Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

Yale makanisa yaliyopo pale kwa mchina mwisho Wasabato, Karibu na jumbi Roman Catholic ukienda mfenesini kuna lingine mpaka kule shamba karibu na jku sijui kanisa gani yale mbona hayavunjwi na wasabato wameongeza eneo kwa kununua nyumba HOW?.

Pia makanisa yote hayo yapo uswahili ndani ndani huko sijwahi sikia hata siku moja rabsha.

Sema mkuu wa wilaya kachemka au alikosa neno la kuweka hapo akaongea alilokuwa hajategemea, sasa mvua kipindi hiki wapi na wapi 😆😂🤣🤣👍🏾
 
So, what is your point here na tushike lipi hasa...?

Kwamba mamlaka za mipango miji huko Ugunja - Zanzibar ziliamua kulivunja kanisa la Mch. David Suni kwa sababu they are all insecure....?

Au tumwamini DC asemaye kuwa, zimevunja kanisa hilo kwa sababu ya utabiri wa hali ya hewa kusema kuna mvua kubwa zinakuja huko Ugunja - Zanzibar na mvua hizo zimelenga kuja kulipitia kanisa hilo tu ktk mtaa huo...?
 
Hao wakazi wapo sahihi. Kwa tabia yenu ya makelele mkiruhusiwa tu basi kisiwa chote mtakimeza kwa makelele yenu.
Mkuu.... Sisi kuswali na kutumia spika wewe inakuumiza nini? Makelele ninyi hamna mnapopiga kengele ? Kama hupendi adhana una matatizo binafsi. Wengine inawasaidia hata kuamka kwenda kazini asubuhi na usiku pia kujua muda wa kula.acha chuki binafsi. Heshimu dini za wenzio
 
We jamaa vipi badala unatumia akili mbovu sana kuhalalisha huu unyama wa mkuu wa wilaya. Kila mtu ana uhuru wa Kuabudu aisee kinyume na hapo ni uvunjaji wa katiba. Mama Samia kamata mkuu wa wilaya na hiyo manispaa tumeanza kurudi tukipotoka miaka ya kikwete
 
Hiki ndicho DC alipaswa kuzungumza!

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Sawasawa uende Mogadishu ukajenge kanisa unategemea nini? au uende Roma ukajenge msikiti. ndio maana ukienda UK misikiti mingi sababu nchi ina waislamu wengi lakini huwezi kukuta hiyo hali mfano Warsaw sababu hakuna dini nyingine pale. Tuache chokochoko mbona huku kwetu ardhi kubwa kuna makanisa, ma temple ya wahindi, misikiti mpaka kuna watu wanatokea kujiita miungu na makanisa yao na lilivunjwa sababu yako mambo yanavuka mipaka, Umetoka maelezo yanajitosheleza 100% ambaya hatakuelewa basi anayake.
 
Kiongozi Leo nimekuelewa
 
halafu jamaa ajiongeze atafute mtu auze iyo sehemu aache upimbi sheria ya ardhi mtu wa bara haruhusiwi kumilili ardhi zanzibar nashangaa linajifanya halijui atalikosa eneo na pesa pia kwa upimbi wake.
 
Kuna maeneo Bara wakazi woote ni wakristo, ila msikiti ukijengwa hapo wenyeji hawajali. Unawashauri nini wakazi kama hao?
 
Kuna rafiki yangu mmoja wa kike alinitembelea yeye n mwislam sasa nikafungulia redio ikapiga kwaya alibadilika ghafla na kusema toa ayo madude sitaki kuyasikia 🤣😆😁 nilibaki nashangaa sana wakati mm ingawa na mkristo mawaidha au mambo ya Islamic hayaniathiri hata kidogo kutakuwa na shida mahal maana......
 
Elimu ya madrasa inaharibu sana akili za baadhi ya watanzania.
 
Hujawaona hao wanaolia kuwa ndio wateja? Kwa taarifa yako hata angekuwa mtu mmoja anastahili kuwa na kanisa lake mahali lake pa kusali
 
Mkuu jaribu kujifunza mambo mengi na kuyaelewa utanishukuru.
 
Kwa hiyo hao 1% waache kusali wageukie upagani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…