Mchujo TFF:Ali Mayai apeta,Malinzi afungaishe

Mchujo TFF:Ali Mayai apeta,Malinzi afungaishe

hivi malinzi alishawahi kucheza hata mpira wa makaratasi tu?
 
MCHUJO UCHAGUZI MKUU TFF

Wakati majina 73 yakipita katika hatua ya awali,mgombea tishio Ali Mayai amepita kihunzi hicho. Mwanasoka Ali Mayai wamekuwa akiiundiwa mazengwe na timu ya fitna ya Malinzi ambayo imekosa sababu za kuendelea uongozini.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imechuja jina la Abdallah Mussa katika orodha ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao wa shirikisho. Sababu za kukata jina la Mussa ambaye alikuwa anawania nafasi ya Ujumbe kutoka Kanda Na. 1 ya mikoa ya Kagera na Geita ni kutoambatanisha kivuli cha cheti cha kidato cha nne kwa mujibu wa kanuni ya 9 inayozungumzia sifa nane za kuwania uongozi TFF. Katika majina hayo 73, majina 10 ni wale wanaowania urais, makamu rais sita na wajumbe wa kamati ya utendaji 57.

Wagombea wote hapo juu wanatakiwa kufika kwenye usaili utakaofanyika kuanzia Juni 29, 2017 hadi Julai 1, mwaka huu katika ofisi za TFF Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 4.00 asubuhi wakiwa na nyaraka halisi za viambatisho vyote walivyoweka kwenye fomu za maombi. Vyeti vya elimu ya Sekondari viwe vya Baraza la Mitihani (NECTA
Usaili uwe live kwenye TV
 
Katika pita pita zangu,rada yangu imenasa ya kuwa malinzi anarudi kama rais wa tff na makamu wake ni wambura,tusubiri muda ndio utaoongea
 
Alivyotoka tenga Fifa tulikua nafasi ya ngapi na sasa tupo nafasi ya ngapi?
Narudia tena malinzi hafai kuendelea
Kweli wewe ni Ng'ombe uliekatwa mkia,eeh Tenga alituletea kikombe gani au tulishiriki michuano gani mikubwa zaidi ya nafasi za FIFA.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Alivyotoka tenga Fifa tulikua nafasi ya ngapi na sasa tupo nafasi ya ngapi?
Narudia tena malinzi hafai kuendelea
Unafikiri Tenga alikuwa anamlipa Maximo fedha kutoka mfukoni mwake?
Mshukuru Kikwete alipenda michezo

Halafu kipindi hicho hatukuwa tunaaibishwa na watu walioshindwa uwanjani halafu wanaandika barua za kuomba ubingwa mezani...
 
Tenga alifanya nini cha maana kumzidi Malinzi?

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
Tenga alijenga shirikisho lenye kufata sheria na taaluma, likijumuisha wataalamu mbalimbali,sio TFF ya malinzi haina tofauti na club za simba na yanga uendeshwaji wake, makomandoo kibao na fitna tupu
 
Back
Top Bottom