Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

licha ya kuwa Europe kuna nchi ambazo zinakua na haki nyingi za kibinaadamu mpaka nyengine za aibu lakini bado hawapo huru kama wanavyokua katika maeneo yao, na zaidi ni kuwa Uislamu Europe unashamiri kutokana na Wazawa wengi kuingia katika waislamu, na sio kwa kutegemea wageni.
Sasa wazawa si lazima wapate wa kuwapelekea hiyo imani? Tuache watu wasikie neno ili wachague pa kuamini. Leo hii waislam wengi wanajazana huko kwa wanaojiita manabii kuokoka na kupata uponyaji
 
Siku chache tangu kuripotiwa kwa taarifa za kuvunjwa kwa Kanisa la T.A.G lililopo Sebleni, Unguja ripoti kamili ya kilichotokea imetolewa kutoka upande wa kanisa pamoja na upande wa Serikali ya Zanzibar.

Mchungaji wa kanisa hilo linaloelezwa kuwa limevunjwa, David Victor Suna amefunguka kilichotokea kwa kusema:

MCHUNGAJI AFUNGUKA
“Ni kweli wamevunja nyumba yetu ya ibada licha ya kutambua kuwa tuna uhalali wa kila kitu, na suala hilo kwa sasa lipo kwa wanasheria wetu wanalishughulikia.

“Eneo hilo nilinunua kihalali kabisa kwa Sh milioni 16 na wakati nanunua nilikuta kuna banda ambalo lilikuwa shemu ya mauzo ya kiwanja, nilichofanya nikaboresha kwa kujenga ukuta.

“Lakini baada ya kuanza kuwa tunasali, nikapata malalamiko kuwa wakazi wa hapo hawataki kanisa, wakawa wanakuja viongozi kadhaa wa Serikali kukagua wakiniambia malalamiko ya uwepo wa kanisa letu mahali hapo.

“Kwanza waliniambia nimejenga ukuta kimakosa, kwa kuwa sina kibali cha kujenga ukuta, nikawaambia sawa hilo nakiri kwa kuwa sikuwa najua kama ukta unahitaji kibali, nikawaambia nitafuata mchakato wa kupata kibali kwa mamlaka husika.

“Baada ya mvutano wa muda mrefu nilienda hadi kwa Mkuu wa Wilaya akaniambia kama kama ninataka kibali cha nyumba ya makazi ya kawaida nitapata lakini kama ni kuhusu kanisa hapo siyo sehemu sahihi na hawatanipa kibali kwa kuwa wakazi wa eneo hilo hawataki kanisa.

“Siku hiyo ndiyo nikashangaa wamekuja wakavunja kwa kutumia mgongo wa Manispaa. Viongozi wetu wakuu akiwemo Askofu Mkuu amesema niwe kimya, nisifanye chochote kwa sasa, wao ndiyo watakaotoa tamko kwa kuwa suala letu limefika ngazi ya kitafa.

“Mimi ni mkazi wa Unguja miaka mingi, najua wanachofanya ni kitu ambacho wanakifanya muda mrefu, kuna upande ambao unakuwa una nguvu kubwa kiimani kuliko mwingine.

“Mimi kwa sasa nipo kimya, hata kule walipofunja siendi kwa kuwa sitaki matatizo, sijafanyiwa fujo zaidi ya siku ile ambayo walivunja, lakini mpaka sasa (Machi 11, 2022) sijapata tatizo lolote.”

TAMKO LA SERIKALI, LAMSAKA MCHUNGAJI
Mkuu wa Wilaya wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja, Rashid Msaraka amezungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2022 baada ya kufika eneo la tukio.

“Mamlaka zinazohusiana na utabiri wa hali ya hewa, zimetoa tathmini yao kuhusu mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni, nikatoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuwa na tahadhari ya maeneo hatarishi, moja kati ya maeneo hayo ni hiyo iliyobomolewa.

“Nyumba mojawapo iliyobomolewa ni nyumba ya kawaida lakini taarifa inayosambaa ni kanisa, hapana mimi sina kibali cha kujengwa kwa kanisa.

“Hivyo, imevunjwa kwa kuwa ni sehemu ya nyumba zilizokuwa hatarishi, tunaweka mazingira sawa, siyo hapa tu bali ni maeneo yote.

