Primitive ideaHao wakazi wapo sahihi. Kwa tabia yenu ya makelele mkiruhusiwa tu basi kisiwa chote mtakimeza kwa makelele yenu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Primitive ideaHao wakazi wapo sahihi. Kwa tabia yenu ya makelele mkiruhusiwa tu basi kisiwa chote mtakimeza kwa makelele yenu.
Sawa ni wahamiaji kwani hawaingii katika idadi ya wazanzibari wakaazi kwa wale ambao wana zaidi ya miaka mi5 ?
alivunjiwa kwasababu eneo ni hatarishi, alipewa fidia, au mlishirikiana naye vipi kuhusu haki zake, au kwasababu ni mkristo?Siku chache tangu kuripotiwa kwa taarifa za kuvunjwa kwa Kanisa la T.A.G lililopo Sebleni, Unguja ripoti kamili ya kilichotokea imetolewa kutoka upande wa kanisa pamoja na upande wa Serikali ya Zanzibar.
Mchungaji wa kanisa hilo linaloelezwa kuwa limevunjwa, David Victor Suna amefunguka kilichotokea kwa kusema:
MCHUNGAJI AFUNGUKA
“Ni kweli wamevunja nyumba yetu ya ibada licha ya kutambua kuwa tuna uhalali wa kila kitu, na suala hilo kwa sasa lipo kwa wanasheria wetu wanalishughulikia.
“Eneo hilo nilinunua kihalali kabisa kwa Sh milioni 16 na wakati nanunua nilikuta kuna banda ambalo lilikuwa shemu ya mauzo ya kiwanja, nilichofanya nikaboresha kwa kujenga ukuta.
“Lakini baada ya kuanza kuwa tunasali, nikapata malalamiko kuwa wakazi wa hapo hawataki kanisa, wakawa wanakuja viongozi kadhaa wa Serikali kukagua wakiniambia malalamiko ya uwepo wa kanisa letu mahali hapo.
“Kwanza waliniambia nimejenga ukuta kimakosa, kwa kuwa sina kibali cha kujenga ukuta, nikawaambia sawa hilo nakiri kwa kuwa sikuwa najua kama ukta unahitaji kibali, nikawaambia nitafuata mchakato wa kupata kibali kwa mamlaka husika.
“Baada ya mvutano wa muda mrefu nilienda hadi kwa Mkuu wa Wilaya akaniambia kama kama ninataka kibali cha nyumba ya makazi ya kawaida nitapata lakini kama ni kuhusu kanisa hapo siyo sehemu sahihi na hawatanipa kibali kwa kuwa wakazi wa eneo hilo hawataki kanisa.
“Siku hiyo ndiyo nikashangaa wamekuja wakavunja kwa kutumia mgongo wa Manispaa. Viongozi wetu wakuu akiwemo Askofu Mkuu amesema niwe kimya, nisifanye chochote kwa sasa, wao ndiyo watakaotoa tamko kwa kuwa suala letu limefika ngazi ya kitafa.
“Mimi ni mkazi wa Unguja miaka mingi, najua wanachofanya ni kitu ambacho wanakifanya muda mrefu, kuna upande ambao unakuwa una nguvu kubwa kiimani kuliko mwingine.
“Mimi kwa sasa nipo kimya, hata kule walipofunja siendi kwa kuwa sitaki matatizo, sijafanyiwa fujo zaidi ya siku ile ambayo walivunja, lakini mpaka sasa (Machi 11, 2022) sijapata tatizo lolote.”
TAMKO LA SERIKALI, LAMSAKA MCHUNGAJI
Mkuu wa Wilaya wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja, Rashid Msaraka amezungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2022 baada ya kufika eneo la tukio.
“Mamlaka zinazohusiana na utabiri wa hali ya hewa, zimetoa tathmini yao kuhusu mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni, nikatoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuwa na tahadhari ya maeneo hatarishi, moja kati ya maeneo hayo ni hiyo iliyobomolewa.
“Nyumba mojawapo iliyobomolewa ni nyumba ya kawaida lakini taarifa inayosambaa ni kanisa, hapana mimi sina kibali cha kujengwa kwa kanisa.
“Hivyo, imevunjwa kwa kuwa ni sehemu ya nyumba zilizokuwa hatarishi, tunaweka mazingira sawa, siyo hapa tu bali ni maeneo yote.
“Yote yanayoendelea mitandaoni kuwa kuna maandalizi ya vita ya Waislamu dhidi ya Wakristo siyo kweli.
“Katika taarifa zinazosambaa kuna mtu anaitwa David Suna, sijui kama ni kiongozi wa kawaida au kiongozi wa dini, hatumfahamu, nimempa maelekezo Kamanda OCD kumtafuta huyo Daudi Suna ili kutoa maelezo ya kinachoendelea mitandaoni.
“Sisi tumemwambia ODC hiyo clip inayosambaza ni mbaya na ni ya uchochezi.
“Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu ana haki ya kuambudu lakini lazima kuwe na utaratibu.
“Nasisitiza kuwa hapakuwa na kanisa, kulikuwa na nyumba za kuishi. Tunatoa taarifa kuwa hakuna rabsha yoyote.
