Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

Sasa si ni wachache hamna nguvu na mmejificha, sasa kama wewe si ajabu una jina la kizungu ambalo hutafsiriwa ni mkristo na hata kwa watu zako wa karibu wanajua ni mkristo huambii kuwa mimi ni mkana Mungu.
Sasa hapo hata wewe ukienda kuvunja kanisa, kufanya ujambazi n.k nani atajua kuwa ni atheist?
Weka mbali hoja yako ya uchache na anonymity, Atheist hana sababu ya kufanya uharibifu wa nyumba za ibada

Ishu ya majina nowdays sio hoja ya ku-describe imani ya mtu (religion perspective)

Ukiwa mbeya wakina abdalla ni wengi, kina mwamedi, kina khadija, zuberi, asha, saidi ni wengi lakini utashangaa ukiambiwa hao wote sio waislamu na watakushangaa kwanini uwahusishe na uislamu
 
Nenda mahakamani kama una ushahidi, pia kwanini hamtaki kujitoa kwenye muungano?

Mahakama ya mvamizi hahaha! Hatutaki kujitoa au hamtaki kuondoka. Si muondoe majeshi yenu yaliyojaa kila mtaa.
Kwa nini mnakuja kutuuwa kila uchaguzi huku mkiweka vibaraka wenu?
 
Weka mbali hoja yako ya uchache na anonymity, Atheist hana sababu ya kufanya uharibifu wa nyumba za ibada

Ishu ya majina nowdays sio hoja ya ku-describe imani ya mtu (religion perspective)

Ukiwa mbeya wakina abdalla ni wengi, kina mwamedi, kina khadija, zuberi, asha, saidi ni wengi lakini utashangaa ukiambiwa hao wote sio waislamu na watakushangaa kwanini uwahusishe na uislamu

Hivi hujasoma hata historia wakomunist wamefanywa nini Soviet Union Na wanafanya nini China?
 
Ila kiukweli huo unaoita uvumilivu ni pale tu ambapo hamjaguswa sehemu zenu ila ukiguswa hakuna uvumilivu.
Huku bara wanaolalamika ubaguzi (mfumo kristo) siku zote ni waislamu ila majibu mnayowajibu ni kuwa hawana elimu wanapenda kulalamika na maneno mengi ya karaha.
Kwani ni uongo?
 
Mali gani mnayotupa Bure ? Labda kuja kutuuwa , kututia vilema Na kutuvutugia nchi Na kuweka vibaraka wenu kila ufikapo uchaguzi
Kaa ulee mimba..zenji ni koloni la Tanganyika maisha..

#MaendeleoHayanaChama
 
Weka mbali hoja yako ya uchache na anonymity, Atheist hana sababu ya kufanya uharibifu wa nyumba za ibada

Ishu ya majina nowdays sio hoja ya ku-describe imani ya mtu (religion perspective)

Ukiwa mbeya wakina abdalla ni wengi, kina mwamedi, kina khadija, zuberi, asha, saidi ni wengi lakini utashangaa ukiambiwa hao wote sio waislamu na watakushangaa kwanini uwahusishe na uislamu
Ndio nakwambia kwamba huwezi kumjua huyo atheist, wewe ukiamua kuvunja msikiti nani atajua kuwa ni atheist?
 
H
Siku chache tangu kuripotiwa kwa taarifa za kuvunjwa kwa Kanisa la T.A.G lililopo Sebleni, Unguja ripoti kamili ya kilichotokea imetolewa kutoka upande wa kanisa pamoja na upande wa Serikali ya Zanzibar.

Mchungaji wa kanisa hilo linaloelezwa kuwa limevunjwa, David Victor Suna amefunguka kilichotokea kwa kusema:

MCHUNGAJI AFUNGUKA
“Ni kweli wamevunja nyumba yetu ya ibada licha ya kutambua kuwa tuna uhalali wa kila kitu, na suala hilo kwa sasa lipo kwa wanasheria wetu wanalishughulikia.

“Eneo hilo nilinunua kihalali kabisa kwa Sh milioni 16 na wakati nanunua nilikuta kuna banda ambalo lilikuwa shemu ya mauzo ya kiwanja, nilichofanya nikaboresha kwa kujenga ukuta.

