Mchumba wangu ananishirikisha katika kila kitu cha maendeleo anachofanya

Mchumba wangu ananishirikisha katika kila kitu cha maendeleo anachofanya

Umewaza nnachowaza 🤣🤣 yani hawa watu ni umenunua cheni ya bandia kwa hela feki..
Watu wanamtetea sana jamaa! Mi binafsi tukiachana na huo ujinga mnaomuona nao huyu mleta mada, Mshkaji anamtumia! Sio kimwili tu anamtumia sana kiakili 🤣 ilihali hajamtolea hata barua , kuashiria kwamba hana commitment yoyote mwisho wa siku ataoa mtu mwingine!!!!
Kuna watu hawana akili kwenye mengine ila ukiwapa kazi ya kusuka mpango basi wanausuka hswaa, mleta uzi inaonekana ana madini sema tu kuna hizo error zinazojitokeza kibinadamu
Akili zako kama za huyo binti kwenye mada, maana unatumia nguvu nyingi kutetea upuuzi. What if Jamaa anamshirikisha kila kitu na huyo binti anaona kazi inayofanyika hapo utasemaje?.
 
Akili zako kama za huyo binti kwenye mada, maana unatumia nguvu nyingi kutetea upuuzi. What if Jamaa anamshirikisha kila kitu na huyo binti anaona kazi inayofanyika hapo utasemaje?.
"What if" what???
Jamaa akimshirikisha haiondoi kuwa hajamuoa kwahiyo anaweza kuachwa anytime hivyo vishirikisho vitakua vimemsaidia nini?? Hatusemi kuwa jamaa aspend juu yake, bali hio so-called "kushirikishwa" ina msaada gani juu ya huyo dada? Hio kazi inayofanyika hati imeandikwa jina la jamaa au dada?? 😂😂

Muwe mnawaza nje ya Box
 
Umewaza nnachowaza [emoji1787][emoji1787] yani hawa watu ni umenunua cheni ya bandia kwa hela feki..
Watu wanamtetea sana jamaa! Mi binafsi tukiachana na huo ujinga mnaomuona nao huyu mleta mada, Mshkaji anamtumia! Sio kimwili tu anamtumia sana kiakili [emoji1787] ilihali hajamtolea hata barua , kuashiria kwamba hana commitment yoyote mwisho wa siku ataoa mtu mwingine!!!!
Kuna watu hawana akili kwenye mengine ila ukiwapa kazi ya kusuka mpango basi wanausuka hswaa, mleta uzi inaonekana ana madini sema tu kuna hizo error zinazojitokeza kibinadamu
Ataachwa kwa vile jamaa anaona hana akili, mwanamke akikosa akili hata familia hataweza kuitunza. Huwezi jua it's a way kufahamu aina ya mwanamke anayetaka kuishi nae. Kupata kijana miaka 30 anajitahidi kujiendeleza kiuchumi ni jambo jema, vijana wengi saivi ni mba mba mba hamna kitu kabisa..
 
Ataachwa kwa vile jamaa anaona hana akili, mwanamke akikosa akili hata familia hataweza kuitunza. Huwezi jua it's a way kufahamu aina ya mwanamke anayetaka kuishi nae. Kupata kijana miaka 30 anajitahidi kujiendeleza kiuchumi ni jambo jema, vijana wengi saivi ni mba mba mba hamna kitu kabisa..
Hakuna sababu hapo ataachwa kama bwana akitaka..
Kipimo cha akili ni nini??? Maana nusu ya wanaoolewa huwa hawana hizo sifa mnazozisemaga tena ni watu hovyo kabisa... watu wanaolewa Mungu akipenda sio kisa kuvumilia kutumika kiakili! Kama anamtaka amuoe afu waendelee kufanya maendeleo ili dada awe na haki zake
 
Kuna siku mzee mmoja alinikuta mgahawani nakula
Tunafahamiana nae kwasababu alikua na uhitaji kidogo unahousiana na kazi yangu nikamsaidia
Aliketi kishaakaagiza soda mbili moja akanipa kisha yeye akaendelea kunywa yakwake......katika maongezi ongezi akaniambia...
Wewe bado nikijana mdogo sana
Pia hongera kwa kupata kazi yakufanya
Lakini ...utakosea na kupoteza dira yako yote pindi utakapoweka kichwani mwanamke!
Nikamuuliza kwanin ....? Akanijibu....
Wanawake wengi wao hawajielewi kabisa
(Unaweza )kumpata mzuri akachangia maendelea yako kwa kiasi kikubwa mnoo,lakini ni mmja tu kati ya 100
Ila wengi wao hawajui wanachokitaka
Na baadhi yao hawajijui hata wao wenyewe
Kwahyo kwa ushauri wangu pambnia kutimiza ndoto zako zooote au ukiwa umeshafanya kwa 80% ndio uanze kuangalia kwasababu hata ukimpata mjinga kwa hapo ulipofika utaweza kupigana kufikia hapo zaidi
Kuliko kujichanganya leo ikiwa huna chochote atakuja akufukie zaidi...!

