Mchumba kakataa kuongea na mimi kwenye simu aliyopelekewa na mama yangu

Mchumba kakataa kuongea na mimi kwenye simu aliyopelekewa na mama yangu

Hahahaaa umesema una miaka mingapi tena?

Nakushauri pambana na masomo achana na hayo mambo kwa sasa maana inaonekana bado akili haijakomaa hayo mambo yatakusumbua na yanaweza kukuharibia masomo.
 
Hahahaaa umesema una miaka mingapi tena?

Nakushauri pambana na masomo achana na hayo mambo kwa sasa maana inaonekana bado akili haijakomaa hayo mambo yatakusumbua na yanaweza kukuharibia masomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
nashkuru na mimi nimeamua niachane na ayo mambo tu yatanichanganya kweli
 
Nimegundua yafuatayo kuhusu miguno yake
1. Mchumba wako Hana simu na kapigwa marufuku kumiliki simu (yaani anachungwa)
2. Wakati anapelekewa simu inaonesha kulikuwa na mzazi wake ndani ya nyumba ambaye huenda ni Mama yake.
3. Mama yako kumwambia azungumze na wewe eti hakuna tatizo (Hakuna tatizo kwenu ila kwake kuongea na simu Kuna tatizo endapo angefumwa akiongea na simu)

KUWA NA AMANI, KUKU BADO NI WAKO MANATI YA NINI. Bado anakupenda ila ndo Kama hivo.
 
Kitu nilichogundua ndugu zangu Wanaume tunakazi kubwa sana ya kuwa baba kwa vijana wetu with all respect kwa single mothers lakini kuna sehemu panapungua Hebu angalia mtu wa second year yuko anajaribu kuoa mtu wa form five na mama yuko anatoa sapoti ya hela yote
 
Komaa umalize chuo upate kazi. Mke atakuja mwenyewe.
Kuku wako manati ya nini.
 
Dogo una miaka 22,
Mwanafunzi,
Huna mbele wa nyuma,
Unakaa kwenu,
Huna ajira.
SWALI:
Huyo mke unayemtaka utamlisha nini?
Kwanini unamgeuza mama yako kuwa kuwadi wa kukuunganishia demu?
Hivi unajua binti wa form five ni mdogo sana kuingia kwenye ndoa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto na mama ahaaa, ila si mbaya, kama unempenda mnunuie simu wacha kumsumbua mama. Afu soma mwaka wa pili ngumu sana.
 
Yani chuo mwaka wa pili kabakiza mwaka mmoja atunukiwe degree huyu.

Pumbavu kabisa
Itabidi hap JF tuanze kutembeza bakoraz
Shwaini.

Bi mdashi anahangaishwa bure utadhani kazaa dafu kubabeki
Mimi sijamaliza kusoma. Yani daaah vijana wa siku hizi hasara tupu.

Mwaka wa pili chuo unafanya utoto namna hii. Alafu hao wazazi nao...hamna kitu.


Huyu jamaa dem kashamuona fala. Atakuja msela badboy atamgonga huyo dem

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaha dahh corona iishe mrud shule sasa unataka ushauriwe nn apo iv unajua maana ya mchumba ww [emoji23][emoji23]
 
Mfundisheni dogo afanye nini ili mambo yaende poa kuliko kumpiga vijembe. Ninyi ndio mabroo kama anakosea akamwambie nani? Inawezekana yeye ndio first born hana mshauri wa namna ya kuapproach. Mpeni maarifa mdogo wenu. Namsifu sana dogo kuchukua hatua za awali, ila kuna point unakosa mawazo na ndio hapo akaona atumie simu ya bimkubwa wake.

Asipotongoza mtamwita shoga. Mpeni maujanja sio kuponda kila kitu. Haya mambo ya mapenzi hayana formula. Na ndoa inaanza sasa. Ni vyema kijana akaoa akifika umri wa miaka 22 hadi 27. Akizidi hapo atachelewa sana kuoa kwa sababu atakuwa anakumbana na matatizo tu ya mahusiano. Ukioa mapema huwezi ona negativity nyingi kwenye masuala ya ndoa.

Dogo palilia hilo penzi lako mapema bila shaka huyo ndio atakuwa mkeo. Usikatishwe tamaa na hawa mabroo wako wa mitandaoni. Wengine above 30 lakini hawana hata girlfriend unafikiri watakushauri nini kuhusu mahusiano zaidi ya kuponda tu.
 
Back
Top Bottom