Charles Wachira, mchungaji mwandamizi katika kanisa la Jesus Christ Compassion Ministry (JCM), amejiuzulu wadhifa wake baada ya kiongozi wa kanisa hilo, Askofu Ben Kiengei kukubali kumkaribisha Rais William Ruto siku ya Jumapili, hatua ambayo amesema imefanywa “kinyume na matakwa ya wengi.”
Mchungaji Wachira, ambaye anaishi Marekani, amesema kuwa kwa kanisa kukubali kumpokea Rais Ruto katika kanisa la Ruiru, Askofu Ben ameshindwa kuonesha misingi sahihi ya uongozi na hajajali kilio cha Wakenya wengi wanaodai haki na uwajibikaji kutoka kwa serikali ya Rais Ruto.
“Kanisa halipaswi kamwe kuonekana kama halijali maumivu ya watu,” amesema Mchungaji Wachira katika sehemu ya taarifa yake ya kujiuzulu.
Taarifa hiyo inaendelea kusema, “Mchungaji Charles Wachira anaamini kuwa uongozi wa kiroho lazima usimame imara katika ukweli, haki na kulinda maisha ya wasio na hatia. Pale ambapo maamuzi ya uongozi yanaleta mkanganyiko, mgawanyiko au hali ya kutoelewana miongoni mwa waumini, inakuwa ni lazima kuchukua msimamo wa kimaadili.”
Aidha, mchungaji huyo amesisitiza kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu katika kanisa la JCM umetokana na msimamo wa dhamira yake, siyo kukubali kushinikizwa au kufanya maafikiano.
============
Charles Wachira, a senior pastor at the Jesus Christ Compassion Ministry (JCM), has resigned after the church's leader, Bishop Ben Kiengei, accepted to host President William Ruto on Sunday 'against the will of the majority'.
Pastor Wachira, who is based in the US, says by the church accepting to host President Ruto at the Ruiru church, Bishop Ben has failed to show proper leadership principles and is not concerned about the many Kenyans crying out for justice and accountability from President Ruto's government.
"The church must never appear indifferent to the pain of the people," says Pastor Wachira in part of his resignation statement.
The statement continues, "Pastor Charles Wachira believes spiritual leadership must stand firmly on truth, righteousness, and the defense of innocent life. When leadership actions create confusion, division, or moral discomfort among believers, it becomes necessary to take a principled stand."
The pastor has clarified that his decision to resign from the JCM Church reflects conviction and not compromise.
Source: Buzzroom Kenya