Mchuma Janga hula na Wakwao - The Case of Corona and Social Distancing

Mchuma Janga hula na Wakwao - The Case of Corona and Social Distancing

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
17,572
Reaction score
27,416
Ukitaka maji utakwenda Kisimani na Ukitaka Mchicha utakwenda Shambani…, Sidhani kama itakuwa busara kuomba ushauri wa kiimani kwa daktari, vilevile busara itakwambia mambo ya kiafya huenda mchungaji au mtu wa Imani asiwe sahihi kuliko daktari kwa ushauri muafaka. Wataalamu wa Imani ni madaktari wa roho kwa kuwapa watu amani na kuepusha panic, kuwafanya wasife moyo n.k.

Uzuri hayo yote wanaweza kuyafanya kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa hili gonjwa ambao ni wataalamu wa afya na ushauri wao unasema social distancing, na kuepuka misongamano, huenda kweli wapo wale ambao damu ya Yesu inawaponya ila sidhani kama wamejiuliza kwa mikusanyiko yao wakichukua huo ugonjwa huko na kuupeleka mitaani wale ambao sio waumini pia watakuwa na kinga au la!!!, In this day and age ya teknolojia wanaweza kuendesha na kutibu roho za waumini kwa njia ambazo haziitaji mikusanyiko.., watu wamefunga shule kuepuka misongamano alafu watoto hao unawakuta wamesongamana kwenye hizi ibada.., Vilevile hawa watu wa Imani wakumbuke pia Malaria inatuangamiza sana watu wa tropics kuliko hata hii Corona wasisahau kuombea na hii malaria nayo itokomee…, ila wavute Subira kwanza wale ambao Mungu amewalaani ingawa hawalali kwa kutafuta chanjo wapate kwanza chanjo ili tuendelee na mikusanyiko na maombi…

When push comes to shove mwisho wa siku chakula ndio cha muhimu kwa binadamu, kwahio si vibaya watu tukaweka stock ya chakula na sababu huwezi ukala vyakula vingine bila kupika kwa kuhitaji fuel ni vema kwa sasa chakula kipo kingi tukakumbuka mababu zetu walifanya nini (pickling) au watu wa Korea kwa kutengeneza Kimchi (fermented vegetable) ambayo inaweza kukaa miaka bila kuharibika (kwanini ufanye hivyo ?) ikitokea ya India ya kuambiwa usitoke nje atleast utakuwa na cha kuweka tumboni na hautakufa kwa njaa

Peace

Tuendelee kuombeana kila mtu kwa nafasi yake na kuwapa moyo wataalamu sababu wao ndio watatutoa kwenye hili janga…
 
Wanataka sadaka zetu tu. Sisi raia hatuna pakumulia Magu anataka Kodi huku kwa Makanisa nao wanataka Kodi( sadaka) yaani unajikuta kila unachoingiza unawatafutia wao tu na wanao.
 
Wanataka sadaka zetu tu. Sisi raia hatuna pakumulia Magu anataka Kodi huku kwa Makanisa nao wanataka Kodi( sadaka) yaani unajikuta kila unachoingiza unawatafutia wao tu na wanao.
Sadaka zetu wachukue kwa M-Pesa, bila kutuweka katika hatari ya Corona, mtu mmoja tu anaweza kwenda kuchuma hili janga na kutuletea mtaani balaa,,,,
 
Back
Top Bottom