“Yote yanayoendelea mitandaoni kuwa kuna maandalizi ya vita ya Waislamu dhidi ya Wakristo siyo kweli.

“Katika taarifa zinazosambaa kuna mtu anaitwa David Suna, sijui kama ni kiongozi wa kawaida au kiongozi wa dini, hatumfahamu, nimempa maelekezo Kamanda OCD kumtafuta huyo Daudi Suna ili kutoa maelezo ya kinachoendelea mitandaoni.

“Sisi tumemwambia ODC hiyo clip inayosambaza ni mbaya na ni ya uchochezi.

“Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu ana haki ya kuambudu lakini lazima kuwe na utaratibu.

“Nasisitiza kuwa hapakuwa na kanisa, kulikuwa na nyumba za kuishi. Tunatoa taarifa kuwa hakuna rabsha yoyote.

“Tumewaambia wale ambao wanaona hawajatendewa haki basi waje watuambie lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza.

“Tutahakikisha tunawalinda raia wote bila kuwa na ubaguzi, usalama wa raia wa kila mtu ni muhimu. Zanzibar ni sehemu ambayo ina historia ya kuw ana makanisa tangu enzi na enzi, hatutamvumilia mtu au watu ambao watakuwa wanania ya kuharibu taswira ya Serikali ya Zanzibar.”

Pia Soma~~ Zanzibar: Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna, yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo
Kuna watu wengine ni wakorofi tu of all places kwanini ujenge kanisa Zazibar? ambao hamna wateje? 99% ni dini moja ya kiislamu? Ni yale yale ya kuweka bucha ya kitimoto karibu na mskiti wakati kuna sehemu zingine kwa kisingizio xha uhuru wa mtu kufanya biashara popote.
 
Nitoke nje ya mada kidogo, hv makanisa ya kilokole kuubiri bila vipazasauti haiwezekani. Yaan SoMo haliwezi kueleweka. Japo dini na madhehebu mengine nao hufanya hivyo lakini wanaunafuu kidogo ukilinganisha na walokole.
 
mkuu, wakishejenga huwa wanapata misaada kutoka kwa makanisa makubwa ya bara au ulaya kwa kisingizio kuwa wanasambaza neno la bwana. Watu wanatafuta Ugali tu usimlaumu sana mzee.
 
Mkuu Zanzibar ni nchi ya kiislamu, 99% ya watu wake ni waislamu, kwahiyo hakuna cha ajabu kuwa na mifumo ya kiislamu kwenye maisha yao, ni tofauti na Bara ambapo uwiano wa dini hizi mbili ni mkubwa nearly 50 - 50, So cha muhimu ni kufahmu kuwa haiwezekani mazingira ya Zanzibar yakawa sawa na Bara. Tujaribu kulitathmini kwa uandani na sio kuishabiki. Tatizo kuu la Zanzibar ni suala la Makanisa kuwa yanaengezeka kwa kasi kila siku zinavyokwenda, Na hilo linawafanya wananchi wao wengi kuwa insecure. Nchi nyingi ambazo ziko dominated na dini moja kwa zaidi ya 90% ni lazima watu wa dini nyengine wata experience mambo kama hayo, na hasa wakiwa Wageni.
Kuna vitu unachanganya hapa.
Ngoja nikuweke sawa kidogo.
1. Uhuru wa kuabudu unaletwa na kulindwa kikatiba na sio idadi ya waumini wa eneo husika, hivyo wingi wa waislamu kwa Zanzibar sio sababu ya kuwanyima uhuru wa kuabudu wakristo.

2. Nchi ya Tanzania na Zanzibar, serikali ya Tz na SMZ zote hazina dini, hivyo hakuna dini iliyo juu ya mwingine linapokuja suala la kuabudu. Sio sahihi kwa muislamu kumpangia mkristo namna ya kuabudu, and vice versa.

3. Tanzania ni kubwa sana, na Zanzibar ni eneo dogo katika Tanzania, yapo maeneo mengi yenye aina fulani ya waumini wa dini au imani iliyotawala zaidi lakini hawezi kuona hali ya waumini fulani kuzuia shughuli za kuabudu za imani nyingine.

