Mchujo TFF:Ali Mayai apeta,Malinzi afungaishe

Mchujo TFF:Ali Mayai apeta,Malinzi afungaishe

Kuna vipambe vya malinzi tangu asubuhi vimekomaa kumtetea jamaa yao na kumponda Mayai, vimekenua asubuhi vilipodanganyana eti Mayai amekatwa basi vikajifanya vinajua sheria za uchaguzi za tff sasa bado vinahangaika hapa.
kama jamaa yenu yupo vizuri si mtulie apambane kwenye sanduku la kura?
 
Mwenyekiti wa sasa wa CAF kabla ya uchaguz alibezwa kama anavyobezwa Ally Mayai Tembele.
 
Figisufigisu zimebuma naona...

Hashtag ni ileile [HASHTAG]#malinzimustquit[/HASHTAG] [HASHTAG]#malinziout2017[/HASHTAG]
 
Kama sikosei Ali mayai tembele alipata 0 form 4 cheti atatoa wapi?
 
Malinzi angekuwa mungwana angejiuzulu hiyo nafasi maana huu upepo sio umechafuka upande cha ajubu bado anataka kuendelea viongozi wetu wanashindwa kusoma nyakati
 
Before we know TFF will become Kagera Star...kuanzia mfagiaji mpaka boss wote watakuwa jamaa wanyumbani
 
Kuja mtu anatokwa na povu humu atakuwa katumwa aje aangalie upepo na huku,,,,,,kamwambie hamtumtaki sio ngumi hapa
 
MCHUJO UCHAGUZI MKUU TFF

Wakati majina 73 yakipita katika hatua ya awali,mgombea tishio Ali Mayai amepita kihunzi hicho. Mwanasoka Ali Mayai wamekuwa akiiundiwa mazengwe na timu ya fitna ya Malinzi ambayo imekosa sababu za kuendelea uongozini.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imechuja jina la Abdallah Mussa katika orodha ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao wa shirikisho. Sababu za kukata jina la Mussa ambaye alikuwa anawania nafasi ya Ujumbe kutoka Kanda Na. 1 ya mikoa ya Kagera na Geita ni kutoambatanisha kivuli cha cheti cha kidato cha nne kwa mujibu wa kanuni ya 9 inayozungumzia sifa nane za kuwania uongozi TFF. Katika majina hayo 73, majina 10 ni wale wanaowania urais, makamu rais sita na wajumbe wa kamati ya utendaji 57.

Wagombea wote hapo juu wanatakiwa kufika kwenye usaili utakaofanyika kuanzia Juni 29, 2017 hadi Julai 1, mwaka huu katika ofisi za TFF Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 4.00 asubuhi wakiwa na nyaraka halisi za viambatisho vyote walivyoweka kwenye fomu za maombi. Vyeti vya elimu ya Sekondari viwe vya Baraza la Mitihani (NECTA
Malinzi amewaweka line up ya wapiga kura wake siku nyingi either by corruption or not! Na atashinda unless kuwe na nguvu tofauti like involving TAKUKURU otherwise jamaa atashinda asubuhi mapema
 
Back
Top Bottom