BenKaile
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 443
- 375
Naona watu hapa kwenye huu uzi wanafanya utani na kebehi tu kisa muonekano wa kanisa au jambo lilivyotokea, nadhani baada ya hayo tuzidi kujikita ndani katika kujiimarisha kwenye afya ya akili zetu. Kwanza fikra madhubuti, mawazo ya msingi na kujenga uhusiano mwema na jamii husika. Yaliyowakuta hawa wanandoa hatujui bado ila binadamu tunapitia mambo mengi mno na tunapaswa kuwa na nguvu ya kuyatatua bila kujenga majeraha au madhara makubwa kama haya ya kifo. Mchungaji hakuwa mwendawazimu mpaka kuyaandika wazi kitakacho mfikisha kufanya alichofanya kwa mkewe na kwake binafsi, sio jambo jema kabisa alilotenda ila liwe somo na onyo kwetu tunaoendelea kupata pumzi ya bure ya Mwenyezi Mungu.
NB: Dunia ya sasa ni chafu sana, utacheka hapa ila kesho jambo la aibu na ajabu linaweza kukukaribia. Chukua hatua!
NB: Dunia ya sasa ni chafu sana, utacheka hapa ila kesho jambo la aibu na ajabu linaweza kukukaribia. Chukua hatua!