Mchoro wa picha ya ndala unamaanisha nini kwa klabu ya Yanga?

Mchoro wa picha ya ndala unamaanisha nini kwa klabu ya Yanga?

King Mukhil

Member
Joined
Oct 15, 2017
Posts
14
Reaction score
7
Nimekuwa nikiona mchoro wa picha ya ndala pale timu ya Dar es Salaam Youngs Africa inapoandikwa katika magezeti kama alama ya uwakilishi wa timu hiyo.

Kama mpenzi wa klabu ya Yanga na soka la Tanzania kwa ujumla nashindwa kuelewa picha ya ndala inawakilisha ujumbe gani kwa klabu hiyo.

Lakini zaidi ya yote asili yake ni nini na waandishi walianza lini kutumia kama lugha ya picha kwa vijana hao wa Jangwani?

Naomba kupata uwelewa wa hili.

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Ndala hua siku zote inavaliwa miguuni na kukanyagwa tu kama vile hio tilmu ya Yanga inavokanyagwa mara kwa mara
Hio ndio maana halisi ya Ndala[emoji1321]
 
Nimekuwa nikiona mchoro wa picha ya NDALA pale timu ya Dar es salaam Youngs Africa inapoandikwa katika magezeti kama ALAMA ya uwakilishi wa timu hiyo..
Kama mpenzi wa klabu ya YANGA na soka la Tanzania Kwa ujumla nashindwa kuelewa picha ya ndala inawakilisha ujumbe gani Kwa klabu hiyo.
Lakini zaidi ya yote asili yake ni nini na waandishi walianza lini kutuimia kama lugha ya picha kwa vijana hao wa jangwani..?
Naomba kupata uwelewa wa hili..

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
Ndala hukanyagwa mkuu.
 
Picha ya ndala inawakilisha makabwela aka wanyonge kwa mujibu wa JPM, hii ilitokana na mgogoro uliozuka kwenye klabu hiyo ambapo kuna kundi moja lilikuwa ni watoto wa mjini enzi hizo walijiita RAISONI huku lile kundi lingine la wananchi wa kawaida wakiliita KANDAMBILI / NDALA (wananch wa kawaida si unajua walikuwa wanavaa NDALA wakati wenye nazo wanavaa viatu vya maana enz hizo RAISON)...mwisho wa siku wenye timu yao walichua timu (wenye NDALA)
 
Nimekuwa nikiona mchoro wa picha ya NDALA pale timu ya Dar es salaam Youngs Africa inapoandikwa katika magezeti kama ALAMA ya uwakilishi wa timu hiyo..
Kama mpenzi wa klabu ya YANGA na soka la Tanzania Kwa ujumla nashindwa kuelewa picha ya ndala inawakilisha ujumbe gani Kwa klabu hiyo.
Lakini zaidi ya yote asili yake ni nini na waandishi walianza lini kutuimia kama lugha ya picha kwa vijana hao wa jangwani..?
Naomba kupata uwelewa wa hili..

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
Manake Ndala yake Chooni tu
 
weka picha bhana,
IMG_20171015_162108_973.JPG
 
Back
Top Bottom