4. Huo uwiano wa waumini wa kiislamu kuwa 99% ya wazanzibar wote sio wa kweli wala sio rasmi. Ni kweli wako wengi lakini sio kwa kiwango hicho. Zanzibar ni eneo lenye mchanganyiko wa watu wengi sana kwa sasa kuanzia waislamu, wakristo, wahindu, wabagani nk. Kuna mitaa hapa Zanzibar ina misikiti na ikipigwa adhana unaweza kukuta msikitini kuna imamu na muumini mmoja tu!
 
Wapuuzi hao Waislamu yani wanajitetea kuvunja nyumba ya mtu????? Kwa hiyo sababu mpo wengi zanibar mnaamua tu kuvunja Kanisa yani huu ni mwanzo wa yale mambo ya Kuchoma makanisa na kuua mapadri yaliyotokea enzi za JK jamaa wakiona kiongozi wa Nchi ni dini yao yani wanatakaga kutawala kila sehemu wao ndo waamue juu ya maisha ya watu fakeni kabisaaaa mama akikaa vibaya wataanza kuchoma makanisa... Mbona enzi za JPM hawakujaribu huu utumbooi????
 
Kuna vitu unachanganya hapa.
Ngoja nikuweke sawa kidogo.
1. Uhuru wa kuabudu unaletwa na kulindwa kikatiba na sio idadi ya waumini wa eneo husika, hivyo wingi wa waislamu kwa Zanzibar sio sababu ya kuwanyima uhuru wa kuabudu wakristo.

2. Nchi ya Tanzania na Zanzibar, serikali ya Tz na SMZ zote hazina dini, hivyo hakuna dini iliyo juu ya mwingine linapokuja suala la kuabudu. Sio sahihi kwa muislamu kumpangia mkristo namna ya kuabudu, and vice versa.

3. Tanzania ni kubwa sana, na Zanzibar ni eneo dogo katika Tanzania, yapo maeneo mengi yenye aina fulani ya waumini wa dini au imani iliyotawala zaidi lakini hawezi kuona hali ya waumini fulani kuzuia shughuli za kuabudu za imani nyingine.

4. Huo uwiano wa waumini wa kiislamu kuwa 99% ya wazanzibar wote sio wa kweli wala sio rasmi. Ni kweli wako wengi lakini sio kwa kiwango hicho. Zanzibar ni eneo lenye mchanganyiko wa watu wengi sana kwa sasa kuanzia waislamu, wakristo, wahindu, wabagani nk. Kuna mitaa hapa Zanzibar ina misikiti na ikipigwa adhana unaweza kukuta msikitini kuna imamu na muumini mmoja tu!

Mkuu kuhusu hiyo namba 4 halina utata kabisa, Ni kweli Zanzibar kuna Wakristo wengi ila majority yao ni wahamiaji. Wakiristo wa asili kwa maana ya wale wanaotambulikana kama ni wazanzibari wakichanganyika na wahindu hawawezi kufika hata asilimia 1.
 
Nitoke nje ya mada kidogo, hv makanisa ya kilokole kuubiri bila vipazasauti haiwezekani. Yaan SoMo haliwezi kueleweka. Japo dini na madhehebu mengine nao hufanya hivyo lakini wanaunafuu kidogo ukilinganisha na walokole.
Kabla ya hilo swali lako kujibiwa, anza kwanza kajiuliza hili swali; hivi makanisa ya kikatoliki hayawezi kuwaita waumini wao kuja kanisani kusali bila kuwagongea kengele?
Kwani waumini hawana saa?
Hawajui muda wa ibada?
 
Huyo Mkuu wa wilaya ya Mjini Magharibi ndie mjinga kabisa, amekuja kutetea wahalifu kwa kuficha ukweli makusudi.

Anadai jengo lililovunjwa sio kanisa ni nyumba, sawa nikubaliane na sababu yake ya kijinga, ila hata kama ni nyumba walivunja baada ya kutoa notice?

Anadai tena hiyo nyumba imejengwa sehemu hatarishi, kwa hiyo wameiona hiyo nyumba pekee ndio iko pahala hatarishi hakuna nyingine jirani nayo waivunje?

