Mchongo ni rushwa

Mchongo ni rushwa

Johnson Alex Otieno

Senior Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
172
Reaction score
57
"Mchongo".
Rushwa/Takwima/Chai/Zawadi/Asante.
Ukifika Swekeni unaambiwa kuna MCHONGO,tafuta wanaoeleweka,leta majina yao wapate mchongo.
Wanaoeleweka ni wale wanaotoa chochote kitu kwa mwenye mchongo.

Athari za MCHONGO.
Tumekuwa na watendaji wabovu,wasiojiamini,walamba viatu na wenye kujipendekeza.

Michongo imekandamiza na kuua haki za watu,imeua mioyo ya wazalendo na uzalendo wa wananchi wa swekeni.

Michongo imetengeneza makundi katika ofisi nyingi za Swekeni,Kuna upendeleo wa makusudi kwa wenye utayari wa kutoa kitu Ili wapate mchongo.Asiyetoa huonekani mkaidi na asiyefaa.

Michongo imeleta viongozi wenye mitazamo inayofanana,mbaya zaidi mitazamo Yao ni mfu,ndio maana swekeni maendeleo ni Duni sana,hapa swekeni ni matumizi ya nguvu na mabavu badala ya Hoja kujibiwa kwa hoja.

Tufanye nini kuiokoa Swekeni?
Tujifunze ,tufundishwe kushika na kuishi Sheria ya Bwana.

"Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa"
Wazee waswekeni tunatoa wito kwa wananchi wote wa swekeni na viunga vyake kutoshiriki kazi yeyote ambayo itakuja kwa jina la mchongo.

SILAHA YA MNYONGE NI UMOJA
 
Tanganyika mnaigeuza geuza majina kila mtu anavyojisikia kuita, mara bongo, leo huyu naye kaja na uswekeni, yote kwa yote ni heri tu!

Mtoa mada elewa kuwa hakuna raia wanaojifinyanga na kujishepu wenyewe bila kuwa muongozo wenye kueleweka na muongozo ni sheria.

Ukiona pahala hakuna rushwa, raia wazalendo wanaoipenda nchi yao na kujivunia, wanampenda kwa dhati Rais wao na mambo mengine mema nk nk, elewa sheria za msingi zinawabana kuwa kama walivyo, kila mtu anawajibika alipo na akitaka kuvuka mstari kuna nguvu iliyopo inamrudisha anapostahili.

Ukiona Serikali nzima na Taifa kwa ujumla wanaishi kama manyani kwenye shamba la bibi, ama ufalme wa wanyama kwenye hifadhi, elewa nchi hiyo hakuna sheria inayowalazimisha kuishi kwa kufuata kanuni na taratibu na maisha hayo ya vurugu yanakuwa yanapendwa na walio wengi.

Tukiambiwa Katiba mpya pendekezwa ya Waryoba ama nyingine itakayofanana na hiyo kuwa ndiyo msingi wa sheria utakaotuweka vizuri, hakuna anayejali kwa kuona jambo hilo litapelekea kunyang'anywa matonge midomoni.

Maisha haya ya michongo hayatokei tu from no where, lazima kuna chanzo chenye mashiko.

Na mkitaka watu waishi kwa haki wasiishi kwa michongo inawezekana pia, ni maamuzi tu.
 
Back
Top Bottom