Mchora katuni Opptertus John Fwema ashikiliwa na Polisi kwa Makosa ya Mtandao

Mchora katuni Opptertus John Fwema ashikiliwa na Polisi kwa Makosa ya Mtandao

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Cartoonist Oppter John Fwema anashikiliwa na polisi kituo cha Oysterbay. Nimeongea na mdogo wake na amenambia kuwa Oppter alikamatwa nyumbani kwake Bunju siku ya Ijumaa tarehe 3 September 2021kwa makosa ya mtandao. Taarifa zaidi zinaendelea kupatikana Polisi na kwa familia na tutajuzana zaidi.

Oppter anafahamika kwa katuni zake zenye ujumbe wa kukosoa serikali.

2ojspt.jpg

Mchoro wa Katuni uliomuingiza matatani

Screenshot_20211002-113622_Instagram.jpg

Ukurasa wake wa Instagram

129A538E-C9C4-4482-8DD6-6EDBF997C5E1.jpeg


=≈========UPDATE==========

Polisi wamezuia dhamana yake. Kwa mujibu wa ndugu na jamaa wanaofuatilia wamenijuza kuwa
Wanasheria nguli wamejitokeza kufuatilia sakata la msanii huyu.

Inawezekana uwepo wa wanasheria ukapelekea haki kutendeka bila kukiuka haki za mtuhumiwa.

Nitaendelea kuwajuza zaidi kadiri taarifa sahihi zinavyopatikana

===≈====== UPDATE ==========
02/10/2021
Mpaka naandika ujumbe huu, ndugu wanasema kesi imeshikiliwa na RCO, tangu amekamatwa hakuchukuliwa maelezo ambapo amehojiwa Alhamisi wiki hii.

Wanasheria wameshajitokeza kufuatilia haki za mchoraji huyu wa vibonzo.

===≈====== UPDATE ==========
04/10/2021
Wakili Msomi Jebra Kambole amejitolea kushughulikia suala la Mchoraji Optter Fwema.

Ameshawasiliana na ndugu wa mshikiliwa kwa ajili ya taratibu za kisheria.

Mashirika na majukwaa ya kimataifa wameanza kufuatilia na kuanzia leo sauti zitapazwa.

Wakili kutoka THRDC alikuwepo kituo cha polisi akaonana na mpelelezi wa kesi na Msanii Optter.

Polisi wamesita kumpa dhamana leo, wanasema faili limepelekwa kwa state attonery kisha kesho watampeleka mahakamani.


Msukumo wa kijamii umesaidia kiasi kikubwa kwenye hili kwa sababu hapo awali polisi waligoma kutoa ushirikiano na kingine hawakutaka jamii ijue anashikiliwa.

-------------SAHIHISHO------------

Watu wengi wanamfananisha mchoraji Optter na mwanavibonzo mwingine aitwaye Fredy ambaye alitumia sana kalamu yake kuwachora upinzani wakati wa uchaguzi

PIA, SOMA:
- Mchora katuni Oppter afutiwa kesi, akamatwa tena na polisi

VISA DHIDI YA WANAHABARI WENGINE WA TANZANIA:
 
Kipanya katuni zake huwa hazipo straight kama huyu, masudi anaficha maana sana ukiigundua unakua genius, sasa huyu ndugu anafungua code zote msomaji hapati tabu kufafanua

Sent using Jamii Forums mobile app
labda uko sahihi lakini naona tofauti yao zaidi ni kuwa kipanya ni maarufu hata akifinywa tunajua na huyu ndio anachipukia ndiyo maana imechukua karibu wiki kadhaa kujulikana aliko na hii ina maana kuwa hata humu jf kwa majina yetu yasiyo ya kweli unaweza potea na mtu asijue uliko kitu amabacho nikitisho cha uhuru wa kutoa maoni kama tulikimea wasiojulikana wakati wa Jpm kwanini tuna sugar coat wakati huu kujustfy vitendo viovu?

#free Cartoonist Oppter
 
Back
Top Bottom