Wazambia wanatarajiwa kupiga kura August 13 katika uchaguzi mkuu wa urais unaotajwa kuwa kipimo kikubwa cha mageuzi ya kiuchumi ya serikali iliyopo madarakani dhidi ya ugumu wa maisha unaowakabili raia wa kawaida.
Rais Hakainde Hichilema (UPND), aliyeingia madarakani mwaka 2021 na kusifiwa na taasisi za kimataifa kama IMF kwa kupunguza madeni na kukuza uchumi, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Brian Mundubile (NRPUP) anayeongozana na muungano wa vyama vya upinzani.
Soma zaidi:Zambia yasitisha Kodi (VAT na Excise Duty) kwenye Mafuta kupunguza makali ya maisha
Licha ya jitihada za serikali za kurejesha utulivu wa kiuchumi, wapigakura wengi—hasa vijana waliotawala orodha ya zaidi ya wapigakura milioni 8.7 waliojisajili—wanalalamikia kupanda kwa gharama za maisha, bei za chakula, na ukosefu wa ajira.
Huku kukiwa na matukio machache ya mivutano ya kisiasa na tuhuma za kikwazo cha kampeni kutoka kwa upinzani, matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa ifikapo Agosti 17, ambapo mgombea anahitaji kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura ili kutangazwa mshindi wa moja kwa moja.
Source:Africanews