeneza application mfano Kama ile ya baraka mpenja, Millard ayo ila nikikumbuka mtaji nilio nao naona kabisa hili linabaki kuwa wazo tu. Hapa penyewe nahitaji washauri waje tujadiri.

Karibuni.[emoji16]
 
Nunua dawa za kuongeza nguvu za kiume, Dawa za kuongeza makalio, dawa za kupunguza mwili.
Niko nimekaa pale utakuja kunishukuru baadae ...
 
Nunua dawa za kuongeza nguvu za kiume, Dawa za kuongeza makalio, dawa za kupunguza mwili.
Niko nimekaa pale utakuja kunishukuru baadae ...
Nikisha nunua nazifanyia Nini mkuu.?

Weka nyama nyama kidogo
 
Anza kuwaunzia mikeka hao followers wako,fanya kile unapenda,Kama hiyo ulipata uko uko kwenye kamari basi tafuta ujanja mwingine uko uko,na tafuta namna ya kupost matangazo mbali mbali na kupata commission
 
Followers 60k walikufuata kwenye huduma gani ya kimichezo?
 
Anza kuwaunzia mikeka hao followers wako,fanya kile unapenda,Kama hiyo ulipata uko uko kwenye kamari basi tafuta ujanja mwingine uko uko,na tafuta namna ya kupost matangazo mbali mbali na kupata commission
Poa poa mkuu.
 
Anaetaka followers kwa ajili ya reputation ya biashara yake anicheki.
10,000 (10k) Followers kuanzia Tsh 45,000 tu.
 
Tafuta trending good (unaweza anza hata na jersey kadhaa kama ulivyoshauriwa) halafu agiza toka china au katafute kariakoo kwenye maduka ya jumla. Piga picha vizuri then post IG kwa maelezo mazuri kabisa. Piga sponsered ads hata $20 hela yako itarudi tu. Then subiri simu za wateja uanze kula faida. 😎
 
Mkuu nimekuelewa.
 
Njoo nikufanyie Designing ya App kwa bei rahisi then Developer ataikamilisha hiyo pesa inatosha

User tiali unao Utachofanya unawa Tap nakuwaingiza kwenye App yako

Kwenye App utapata pesa kwa Paying User na Ads za Kampuni

Check DM for more negotiation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…