Mchungaji Jean Felix wa kanisa la assembles of God apandishwa kizimbani Moshi, kwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza watu nje ya nchi, ambapo alifanya jaribio la kuwatorosha watoto wawili kutoka Moshi hadi DSM ambapo alishtukiwa na kutiwa nguvuni na leo kusomewa mashtaka na baadae kurudishwa rumande.
source: TBC1
============
MCHUNGAJI Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo(DRC) Jean Felix Bamana (45) amesomewa mashitaka akiwa kitandani katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi mjini Moshi, akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha binadamu.
Mchungaji Bamana ambaye ni mlemavu wa miguu, aliibua mvutano mkubwa ndani ya Jeshi la Polisi na serikali, alikamatiwa jijini Dar es Salaam akiwa na watoto wawili ndugu ambao aliondoka nao mjini Moshi, kwa ahadi ya kwenda kuwatafutia shule.
Alisomewa mashitaka hospitalini baada ya kugoma kupelekwa mahakamani tangu jumatatu wiki hii akidai ni mgonjwa huku askari wanaomlinda wakilalamika kuwa anafanya mchezo wa kuigiza.
Mshitakiwa huyo alisomewa mashitaka mawili ambayo yanaangukia kwenye sheria ya usafirishaji binadamu namba 6 ya mwaka 2008,mashitaka ambayo hayana dhamana hivyo kupelekwa rumande katika gereza kuu la mkoa wa Kilimanjaro la Karanga.
ZAIDI -> Mchungaji asomewa mashitaka hospitalini | Fikra Pevu | Kisima cha busara!