Mchora Katuni wa Eritrea aachiwa huru baada ya kukaa gerezani miaka 15. Huenda wakina Soka watapatikana siku moja

Mchora Katuni wa Eritrea aachiwa huru baada ya kukaa gerezani miaka 15. Huenda wakina Soka watapatikana siku moja

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
Biniam Solomon, mchoraji katuni maarufu wa kejeli nchini Eritrea anayejulikana kwa jina la usanii Cobra, ameachiwa huru baada ya kukaa kizuizini kwa miaka 15 bila kufikishwa mahakamani.

Solomon alikamatwa mwaka 2011 jijini Asmara na tangu wakati huo hakuwahi kusomewa mashtaka yoyote wala kupata fursa ya kujitetea mbele ya jaji. Sababu za kuendelea kushikiliwa kwake kwa kipindi chote hicho hazikuwekwa wazi na serikali ya Eritrea.

Katika kipindi chote cha miaka 15, Biniam alikuwa amekatwa mawasiliano na familia yake. Taarifa zinaeleza kuwa alikuwa akipata matibabu ya nadra sana wakati afya yake ilipozorota. Hata baada ya kuachiliwa kwake hivi karibuni, mamlaka nchini Eritrea hazikutoa ufafanuzi wowote kuhusu sababu za kumwachia ama sababu za kumkamata hapo awali.

Maybe na akina Soka wako hai kuna siku tutawaona!

20260314_103949.jpg

Eritrean satirical cartoonist Biniam Solomon, also known by his pen name Cobra, has been released after spending 15 years in detention without charge in Asmara, Eritrea. Solomon, arrested in 2011, had never been tried. The reasons for his continued imprisonment were not made clear.

During his detention, Biniam had no contact with his family and received only occasional medical treatment. The authorities did not explain the reason for his release. Biniam was known for his sharp cartoons criticizing political and social issues. His work appeared in Eritrean newspapers during a brief period of media freedom.

The government closed the private press because it was "endangering national security", and several journalists were jailed. Human rights groups have long said Eritrea detained thousands of people without trial, allegations the government denies.

Source: All Africa
 
Ninasikitika tu kukueleza ni kuwa waliuwawa kikatili wale vijana.

Tangu tukio la Sativa kufeli na kurudi kuelezea umma A-Z ya yaliyomsibu , baada ya hapo wakimkamata mtu wanahakikisha wametenganisha kichwa na mwili na video wamechukua na kuwatumia maboss wao kuwa kazi imeisha, kushindwa kummaliza Sativa umeona matokeo yake baada ya kupona alivyowapeleka mchakamchaka.

Haki ya kweli kwa sasa ninaamini itapatikana katika visasi na kwa muda huu naipa timeline yake tujiandae kwa matukio kuanzia mwaka huu hadi 2028.
 
Nyie wajinga wajinga ndiyo maana tunasema mnatumika, kwa kujua ama kutokujua.

Hauwezi kulinganisha mtu kupotezwa na dalili zote kuonekana ameuawa na mtu kuwekwa kizuizini.

Nyie ndiyo mnakuja na story za Polepole kuwa Kigamboni ili watu waendelee kuwa na matumaini hewa ili siku ziende na watu wasahau. Hivi unategemea mtu kama Mdude wawe wanamlisha na kumpa chai kila siku wakati walishaonyesha kutaka kumuua zaidi ya mara moja?
 
Back
Top Bottom