Mchungaji apandishwa kizimbani kwa biashara haramu

paulk

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
240
Reaction score
3
Mchungaji Jean Felix wa kanisa la assembles of God apandishwa kizimbani Moshi, kwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza watu nje ya nchi, ambapo alifanya jaribio la kuwatorosha watoto wawili kutoka Moshi hadi DSM ambapo alishtukiwa na kutiwa nguvuni na leo kusomewa mashtaka na baadae kurudishwa rumande.

source: TBC1

============

MCHUNGAJI Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo(DRC) Jean Felix Bamana (45) amesomewa mashitaka akiwa kitandani katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi mjini Moshi, akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha binadamu.

Mchungaji Bamana ambaye ni mlemavu wa miguu, aliibua mvutano mkubwa ndani ya Jeshi la Polisi na serikali, alikamatiwa jijini Dar es Salaam akiwa na watoto wawili ndugu ambao aliondoka nao mjini Moshi, kwa ahadi ya kwenda kuwatafutia shule.

Alisomewa mashitaka hospitalini baada ya kugoma kupelekwa mahakamani tangu jumatatu wiki hii akidai ni mgonjwa huku askari wanaomlinda wakilalamika kuwa anafanya mchezo wa kuigiza.

Mshitakiwa huyo alisomewa mashitaka mawili ambayo yanaangukia kwenye sheria ya usafirishaji binadamu namba 6 ya mwaka 2008,mashitaka ambayo hayana dhamana hivyo kupelekwa rumande katika gereza kuu la mkoa wa Kilimanjaro la Karanga.

ZAIDI -> Mchungaji asomewa mashitaka hospitalini | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 
.....Ana mahusiano ya karibu sana na Mh. Mch. Dr. Mama Getrude Lwakatare... bila shaka dhamana itapatikana...
 
kaaaz kwel kwel, iyo ki2 c ilipigwa marufuku tokea enzi za mkoloni
 
Mbona hilo deal la kuuza wasichana nje ya nchi Rwekatare amelifanya siku nyingi sana?
 
Halafu wenye ndugu zao wakidunga RISASI wachungaji wa style kama hizi...kesi zote wanabambikiwa waislamu
 
Sheria haina dini.Mimi nadhani siyo sahihi kuhusisha makosa na dini, wala kauli kuwa sheria inapindishwa kwa dini fulani pia siyo sahihi hususani kwa Great Thinkers.Uharifu ni tabia ya mtu bila kujali ni wa dini au dhehebu gani.Bila shaka yeyote atakayebainika na ushaidi ukapatikana dhahiri sheria itachukua mkondo wake.

Kwa wapenda amani, waacha Mungu na wazalendo wa nchi hii inatupasa kukemea ubaguzi na ukiukwaji wa sheria wa aina yoyote.
 
Wewe ndio unasema hivyo...lakini matukio haya yapo mengi katika jamii ...viongozi wa dini wanafanya mambo ya ajabu sana....

Kwenye hili tukio ndugu wa hao watoto wangeamua kumshughulikia huyo mchungaji ungesikia kelele humu
Mara UAMSHO,PONDA ,FARIDI,WAVAA VIPEDO
 
Mbona hilo deal la kuuza wasichana nje ya nchi Rwekatare amelifanya siku nyingi sana?

"? " naona unakwepa kuwa shahidi katika kuisaidia polisi nadhani ndiyo maana umemalizia na alama hiyo ya kuuliza.
 
Mkuu wasikupe tabu yule padri Mushi kule zenji ni ishu ya madawa, then wameona waislam ndo wakuwasingizia
 
Mimi sitetei wala si shutumu mtu yeyote kwa vile sina vielelezo.Il ninachosema vitendo viovu vya aina hiyo havifanywi na viongozi wa dini tu, bali watu mbalimbali ndani ya jamii bila kujali nyazifa zao.Na hivyo niwajibu wa jamii kuwaadhibu na kukomesha maovu yote kwa njia za kisheria bila upendeleo wa namna yoyote
 
"? " naona unakwepa kuwa shahidi katika kuisaidia polisi nadhani ndiyo maana umemalizia na alama hiyo ya kuuliza.

.
Yule mama kauza mabinti wengi tu kwa wazungu wake wa unga. Hilo halina shaka kabisa.
.
 
.
Yule mama kauza mabinti wengi tu kwa wazungu wake wa unga. Hilo halina shaka kabisa.
.
Mkuu unajua hizi ni "serious allegations"...kama unaushahidi wa kutosha wa jambo hili kwa huyu mama na wengine wote wanaojihusisha na uharamia huu...nitakuwa wa kwanza kuchangia gharama za kuendesha kesi.
 
Ushahidi gani...?kila mtu anajua...
 
Mkuu unajua hizi ni "serious allegations"...kama unaushahidi wa kutosha wa jambo hili kwa huyu mama na wengine wote wanaojihusisha na uharamia huu...nitakuwa wa kwanza kuchangia gharama za kuendesha kesi.

.
Hiyo kesi utaendesha nchi gani? Tanzania? Binti akiuzwa ulaya ndugu wanafurahi mtoto wao kukwea pipa.
Baba akibaka wanasema tungejua je ni lijali?
Wewe hujamfuatilia mama Rwekatare akitoa ushuhuda jinsi anavyo wapatia wake buzi la la kidosi na kwamba ni jambo analojivunia na wapambe wake wanashangilia kwa vigele gele kwamba binti kapata buzi mdosi? Tanzania ni zaidi ya unavyoifahamu.
.
 
Halafu wenye ndugu zao wakidunga RISASI wachungaji wa style kama hizi...kesi zote wanabambikiwa waislamu

wewe una undugu wa Damu na Akina Isack Newton na Faradays bila shaka maana una Miakili sana sana sana! FBI wapewe visa kama hivi wazidi kupata Picha kamili na sahihi sio ile ya kuchorwa CCM kisiwandui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…