“Tumewaambia wale ambao wanaona hawajatendewa haki basi waje watuambie lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza.
“Tutahakikisha tunawalinda raia wote bila kuwa na ubaguzi, usalama wa raia wa kila mtu ni muhimu. Zanzibar ni sehemu ambayo ina historia ya kuw ana makanisa tangu enzi na enzi, hatutamvumilia mtu au watu ambao watakuwa wanania ya kuharibu taswira ya Serikali ya Zanzibar.”
Pia Soma~~ Zanzibar: Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna, yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo
We jamaa vipi badala unatumia akili mbovu sana kuhalalisha huu unyama wa mkuu wa wilaya. Kila mtu ana uhuru wa Kuabudu aisee kinyume na hapo ni uvunjaji wa katiba. Mama Samia kamata mkuu wa wilaya na hiyo manispaa tumeanza kurudi tukipotoka miaka ya kikwete
Kuna maeneo Bara wakazi woote ni wakristo, ila msikiti ukijengwa hapo wenyeji hawajali. Unawashauri nini wakazi kama hao?
Ebu tuambie serikali imesema hivyo kwa katiba gani?au unajikosha tu humu...na kuleta propaganda za kijinga.Zanzibar ni nchi ya kiislamu, kwahiyo uhuru huo unaozungumzia huwa una mipaka mkuu. NI tofauti kabisa na Bara
Mzanzibari ni nani ?utambulisho wa mzanzibar hauhusiani na ukaazi. Hapa tunazungumzia uzanzibari na sio ukaazi. hivo ni vitu viwili tofauti.
Kwa hyo mabwabwa Wana thaman kubwa huko zenji?
Ila tambueni dini tumeletewa na mkoloni
Watu hawajiulizi mbona hakuna nabii mwenye rangi nyeusi yaan mwafrika ina maana SS weusi tulitengwa hatukuhtaji dini
Watakatifu wote watu weupe weus n wakuhesabu Sana Tena had tuwalazmishe
Msikitini lugha n kiarabu TU Kwan MUUMBA hasikii kiswahili kwann tusiswali kiswahili ili kila mtu aelewe?
TUJIOKOE KIFIKRA
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Si muondoke Tu wavamizi mkajenge makanisa mpaka vyooni huko kwenu Tanganyika , ?Kwa akili zako ndefu unaona nyie huwa hampigi kelele?
Au kwa vile tunawavumilia tu mnaona mko Sawa?
Mzanzibari ni nani ?
Ebu tuambie serikali imesema hivyo kwa katiba gani?au unajikosha tu humu...na kuleta propaganda za kijinga.
#MaendeleoHayanaChama
Siongei na sheria naongea na wewe hapa mkuu.Mbona sheria ya nani mzanzibari ipo Zanzibar.
Hawa jamaa wakiwa majority wanakua miyeyusho sana kwa wanachofanyiwa china au myamar ni sawa kwa kua wao niwachache ?Mkuu Zanzibar ni nchi ya kiislamu, 99% ya watu wake ni waislamu, kwahiyo hakuna cha ajabu kuwa na mifumo ya kiislamu kwenye maisha yao, ni tofauti na Bara ambapo uwiano wa dini hizi mbili ni mkubwa nearly 50 - 50, So cha muhimu ni kufahmu kuwa haiwezekani mazingira ya Zanzibar yakawa sawa na Bara. Tujaribu kulitathmini kwa uandani na sio kuishabiki. Tatizo kuu la Zanzibar ni suala la Makanisa kuwa yanaengezeka kwa kasi kila siku zinavyokwenda, Na hilo linawafanya wananchi wao wengi kuwa insecure. Nchi nyingi ambazo ziko dominated na dini moja kwa zaidi ya 90% ni lazima watu wa dini nyengine wata experience mambo kama hayo, na hasa wakiwa Wageni.
Siongei na sheria naongea na wewe hapa mkuu.
Nakuuliza wewe mzanzibar ni nani ?
Na moja ya mafunzo ni kuvunja vitu / kuharibu au kukataza watu wasio sawa na wewe ?Mkuu Zanzibar ni nchi ya kiislamu, 99% ya watu wake ni waislamu, kwahiyo hakuna cha ajabu kuwa na mifumo ya kiislamu kwenye maisha yao, ni tofauti na Bara ambapo uwiano wa dini hizi mbili ni mkubwa nearly 50 - 50, So cha muhimu ni kufahmu kuwa haiwezekani mazingira ya Zanzibar yakawa sawa na Bara. Tujaribu kulitathmini kwa uandani na sio kuishabiki. Tatizo kuu la Zanzibar ni suala la Makanisa kuwa yanaengezeka kwa kasi kila siku zinavyokwenda, Na hilo linawafanya wananchi wao wengi kuwa insecure. Nchi nyingi ambazo ziko dominated na dini moja kwa zaidi ya 90% ni lazima watu wa dini nyengine wata experience mambo kama hayo, na hasa wakiwa Wageni.
Siongei na sheria naongea na wewe hapa mkuu.
Nakuuliza wewe mzanzibar ni nani ?