Si tetesi tena bali ni uhakika kuwa Tundu Antipasy Mghway Lissu (Makamu Mwenyekiti taifa wa sasa) atapambana na wenzake wawili kuwania nafasi ya uenyekiti taifa - CHADEMA...
Mwingine aliyekwishajitokeza ni mwanachama mmoja ajulikanaye kwa jina Odero C. Odero. Na wa tatu japo hajasema waziwazi lakini ni wazi kuwa atawania ni mwenyekiti wa sasa Ndugu Freeman Aikael Mbowe.
Mwandishi wa habari na mchambuzi nguli wa mambo ya kisiasa anayeishi uhamishoni Uingereza ndugu Ansbert Ngurumo katika video hii fupi ya dakika kama 7 hivi anauchambua mchuano huu.
Ansbert Ngurumo anasema: Lissu na Mbowe, chuaneni lakini epukeni tabia ya mtungi.
Your browser is not able to display this video.
Je, wewe unaujua mtungi? Na unazijua tabia za Mtungi?
Tundu Lissu kuwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ni jambo ambalo watawala na Dola hawatapenda kulisikia. Ni heri kwao Tundu Lissu awe waziri wa wizara yoyote kuliko kuwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani.
Ikitokea hivyo Maza hatalala na atajiengua kwenye uchaguzi wa mwakani mapema kama Biden