Mchuano wa kisiasa Moshi kati ya makada wawili wa Chama cha Mapinduzi, Priscus Tarimo na Ibrahim Shayo

Mchuano wa kisiasa Moshi kati ya makada wawili wa Chama cha Mapinduzi, Priscus Tarimo na Ibrahim Shayo

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Kuna mchuano mkali sana unaendelea kwenye siasa za mjii wa Moshi ambako makada wawili wa Chama cha Mapinduzi, Priscus Tarimo (mbunge)na Ibrahim Shayo a.k.a Ibra Line kuelekea uchaguzi Mkuu hapo mwakani.

Mchuano huu umekolea hasa kwenye magroup ya WhatsApp ambako Ibra Line amepewa jina jipya la Kaka wa 'Jimbo 'ukiwa ni makakati wa kumpromoti kisiasa.

Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani joto la kisiasa linazidi kupanda ndani ya chama cha mapinduzi japo pazia baado kabisa halijafunguliwa.

Wachambuzi wa siasa za moshi wanabainisha kuwa mchuano huu hautapoa hadi kelekea kura za maoni ndani ya chama.

"Nikuhakikishie kaka kazi ndo bado kabisa haijaanza hiki kinachoendelea ni mvua za rasharasha tu lakini muda utaongea"anasema mtu wa karibu wa kaka wa Jimbo

"Hebu nikuuliza huyu kaka wa Jimbo ndo nani ,anamiliki Jimbo gani la uchaguzi,kwa nini mnampa umaarufu sana?muda utaongea",anasema mtu wa karibu na Priscus Tarimo.

Miamba hii miwili Mwaka 2020 ilichuana vikali kwenye kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi Katika kuwania kuteuliwa na Chama cha kupeperusha Bendera ya chama.

Walioko karibu na kaka wa 'Jimbo 'wanasema 2020 matokeo ya kura za maoni yalichakachuliwa yakamnyima ushindi lakini walioko upande wa mbunge Priscus Tarimo wanapuuza madai hayo.

Nini kitatokea mwakani je ni Priscus Tarimo tena ama ni Kaka wa 'Jimbo'?,acha tusubirie muda ufike.
 
Wanamlia tu hela zake. Hayo ni majina ya kumlainisha atoe chochote kitu.
 
Back
Top Bottom