Unapokuwa na watendaji serikalini wapuuzi wa sampuli hii ni vigumu sana kuaminiwa na unaowaongoza, ni wazi hilo Kanisa limevunjwa makusudi na hao wajuaji huko Zanzibar kama ilivyo tabia yao, lakini anapojitokeza kiongozi wa serikali kutetea huo uhuni hili kwangu ndio jambo la kushangaza zaidi.

Kumbe serikali ya Zanzibar inaongozwa na gangsters, ajabu anawataka wenye malalamiko waende ofisini kwake, wakati ofisi yenyewe imejaa watu wa aina hiyo hiyo toka kundi la wahalifu hiyo haki itapatikana vipi?

Zanzibar naiona ni sehemu ya hovyo sana kuishi, mindset za watu wake ni za kishamba sana, wanaishi gizani muda mrefu wakiamini wanatenda kwa kufuata misingi ya dini yao kumbe hata hiyo dini yenyewe hawaijui.
 
Kabla ya hilo swali lako kujibiwa, anza kwanza kajiuliza hili swali; hivi makanisa ya kikatoliki hayawezi kuwaita waumini wao kuja kanisani kusali bila kuwagongea kengele?
Kwani waumini hawana saa?
Hawajui muda wa ibada?
Nyie yale mavipaza sauti yenu asubuhii hamuyaoni eti????? Unadhani tunafurahia makelele yale watu tumelala mnaaza kupiga makelele kama wehu...
 
Kuna vitu unachanganya hapa.
Ngoja nikuweke sawa kidogo.
1. Uhuru wa kuabudu unaletwa na kulindwa kikatiba na sio idadi ya waumini wa eneo husika, hivyo wingi wa waislamu kwa Zanzibar sio sababu ya kuwanyima uhuru wa kuabudu wakristo.

2. Nchi ya Tanzania na Zanzibar, serikali ya Tz na SMZ zote hazina dini, hivyo hakuna dini iliyo juu ya mwingine linapokuja suala la kuabudu. Sio sahihi kwa muislamu kumpangia mkristo namna ya kuabudu, and vice versa.

3. Tanzania ni kubwa sana, na Zanzibar ni eneo dogo katika Tanzania, yapo maeneo mengi yenye aina fulani ya waumini wa dini au imani iliyotawala zaidi lakini hawezi kuona hali ya waumini fulani kuzuia shughuli za kuabudu za imani nyingine.

4. Huo uwiano wa waumini wa kiislamu kuwa 99% ya wazanzibar wote sio wa kweli wala sio rasmi. Ni kweli wako wengi lakini sio kwa kiwango hicho. Zanzibar ni eneo lenye mchanganyiko wa watu wengi sana kwa sasa kuanzia waislamu, wakristo, wahindu, wabagani nk. Kuna mitaa hapa Zanzibar ina misikiti na ikipigwa adhana unaweza kukuta msikitini kuna imamu na muumini mmoja tu!

Na kuhusu kuwa Serekali ya SMZ haina dini hio sio kweli, SMZ ina dini na pia ina dhehebu lake. Hata waislamu wasio katika dhehebu ambalo ndio dhehebu linaloshika hatamu wanapata tabu sana. Kama utakua na kumbukukumbua jaribu kukumbuka vizuri vurugu za 90's - 2000's za baina ya Serekali na Aliekua Sheikh Mkubwa wa Dhebu la Ahli Sunna pamoja na Ansar Sunna wengine Sheikh Nassor Bachu, FFU walikua wakiingia mpaka miskitini kupiga watu.
 
Ukweli tuuseme tu, hata kama unatuuma.
Suala la uvumilivu wa kiimani kwa Zanzibar uko chini sana. Kujenga kanisa huwa kunawakera na kuwaudhi mnoo watu waliopo Zanzibar. Makanisa yanayoheshimiwa ni yale ya kihistoria ambayo yanafanya watalii waje, tofauti na hapo yangekuwa yameshavunjwa siku nyingi.

