LD
JF-Expert Member
- Aug 19, 2010
- 3,014
- 578
Wapendwa habarini za Ijumaa, natumaini, mnayo Ijumaa nzuri yenye furaha na amani.
Hata wale ambao wanaiona sio nzuri kwa sababu mbalimbali, bado tuendelee kumshukuru Mungu madamu ametuachia uhai na afya.
Kuna jambo nimeliona katika jamii inayotuzunguka, nikafikiria halafu nikaona tushirikishane mawazo mawili matatu huku tukisubiria jioni yenye baraka!!
Ni hiviii!! Nimekuwa nikiona katika jamii binti anapoolewa na kuachana na wazazi wake, na kuungana na mume wake, na kuwa mwili mmoja, wanaishi kwa pamoja wakisaidiana katika raha, milima na mabonde na maisha yanaendelea. Na Mwanaume kadhalika ana achana na baba na mama yake...................
Lakini inapotokea labda binti amepata tatizo la ugonjwa, utakuta ndugu zake wa damu, yaani mama, dada zake, kaka zake ndo wanajitokeza na kuchukua majukumu ya kumsaidia zaidi. Labda kumpa huduma hospitalini, kumuuguza nk nk..
hata kama mume wake yupo na ndugu wa mume wake yupo.
Wakati mwingine hata huyu mwanaume anaweza asihusike sanaaaa ktk jambo hilo, au akahusika kidogo tu. Na kuna wakati inabidi yule mgonjwa (Binti) apelekwe kwa wazazi wake au kwa ndugu zake wa damu kuuguzwa, mpaka atakapona anarudi kwa mume wake.
Wakati mwingine hata binti akijifungua, atapenda zaidi kuhudumiwa na mama yake mzazi au ndugu zake wa damu, kuliko mama mkwe na ndugu wa mume wake.
Kingine nilichokiona mwanaume aliyeoa, yeye akipatwa na matatizo kama hayo atahudumiwa kwa kiasi kikubwa na mke wake. Na hata kama alikuwa ni mkorofi kwa mke wake, pengine amehamia hata nyumba ndogo, lakini ikifika kwenye ugonjwa anahamia kwa mke wake, na mke atampokea, atamuuguza na kumtunza mpaka atakapopona au atakapoenda huko ambako hakuna hiari..............
Sasa basi, ni kweli kwamba wazazi na ndugu zetu mabinti/wanawake wanahusika na sisi ktk matatizo na shida zetu kwa kiasi kikubwa hata kama tumeolewa?
Je ni kweli kwamba nyumbani kwetu ndio kichaka cha matatizo yetu?
Kwa nini mwanaume akipata tatizo anatafutwa mke wake anahusika zaidiiiiiiiii kuliko mama yake na ndugu zake wa damu?
Kama ndo hivo, basi kina dada tuna kila sababu ya kuwajali ndugu na jamaa zetu kwa sababu kila janga tunalolipata tunakula nao pia.............!!!!