Unajua mimi nikiwaonaga huwa najiuliza, hivi kweli bongo tuna celebrity wa kike anaweza kufanya lolote kubwa la maana litakalo mfanya aache legacy itakayompa heshima kwanzia sasa na kwa vizazi vijavyo?
Nikiaangalia eti hawa akina Jackline Wolper ndio A-list female celebrities wa bongo na hivi vituko vyao nabaki nacheka tu, unachosema ni sahihi kabisa hawa mademu wa kibongo maarufu kwanza hawajielewi na pili hawajui uthamani wao na kingine hawajui kutumia umaarufu wao.
Ndio maana hata sionagi kama wanapata endorsement deals za maana sababu ya kutokujielewa kwao na kuandamwa na skendo za ovyo ovyo ambazo kimsingi zinashusha profile zao bila ya wao kujua.
Wenzao akina Julieth Ibrahim,Genevieve nnaji,Jack Appiah baada ya kuangaika miaka mingi kutengeneza majina yao nakuwa makubwa, sasa hivi wanapiga endorsement deals za maana kwanzia Nigeria mpaka South A. Sasa hawa wetu hapa wametengeneza majina makubwa halafu umaarufu wao unaishia Instagram kwenye mashindano ya kipuuzi, na hapo hapo hawajui ni kwanini kazi zao haziwalipi.
Kweli bongooo bado saana, eti wema sepetu ndio role model wa akina dada waliopo vyuoni kuna mambo mengine yanachekesha saaana.