Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 761
- 1,464
Miaka ya 1990 mchoraji maarufu mwanamama Laura P raia wa US aliichukua picha orijino iliyopigwa na mpiga picha James Kidd katika mashindano ya kukimbiza farasi huko Tombstones, Arizona US na kisha akaichora ya kwake kama hiyo.
James alisema picha hiyo orijino aliyoipiga ilionekana kuwa na kitu ambacho wakati anaipiga hakikuwepo, kulionekana na mwonekano wa kama umbo la mtu lakini halikuwa na kichwa, ndipo mwanamama Laura Baada ya kupata habari hizi akaamua aichukue na kuchora yake kama hiyo.
Laura anasema alipomaliza tuu kuchora picha hiyo ule mwonekano kama wa mtu asiye na kichwa ukaonekana hata katika picha yake hiyo, wakati yeye hakuuchora. Hakujali.
Akaipeleka picha yake hiyo aliyoichora katika maonyesho kwa lengo la kuiuza, ajabu ni kua baada ya siku tatu akaitwa akaifuate. Mnunuzi anasema baada ya kuipachika ukutani ofisini kwake alianza kustaajabu kuona inajihamisha yenyewe, sahivi ipo ukuta huu, baadaye anaiona ipo ukuta ule.
Lakini pia alisema tangu aiweke tuu picha hiyo ofisini kwake documents nyingi ofisini humo zilikuwa zinapotea. Mchoro ukarudishwa kwa Laura mwenyewe ambapo alienda kuuhifadhi nyumbani alikokua anaishi na mumewe ambako mauzauza yaliedelea.
Laura anasema wakati Siku moja rafiki ake amemtembelea akamsimulia kuhusu picha hiyo, rafiki yake huyo alicheka sana kwa dharau kisha akaichukua. Kufika kwake akaiweka mezani, pale pale saa iliyokuwa ukutani ikaanguka na kupasuka, na ni saa iliyowekwa zaidi ya miaka 50 nyuma na haijawahi anguka.
Kuona hivyo akairudisha chap kwa Laura, Laura akaichoma siku hiyo hiyo. Tazama vizuri mchoro huo upande wa kushoto.
.
.
.
Written by Military Genius
Sent using Jamii Forums mobile app