Mchubuo wamzalishia talaka Bi harusi...

Mchubuo wamzalishia talaka Bi harusi...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Mchungaji kapera hakuacha kuangaza-angaza macho
Kwenye kwaya ya kanisa lake akajionea kitoweo murua
Binti sura nyororo na rangi yake ni hudhurungi bila karaha
Mchungaji kuona hivyo akaambuliwa suluba ya mahaba tele
Mchubuo wa Bi harusi wamzalishia talaka yenye simango kibao!

Binti sura yawaka lakini mwili wake kaufunika gubigubi la ushungi
Wengi waliamini hayo ni maadili ya malezi bora aliyolelewa nayo
Kumbe yeye ana lake jambo na siri kubwa alikuwa anaisetiri
Hata umakini wa mchungaji haukufua dafu na mkenge kuingizwa
Mchubuo wa Bi harusi wamzalishia talaka yenye simango kibao!

Hayawi hayawi huwa, mchungaji akabeba chake bila ya mikwara
Siku zikawa siku na Bi harusi kukwepa majukumu yake ya kitandani
Visingizio kibao hasa majukumu kuwa ndiyo ghala la utetezi wake
Asubuhi kudamka mapema na usiku kuchelea kulala akificha utupu wake
Mchubuo wa Bi harusi wamzalishia talaka yenye simango kibao!

Za mwizi ni arobaini na zilipofikia aliona cha moto kikimwakia
Siri ikaanikwa hadharani kumbe mambo yote ni mchubuo!
Mchungaji akajawa na hamaki asiamini alivyonyimwa unyumba
Ama kwa hakika tatizo ni matarajio ya mchungaji kuyumbishwa
Mchubuo wa Bi harusi wamzalishia talaka yenye simango kibao!

Jisomee Mchubuo wa Bi harusi wamzalishia talaka yenye simango kibao
 
lololol! RUTTA leo nimekukumbuka kweli na haya mashair kumbe i was calling you thanks god you heard me.
[MENTION]
gfsonwin[/MENTION] yeah back in business....
 
sijaelewa kitu, mchubuo?

Kongosho nimekubandikia uzi wa kisa chote hiyo tenzi ni ufupisho wake tu labda jisomee utapata khabari yote...............
 
Last edited by a moderator:
wallahi!!! nilitaka kupeleka uzi chitchat kuuliza kijana wa mashairi kaishiwa nini nimpe idea, by the way mchugaji bwana naye feki sa inakuaje anachukua mchumbuo wakati brandnew zipo au alizidiwa maunjanja?
 
ummu kulthum au ni kusakazie huyo mchungaji nini yuko Kenya............na sasa hivi boma lake liko tupu tu..........
 
Last edited by a moderator:
Jamani sio kila king'aacho ni ..........! ndiyo maana siku hizi tumezinduka "TEST before TAKE"
 
Jamani sio kila king'aacho ni ..........! ndiyo maana siku hizi tumezinduka "TEST before TAKE"

Kyaiyembe huyu mchungaji hamjui Muumba ya kuwa kamwagiza ukisha beba mali yako hakuna kuitelekeza labda kwa sababu za uasherati............
 
Last edited by a moderator:
Kyaiyembe huyu mchungaji hamjui Muumba ya kuwa kamwagiza ukisha beba mali yako hakuna kuitelekeza labda kwa sababu za uasherati............
Wote Mchungaji na Kondoo wake walisoma kitabu kimoja tu katika BIBLIA nzima "WIMBO ULIO BORA".
Hivyo mengine kuhusu mahusiano katika BIBLIA hayakuwahusu!
 
"For the first week, I thought she was shy and still adjusting to marriage life because we were yet to consummate our marriage," the pastor explained.
Mkuu
Rutashubanyuma
unisaidie kidogo kwa taratibu za ndoa (hasa za kikristo).
Hawa walikuwa wana ndoa kweli au ilikuwa bado haijafanyika?
 
“For the first week, I thought she was shy and still adjusting to marriage life because we were yet to consummate our marriage,” the pastor explained.
Mkuu
Rutashubanyuma
unisaidie kidogo kwa taratibu za ndoa (hasa za kikristo).
Hawa walikuwa wana ndoa kweli au ilikuwa bado haijafanyika?

Kyaiyembe...jamaa alikuwa kishaoa, shughuli ilikuja wakati wa ku consummate hiyo kitu sura mirinda miguu pepsi
 
Last edited by a moderator:
Kyaiyembe...jamaa alikuwa kishaoa, shughuli ilikuja wakati wa ku consummate hiyo kitu sura mirinda miguu pepsi
Nina wasiwasi kidogo hebu soma hapa;
But one night, he went to bed before her as usual but he was troubled so sleep evaded him.
Thinking that the husband was fast asleep, she went to the bedroom and undressed.
But before she could sneak into bed, her husband, who was fully awake, switched on the light to surprise her. To his shock, his ‘light-complexioned’ wife was dark in complexion, except for her face, part of her arms and legs.
“You bleached your face? Is this why you are always wearing long dresses?” the shocked pastor asked.
NAdhani huyu pastor ni KONDOO wa ukweli na sio KONDOO mcha MUNGU!.
 
"For the first week, I thought she was shy and still adjusting to marriage life because we were yet to consummate our marriage," the pastor explained.
Mkuu
Rutashubanyuma
unisaidie kidogo kwa taratibu za ndoa (hasa za kikristo).
Hawa walikuwa wana ndoa kweli au ilikuwa bado haijafanyika?

Kyaiyembe ni ndoa hiyo kwenye ukristu kuoana siyo lazima mfinyangane siku au wiki hiyohiyo..............wakati mwingine mazingira yanawabana mjizuie...tena inakubalika zaidi kama mm'eamua kufunga hilo swala............lol
 
Last edited by a moderator:
Kyaiyembe...jamaa alikuwa kishaoa, shughuli ilikuja wakati wa ku consummate hiyo kitu sura mirinda miguu pepsi

[MENTION]Lemonade[/MENTION] ni kweli bi harusi alikuwa akikimbia mechi kwa kuhofia asije julikana yeye ni tetracycline..........sura ni nyingine na kiwiliwili ni sura nyingine.....................lakini alikuja kutiwa kitanzini
 
Nina wasiwasi kidogo hebu soma hapa;
But one night, he went to bed before her as usual but he was troubled so sleep evaded him.
Thinking that the husband was fast asleep, she went to the bedroom and undressed.
But before she could sneak into bed, her husband, who was fully awake, switched on the light to surprise her. To his shock, his ‘light-complexioned' wife was dark in complexion, except for her face, part of her arms and legs.
"You bleached your face? Is this why you are always wearing long dresses?" the shocked pastor asked.
NAdhani huyu pastor ni KONDOO wa ukweli na sio KONDOO mcha MUNGU!.

Kyaiyembe upo sahihi kama alijichubua uso wake alichotakiwa ni kumwambia sasa aache kwani kesha pata mume...........na ndoa za kikstristu hakuna talaka bali kwa sababu za zinaa tu.........
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom