Mchumba wa Shilole akataliwa ukweni

Mchumba wa Shilole akataliwa ukweni

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mchumba wa staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ' Shishi Baby ' ,Naftari Mlawa ' Nuh Mziwanda' amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukataliwa ukweni' kwao , Tabora.

Tukio hilo lilijiri ndani ya Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini hapa wakati wawili hao walipokuwa wakipafomu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndipo mashabiki waliposema hawamkubali Nuh na badala yake aolewe na DJ Zirro .

Wakati shoo ya wawili hao ikiendelea, Shilole alikatisha muziki kwa muda na kuwaambia mashabiki kupitia kipaza sauti wamwambie kama Nuh ziwanda ana vigezo vya kuwa mumewe ndipo wakasema hapana na kumpendekeza DJ Zirro ambaye alikuwa akipiga muziki kwenye shoo hiyo .

"Hatumtaki Nuh Mziwanda awe shemeji yetu,bora uolewe na DJ Zirro . Sisi ndiyo tumeamua hivyo , " alisikika mmoja wa mashabiki waliokuwa wakifuatilia burudani hiyo .

Kitendo hicho cha mashabiki kumkataa Nuh Mziwanda kilimfanya bwa ' mdogo huyo ambaye naye anaimba muziki wa Bongo Fleva kujikuta akiropoka na kusema : "Kama mnadhani sina hela basi naomba nitoe mahari hapahapa, " alisema Nuh hukuakiwatupia mashabiki kiasi kidogo cha fedha.

Pamoja na kufanya hivyo , bado mashabiki waliendelea kumkataa Nuh Mziwanda hadi aliposhuka jukwaani ambapo alionekana kukwazwa na jambo hilo kwani tokea aliposhuka alikosa raha kabisa .

Paparazi wetu alimfuata Nuh Mziwanda alipokuwa ameketi baada ya kushuka jukwaani na kumuuliza amejisikiaje kukataliwa ukweni?

"Kusema kweli kuna muda nimejisikia vibaya ingawa hapohapo jukwaani nilijifikiria na kugundua kuwa ni gemu tu hivyo nimejifariji kwa kuona kama ni sehemu ya burudani tu ,"alisema Nuh Mziwanda.
 

Attachments

  • 1410942250158.jpg
    1410942250158.jpg
    67.8 KB · Views: 670

Kwa akili za kawaida madai yao ni akina sepetu wanaofuatia..mavi ya kuku kweli hawa..shule hamna basi majanga tu
Sifahamu kwanini wanataka mpaka mashabiki wawakubali wote wawili,wao wamekwenda kufanya show wafanye show wakimaliza waende zao,personel issue zao hazimuhusu mtu yoyote,wenzao wanafanya siri ma star wa nchi za nje wao
yao wanaaanika kama kama mpunga............
 
Sifahamu kwanini wanataka mpaka mashabiki wawakubali wote wawili,wao wamekwenda kufanya show wafanye show wakimaliza waende zao,personel issue zao hazimuhusu mtu yoyote,wenzao wanafanya siri ma star wa nchi za nje wao
yao wanaaanika kama kama mpunga............

Huyo nuhu ana gundu hadi kwa kina shilole hawamtaki
 
Hivi hiyo Serengeti fiesta inahusika na nini?

ACHA UJINGA WEWE UMeshakuwa chuki roho mbaya havijengi....
haya nakujibu kama kweli ulikuwa hujui inahusika na kusambaza mbolea vijijini!
 
sasa ndo nn,hbr nyingine bwana.Msisahau kutuambia waki-ja-mba pia.
 
ACHA UJINGA WEWE UMeshakuwa chuki roho mbaya havijengi....
haya nakujibu kama kweli ulikuwa hujui inahusika na kusambaza mbolea vijijini!

sasa mi niijue yanini? Mi nayoijua ni Kili music Tour ambalo ni tamasha kwa vijana wajanja
 
Back
Top Bottom