Kuna mambo mawili au matatu yanaweza kumfanya mwanamke asitake kufanya mapenzi ya aina yoyote ile na mwanaume wake.
Moja ikiwa mwanamke hana hisia na wewe kabisa, anaweza kukupenda kama kaka au rafiki ila ile intimacy isiwepo.
Pili, anaweza kuwa yuko kwenye shida ya kisaikolojia, labda kuna kitu alipitia au anapitia na hajaweza kucommunicate na wewe. Ikiwa ana jambo linamtatiza itakuwa ngumu sana yeye kuenjoy mapenzi, zaidi sana yatamkera hivyo anavyofanya anaavoid kukereka.
Tatu, anaweza kuwa ana homone imbalance inayompelekea kukosa hamu ya kufanyana.
Kazi kwako kaka, ongea nae, muombe afunguke na mchunguzi pia. Sijataka kusema jichunguze nawe labda hujui mambo sababu na fahamu sisi wanawake tukimpenda mtu tunaridhika na hicho hicho kitu kidogo anachofanya (though nisisemee wengine), ila kama unahisi unamapungufu rekebisha, mfano skills zako na hygine.
Nimemzungumzia yeye zaidi sababu sisi wanawake tukiwa at our best huwa tunapenda mapenzi kuliko mnavyoweza kufikiri, Yaani mtu pochi imejaa, huna changamoto kazini/biashara na huna changamoto kifamilia. Mambo huwa yanawaka mpaka unamuonea huruma mumeo sometimes ametoka job kachoka huku wewe pia unamsubiri kufanywa.