Na naona maana ya maneno yake kila mala nikiingia JamiiForums.
Kweli mze wangu.
 
Wanawake kweli hamna shukrani ,wewe una mshahara lakini bado unataka mshahara wa mwanaume ununue vitu vyako binafsi tena vya luxury wakati mwenzio mshahara wake unafanya vitu vya maendeleo vya kwenu wote kama familia.
Kuwa nashkrani dada acha ulimbukeni!
 
Huyo sio mtu sahihi kwake! Ampige chini akatafute mwanaume anayejua kuspend, kumbebisha! Kumtoa out na kila aina ya starehe

Nasema hivyo kwasababu ndege wanaofanana huruka pamoja! Huyu jamaa akili zake ni za maendeleo wakati huyu dada yeye anataka starehe, outing, kuletewa zawadi! Kupewa hela wakati ana mshahara! Bora amuache huyo bro naamini atapata mtu wa type yake!
Kati ya wanawake wajinga duniani ww ni mama yao mwisho wa kunukuu
 
Hahahaha mbona umeniquote hapo na kuniita mama!??
Elewa concept, ww ni mjinga sana, na huyo mwanaume wako anajitambua vzr. Ww huyo sio type Yako maana utampotezea muda tu yy anawaza maendeleo ww unawaza starehe na mambo ya hovyo unaobekana ni mbinafsi mno ba haupo tayari kumpa ushirikiano unajiangalia ww tu
 
Elewa concept, ww ni mjinga sana, na huyo mwanaume wako anajitambua vzr. Ww huyo sio type Yako maana utampotezea muda tu yy anawaza maendeleo ww unawaza starehe na mambo ya hovyo unaobekana ni mbinafsi mno ba haupo tayari kumpa ushirikiano unajiangalia ww tu
Nadhani wewe hauelewi unachokifanya!?? Mm sio mtoa maada Mimi ni mchangiaji kama ww
 
Duh! Huyo rafiki yako Ni miyeyusho Sana, Kuna watu ukiishi nao kufanikiwa unaweza kusikia tu kwa watu,mfano mzuri Ni rafiki Yake na mtoa mada.
 
Mshaurini huyu jamani...

MCHUMBA WANGU ANANISHIRIKISHA KATIKA KILA KITU CHA MAENDELEO ANACHOFANYA!

Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye yeye ana miaka 30, nampenda sana na yeye anaonyesha kunipenda kwakuwa kashanitambulisha mpaka kwao na kwetu pia nimeshamtambulisha. Tatizo ni kuwa mpenzi wangu huwa ni muwazi sana, ananishirikisha katika kila kitu chake cha maendeleo anachokifanya na mara nyingi anakuwa anataka mawazo yangu, akitaka kununua kiwanja, kujenga, akitaka kitu chochote hata kama ni mapazia anataka tufanye pamoja.

Mimi nafanya kazi na yeye pia anafanya kazi, haniombi pesa na wala hajawahi lakini tatizo ni kuwa kwakuwa ananishirikisha katika mambo yake basi nashindwa kumuomba pesa kubwa kubwa kwaajili ya kufanya mambo yangu kwani kila hela yake najua imeenda wapi? Kwa mfano labda nataka laki mbili, ninataka kununua kitu changu labda kutoka na marafiki, nikimuambia pesa ananiambia hana si tumenunulia kitu flani, ukiangalia kweli alinunua hicho kitui na alinishirikisha hivyo naona aibu hata kumkasirikia kwani kinakuwa cha maendeleo na najua pesa yake yote.

Naumia sana kwani mimi kama msichana nahitaji kudekezwa na kufanyiwa suprize za zawadi kama marafiki zangu ambao wanaweza kufanyiwa birthday na wapenzi wao, kutolewa out, kununuliwa nguo na zawadi. Mimi nikihitaji kitu inabidi nimuambie mapema kabla ya mshahara ili aniweke kwenye bajeti na sanasana atakupa elfu hamsini hata laki hakupi kwani anakuwa anafanya vitu vingi vya maendeleo ambavyo ananiomba ushauri na ukiangalia anakuwa kweli hana kwani hata yeye hafanyi hizo starehe

Kinachoniuma zaidi ni kuwa hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe kama mwanaume ni lazima aniambie na mara nyingi hupenda kufuata ushauri wangu na si wake. Kunipenda kweli ananipenda lakini nina wasiwasi je tukioana itakuaje kwani mara nyingi anasema tukioana itakua vizuri kama tukishirikiana kwenye mambo ya familia eti mshahara wangu nao tufanyie mambo ya maendeleo wakati yeye kama mwanaume anatakiwa kufanya kila kitu, niko njia panda nawaza je huyu ni mtu sahihi kwangu au nifanyeje?
Huyo ni mtu sahihi kwako.anajiandaa kuwa baba was familia.anakupenda ndo Mana anakushirikisha Kila kitu.Mshukuru Mungu
 
Back
Top Bottom