Mchumba kakataa kuongea na mimi kwenye simu aliyopelekewa na mama yangu

Mchumba kakataa kuongea na mimi kwenye simu aliyopelekewa na mama yangu

sychellis

Senior Member
Joined
Oct 16, 2018
Posts
149
Reaction score
138
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 nasoma Chuo Degree Mwaka wa Pili, kuna binti mmoja mama yangu alinambia ni mzuri ana tabia nzuri, sema mimi nikawa napotezea sikuwa na haja hiyo. Siku moja nilienda kumsalimia mama nikamuona huyo binti, jamani ni mzuri balaa. Yeye baba ni Mzanzibar na mama ni msukuma pia huyo binti anasoma Form Five.

Baba yake kashafariki anaishi na mama na ndugu zake tu, kiufupi nilitokea kumpenda sana hususa likizo nilienda kukaa kwa mama nilipata mda wa kumjua zaidi tukajenga mazoea kiukweli nilitamani na ninatamani aje kuwa mke wangu nipange nae maisha. Ikabidi nimueleze kuwa nampenda na natamani tuje tuishi wote hakunipa jibu lolote miezi ikapita si chini ya mitano ila siku moja nilimueleza kwa hisia kali huku nikiwa na uzuni sana cha ajabu alinikumbatia sana huku akiwa anaaniuliza unanipenda kweli? Nikamwambia ndiyo nikamuuliza na yeye akanambia ndiyo.

Basi kuanzia hapo akawa official mchumba angu bila mtu yeyote kujua na wala mama sikumwambia. Sasa tatizo likaja siku moja nilikua niko kwao nikawa nimemuegamia hivi ghafla mama yake akatokea yule binti akanitoa haraka alafu akanipiga kikofi hivi sasa mama yake aliona wakati ananipiga kwaiyo ikabidi amuite binti yake alimgombeza sana ila mimi hakuniita kesho yake yule mama akamwambia dada wao wa kazi aniambie mimi nisiingie tena ndani kwao basi mimi nikaona fresh.

Tukawa tu tunaonana tunaongea kama kawaida, yule mama namsalimia anitikia fresh tu mule ndani kwao nikawa siendi mpaka yule mama aniite na alikua aniniita akiwa na shida ya jambo. Sasa now nikaamua nikakae hostel, kwahiyo majuzi nikampigia simu mama yangu nikamsalimia nikamuulizia yule binti hajambo mama akanambia hajambo, nikamwambia naomba niongee naye akanambia ngoja niende kwao nikamwite.

Mama akaenda akamwita akamwambia mtu fulani anataka kuongea na wewe cha kushangaza yule binti akawa anasema mh mh mh anakataa ile ya kuguna mama akawa anashangaa anamwambia wewe ongea nae tu kwani kuna tatizo gani? Akawa anasema mh mh we acha tu mama fulani. Basi mama yangu ikabidi aondoke akaniambia amekataa mimi nikasema sawa.

So wakuu naomba mnishauri niachane naye tu huyu binti japo kikweli ninampenda na nina tamani nije nimuoe huyu binti ila nikifikiria hii situation iliyotokea alafu mama yake mswahili kichizi yani. Sema binti ni mzuri wa sura mpaka tabia. Ushauri wakubwa
 
Sasa kuguna guna ndio inakuletea mashaka kiasi hicho
Nenda ukutane nae Huy mtu wako muongee uso kwa macho

Pengine alikua anaona aibu kuongea na Wewe kwenye simu ya Mama yako
 
Daah hii post imejaa utoto kabisa


Halafu dogo mambo gani unaleta hayo unataka uongee na demu wako kwenye simu ya maza ako kabisa tena unamuagiza kabisa akakuitie uongee nae halafu bi mkubwa anaenda kwa nyumba ya binti kabisa kisa kijana wake anataka aongee na binti hvi wazaz wake watawachukuliaje we mwenyewe hutambuliki na binti ndo kwanza mwanafunzi mbona hii haijakaa sawa haingii akilini au uzungu mwingi


Anyway Mimi ni nani ni judge hamna shida hapo ondoa shaka binti muoga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah hii post imejaa utoto kabisa


Halafu dogo mambo gani unaleta hayo unataka uongee na demu wako kwenye simu ya maza ako kabisa tena unamuagiza kabisa akakuitie uongee nae halafu bi mkubwa anaenda kwa nyumba ya binti kabisa kisa kijana wake anataka aongee na binti hvi wazaz wake watawachukuliaje we mwenyewe hutambuliki na binti ndo kwanza mwanafunzi mbona hii haijakaa sawa haingii akilini au uzungu mwingi


Anyway Mimi ni nani ni judge hamna shida hapo ondoa shaka binti muoga

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtoto wa mama


Sent from my iPhone using Tapatalk Pro
 
Shida si uchumba shida aina ya maandishi na uhusishwaji wa bi mkubwa sasa.
Za masiku bibie?
Watu walivyochamba sasa utadhani wao walivyokuwa na miaka 22 hawakuwa na wachumba
 
22 + 30 = 52 dah mzee unataka kulia ujana wako korokoroni ukitoka tu na mchumba wako kaolewa na watoto 6 soma achana na mapenzi
 
Back
Top Bottom