Kwa Zanzibar malaya, mashoga na mateja wana thamani kubwa kuliko muumini wa Kikristo mwenye msimamo.
Hiyo ndo kweli ya nchi yetu. Umaskini unachochea misimamo mikali ya kidini kwa kuamini Mbigu ipo! Z'bar wanasumbuliwa sana na kusikia dini ya Kikristu. Mauaji ya enzi ya Kikwete yalionekana ni kawaida tu! Ingawa nyuma ya pazia tuliambiwa yalichochewa makusudi na hakuna aliyehukumiwa.

Pamoja na hayo, makanisa yanajipa ukuu bila sababu. Ktk mipango miji, maeneo ya ibada yanafahamika na hutengwa mahsusi. Tatizo ni mtu anajifanya Askofu/nabii/mtume anaamua kuanzisha kanisa kwenye nyumba yoyote na popote. Kelele inakuwa ni mtindo mmoja kisa ana wafadhiri wa Marekani wanampa vijifedha vya sementi.
 
Kwa hyo mabwabwa Wana thaman kubwa huko zenji?

Ila tambueni dini tumeletewa na mkoloni

Watu hawajiulizi mbona hakuna nabii mwenye rangi nyeusi yaan mwafrika ina maana SS weusi tulitengwa hatukuhtaji dini

Watakatifu wote watu weupe weus n wakuhesabu Sana Tena had tuwalazmishe

Msikitini lugha n kiarabu TU Kwan MUUNBA hasikii kiswahili kwann tusiswali kiswahili ili kila mtu aelewe?

TUJIOKOE KIFIKRA

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mbona kuna manabii wengi weusi? Kuna Nabii Suguye, Nabii Mwamposa, Mwigira n.k
 
licha ya kuwa Europe kuna nchi ambazo zinakua na haki nyingi za kibinaadamu mpaka nyengine za aibu lakini bado hawapo huru kama wanavyokua katika maeneo yao, na zaidi ni kuwa Uislamu Europe unashamiri kutokana na Wazawa wengi kuingia katika waislamu, na sio kwa kutegemea wageni.
Nchi gani hiyo inayowaingiza wazungu kwa wingi? Huo ni uongo tu! Europe hawana mpango na dini; iwe uislamu au ukristu.
Nchi zenye Usilamu ni kwa wingi ni Ufaransa na Ubelgiji, lakini ni kwa sababu ya wahamiaji toka Uturuki, Morocco, Tunisia, Algeria na francophone wa Afrika magharibi.
 
Mkuu kuhusu hiyo namba 4 halina utata kabisa, Ni kweli Zanzibar kuna Wakristo wengi ila majority yao ni wahamiaji. Wakiristo wa asili kwa maana ya wale wanaotambulikana kama ni wazanzibari wakichanganyika na wahindu hawawezi kufika hata asilimia 1.
Niko Zanzibar na naijua Zanzibar vizuri.
Kwanza wewe jua tu, wazanzibar karibu wote kihistoria ni wahamiaji, wapo waliotoka bara na wapo waliotoka nchi za mbali na visiwa vya jirani.

Pili dini karibu zote zilizopo hapa Zanzibar zimeletwa kutoka mbali (sio dini za asili za wazinzibar), uislamu uliletwa na waarabu na ukristo uliletwa na wazungu huenda hata kabla ya hizo dini kufika Tanganyika, dini za asili hapa Zanzibar ni zile za jadi na mpaka leo zipo!

Sasa jiulize tu, eneo la Zanzibar lenye ukubwa sawa na wilaya Sengerema, lenye 99% ya waumini wa dini ya kiislamu inawezekanaje haya kuwepo;

-Kuna zaidi ya bar 30 zenye kuuza pombe 24hours
-Kuna mahoteli na migahawa zaidi ya 5 yenye kuuza kiti moto 24hours
-Kuna utitiri wa makahaba kila mtaa
-Kuna mashoga kila mtaa
-Kuna utiriri wa mateja na wauza ngada kila mtaa.
-Kuna guest bubu na madanguro ya kienyeji karibu kila mtaa.

Jamani tusiuhusishe uislamu na vitu vya ajabu, uislamu sio utamaduni wa kiarabu na mila za watu wa pwani, uislamu ni imani halisi inayohubiri Amani na Ibada, muislamu halisi hawezi kumchukia mtu mwingine anayeabudu imani zingine.
 
Back
Top Bottom