Mchoraji wa katuni za Sokomoko

Mchoraji wa katuni za Sokomoko

doama

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Posts
808
Reaction score
650
[HASHTAG]#TANZIA[/HASHTAG]

Mchora katuni maarufu ya SOKOMOKO Thaddei Thomas Marealle, amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospital ya Kairuki.

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa kaka yake aitwaye William G Marealle Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Marehemu alijipatia umaarufu kupitia Katuni za Sokomoko zilizokuwa zikichapishwa kupitia gazeti la Sani lililojipatia umaarufu sana miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000

Kupitia gazeti hilo zilikuwepo katuni nyingine maarufu kama vile Kifimbo, Kipepe, Harakati a Pimbi, Ndumila kuwili, Lodi lofa, Madenge, Sukununu za babu Sani, Bush Star na Born Town.

RIP
FB_IMG_1515177654598.jpg
 
Kuna siku wife wa Sokomoko kaenda mbio mpaka katika kilabu cha pombe kamvuta Sokomoko toka ndani ya kilabu na kumwambia nyumbani pamevunjwa tumeibiwa soko akamuuliza je ile chupa yangu pale uvunguni ipo? mke akajibu yenyewe hawakuiiba. Basi Sokomoko tartiibu akamwambia mkewe kumbe wizi wenyewe mdogo tu huku akirudi kilabuni.
 
Jamaa alimkuta Sokomoko mferejini yupo bwiiii basi akaanza kumkojolea huku akisema ndio utaona leo Sokomoko akacheka sana kisha akamwambia ujue hapa nimelala penye mfereji wa haja kubwa.
 
Kuna siku wife wa Sokomoko kaenda mbio mpaka katika kilabu cha pombe kamvuta Sokomoko toka ndani ya kilabu na kumwambia nyumbani pamevunjwa tumeibiwa soko akamuuliza je ile chupa yangu pale uvunguni ipo? mke akajibu yenyewe hawakuiiba. Basi Sokomoko tartiibu akamwambia mkewe kumbe wizi wenyewe mdogo tu huku akirudi kilabuni.
hahahahahaha...
 
Mi nilidhan aliyekuwa anachora kina madenge, lodilofa, kipepe, sokomoko, nk ni mmoja
 
Back
Top Bottom