Johnson Alex Otieno
Senior Member
- Mar 14, 2013
- 172
- 57
"Mchongo".
Rushwa/Takwima/Chai/Zawadi/Asante.
Ukifika Swekeni unaambiwa kuna MCHONGO,tafuta wanaoeleweka,leta majina yao wapate mchongo.
Wanaoeleweka ni wale wanaotoa chochote kitu kwa mwenye mchongo.
Athari za MCHONGO.
Tumekuwa na watendaji wabovu,wasiojiamini,walamba viatu na wenye kujipendekeza.
Michongo imekandamiza na kuua haki za watu,imeua mioyo ya wazalendo na uzalendo wa wananchi wa swekeni.
Michongo imetengeneza makundi katika ofisi nyingi za Swekeni,Kuna upendeleo wa makusudi kwa wenye utayari wa kutoa kitu Ili wapate mchongo.Asiyetoa huonekani mkaidi na asiyefaa.
Michongo imeleta viongozi wenye mitazamo inayofanana,mbaya zaidi mitazamo Yao ni mfu,ndio maana swekeni maendeleo ni Duni sana,hapa swekeni ni matumizi ya nguvu na mabavu badala ya Hoja kujibiwa kwa hoja.
Tufanye nini kuiokoa Swekeni?
Tujifunze ,tufundishwe kushika na kuishi Sheria ya Bwana.
"Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa"
Wazee waswekeni tunatoa wito kwa wananchi wote wa swekeni na viunga vyake kutoshiriki kazi yeyote ambayo itakuja kwa jina la mchongo.
SILAHA YA MNYONGE NI UMOJA