Mchongo wa Kompyuta za Sh milioni 132 huu hapa, Jokate Mwegelo ametumika

Mchongo wa Kompyuta za Sh milioni 132 huu hapa, Jokate Mwegelo ametumika

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
shue.jpg

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na asasi ya BRAC-Maendeleo, imetoa kompyuta 120 zenye thamani ya Sh milioni 132 kwa shule tatu za Wilaya ya Temeke kwenye mradi wa “Skills for Their Future”.

Kompyuta hizo zilikabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo, kwenye hafla iliyofanyika Machi 4, 2022 katika Shule ya Sekondari Karibuni iliyoko Chang’ombe, Dar es Salaam.

Shule zilizonufaika na msaada huo ni Miburani, Wailes na Karibuni.

Akizungumza kwenye tukio hilo, Jokate alisema makubaliano baina ya BRAC - Maendeleo Tanzania na TEA ni mfano wa namna taasisi za umma na zile zisizo za kiserikali au binafsi zinavyoweza kufanya kazi kwa pamoja katika kuboresha maisha ya wananchi.

Jokate alisema TEA inafadhili ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, mabweni, mabwalo na majiko yake, maabara na upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika ngazi zote za elimu Tanzania Bara na ngazi ya elimu ya juu kwa Zanzibar.

“Nichukue nafasi hii kuwasilisha shukrani za dhati kwa serikali kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania chini ya Mkurugenzi Mkuu, Bahati Geuzye. Temeke ni miongoni mwa Wilaya zinazonufaika na Miradi inayofadhiliwa na TEA,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye alisema mamlaka hiyo imeshakarabati shule kongwe 17 za sekondari kati ya 89 zilizopo katika mpango huo wa ukarabati na hivi karibuni ilishiriki kukarabati shule nne za msingi mkoani Dodoma.

Alisema kutolewa kwa kompyuta hizo ni uzinduzi wa mradi wa ‘Skills for Their Future’ unaolenga kutoa mafunzo ya kidijitali kwa vijana wa shule za sekondari ili kuwawezesha kupata ujuzi na stadi zitakazosaidia kuboresha maisha yao.

“Kompyuta hizi zinatolewa baada ya kusainiwa kwa makubaliano maalum ya ushirikiano baina ya TEA na BRAC-Maendeleo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono serikali wanafunzi kujifunza kupitia TEHAMA (teknolojia ya habari na mawasiliano) katika ngazi zote za elimu nchini,” alisema.

Alisema kompyuta hizo zitanufaisha wanafunzi 1,800 na walimu 45 na kwamba ni matumaini yao kwamba wanafunzi wa shule hizo tatu watatumia vizuri fursa ya miundombinu hiyo ya kompyuta kupata maarifa na taaluma zitakazowawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao.

Alisema walimu nao watatumia fursa hiyo kuboresha ufundishaji wa masomo na hivyo kusaidia shule zao kufanya vizuri kitaaluma na kwamba TEA inafarijika kuona wadau wa maendeleo kama BRAC wanatoa mchango wao kupitia mamlaka ya elimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa BRAC-Maendeleo, Suzan Bipa, alisema asasi hiyo imeichagua wilaya ya Temeke katika kutekeleza miradi mbalimbali na wameshirikiana na wilaya kutekeleza miradi mbalimbali ya elimu.

“Tunawashukuru viongozi wa wilaya hii kila tunapokuja kuanzisha mradi mpya mnatupokea vizuri na mnatupa ushirikiano mkubwa nawapongeza sana na tunafanya hivi kwenye maeneo mengi nchini,” alisema.

Alisema mbali na mradi huo wanatekeleza miradi mingine ya usalama na chakula uwezeshaji kwa vijana na wanawake na katika mradi huo wamefanya mambo mengi wilaya ya Temeke.


Chanzo: Nipashe
 
Utakuta ni computer za lak 6 kila moja ila hapo wakafanya kila moja milion moja na lak kama moja hivi, wakla 50% yao
 
Computer 120 kwa gharama ya Tsh mil 132, maana yake computer moja ni 1.1M
Tunaomba picha ya hizo computer na pia specification zake ziwekwe wazi!
 
halafu utakuta aliletewa documents haraka haraka akaweka sahihi bila kusoma ndani na kupata ushauri sahihi wa wataalamu wa ICT

anyway kila mbuzi ale urefu wa kamba yakee, mie saa ivi naenda onja Flying Fish mbili baridiii na kujazia na toti moja ya don
 
Ni wazo zuri na kongole kwa shule tajwa kwa kunufaika na msaada huo..Ila thamani ya hizo kompyuta kwa uelewa wa kawaida unaleta fikra kengeufu...132M kwa Computer 120 tena utakuta ni desktop sio mchezo asee
 
Hiyo pesa kubwa sana. Tunaomba specifications za hizo kompyuta tuhakikishe.
 
Hivi mnadhani Computer mpya intel processor unapata kwa sh ngapi?
 
Wangetoa madawati,vitabu,motisha kwa waalimu
 
Back
Top Bottom