“Lakini baada ya kuanza kuwa tunasali, nikapata malalamiko kuwa wakazi wa hapo hawataki kanisa, wakawa wanakuja viongozi kadhaa wa Serikali kukagua wakiniambia malalamiko ya uwepo wa kanisa letu mahali hapo.

“Kwanza waliniambia nimejenga ukuta kimakosa, kwa kuwa sina kibali cha kujenga ukuta, nikawaambia sawa hilo nakiri kwa kuwa sikuwa najua kama ukta unahitaji kibali, nikawaambia nitafuata mchakato wa kupata kibali kwa mamlaka husika.

“Baada ya mvutano wa muda mrefu nilienda hadi kwa Mkuu wa Wilaya akaniambia kama kama ninataka kibali cha nyumba ya makazi ya kawaida nitapata lakini kama ni kuhusu kanisa hapo siyo sehemu sahihi na hawatanipa kibali kwa kuwa wakazi wa eneo hilo hawataki kanisa.

“Siku hiyo ndiyo nikashangaa wamekuja wakavunja kwa kutumia mgongo wa Manispaa. Viongozi wetu wakuu akiwemo Askofu Mkuu amesema niwe kimya, nisifanye chochote kwa sasa, wao ndiyo watakaotoa tamko kwa kuwa suala letu limefika ngazi ya kitafa.

“Mimi ni mkazi wa Unguja miaka mingi, najua wanachofanya ni kitu ambacho wanakifanya muda mrefu, kuna upande ambao unakuwa una nguvu kubwa kiimani kuliko mwingine.

“Mimi kwa sasa nipo kimya, hata kule walipofunja siendi kwa kuwa sitaki matatizo, sijafanyiwa fujo zaidi ya siku ile ambayo walivunja, lakini mpaka sasa (Machi 11, 2022) sijapata tatizo lolote.”

TAMKO LA SERIKALI, LAMSAKA MCHUNGAJI
Mkuu wa Wilaya wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja, Rashid Msaraka amezungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2022 baada ya kufika eneo la tukio.

“Mamlaka zinazohusiana na utabiri wa hali ya hewa, zimetoa tathmini yao kuhusu mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni, nikatoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuwa na tahadhari ya maeneo hatarishi, moja kati ya maeneo hayo ni hiyo iliyobomolewa.

“Nyumba mojawapo iliyobomolewa ni nyumba ya kawaida lakini taarifa inayosambaa ni kanisa, hapana mimi sina kibali cha kujengwa kwa kanisa.

“Hivyo, imevunjwa kwa kuwa ni sehemu ya nyumba zilizokuwa hatarishi, tunaweka mazingira sawa, siyo hapa tu bali ni maeneo yote.

“Yote yanayoendelea mitandaoni kuwa kuna maandalizi ya vita ya Waislamu dhidi ya Wakristo siyo kweli.

“Katika taarifa zinazosambaa kuna mtu anaitwa David Suna, sijui kama ni kiongozi wa kawaida au kiongozi wa dini, hatumfahamu, nimempa maelekezo Kamanda OCD kumtafuta huyo Daudi Suna ili kutoa maelezo ya kinachoendelea mitandaoni.

“Sisi tumemwambia ODC hiyo clip inayosambaza ni mbaya na ni ya uchochezi.

“Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mtu ana haki ya kuambudu lakini lazima kuwe na utaratibu.

“Nasisitiza kuwa hapakuwa na kanisa, kulikuwa na nyumba za kuishi. Tunatoa taarifa kuwa hakuna rabsha yoyote.

“Tumewaambia wale ambao wanaona hawajatendewa haki basi waje watuambie lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza.

“Tutahakikisha tunawalinda raia wote bila kuwa na ubaguzi, usalama wa raia wa kila mtu ni muhimu. Zanzibar ni sehemu ambayo ina historia ya kuw ana makanisa tangu enzi na enzi, hatutamvumilia mtu au watu ambao watakuwa wanania ya kuharibu taswira ya Serikali ya Zanzibar.”

Pia Soma~~ Zanzibar: Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna, yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo
Hivi kuna makanisa mengine zaidi ya yale ya Mji Mkongwe la waanglikana na la wakatoliki?

Amandla...
 
Mungu awalaani hayo mavaa kobazi itafkia pahala Tanzania itapasuka
 
Back
Top Bottom