Mchungaji apata kipigo, anusurika kuuawa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu

Mji wote ulizizima! Mchungaji mashuhuri, anayeheshimika kwa mahubiri yake makali ya utakatifu, alijikuta kwenye kashfa nzito baada ya kufumaniwa na mke wa mtu. Tukio hilo la kushtua lilitokea katika mji mmoja huko Mashariki ya Kati, na chanzo chetu cha kuaminika kimedokeza kuwa Mchungaji huyo alitumia mamlaka yake kumshawishi mke wa mmoja wa waumini wake na hatimaye kuingia katika uhusiano wa siri.

Mume wa mwanamke huyo, ni mwanajeshi jasiri aliyekuwa mstari wa mbele katika ulinzi wa taifa. Alipotakiwa kwenda vitani, Mchungaji huyo alipata nafasi ya kutimiza tamaa zake za mwili. Lakini kilichofuata ni zaidi ya sinema! Mchungaji alipoona kuwa mambo yameharibika, alihakikisha kuwa mume wa mwanamke huyo anashiriki katika mapambano makali zaidi ya vita, ili afe vitani.

Baada ya kifo cha mwanajeshi huyo, Mchungaji alimuoa mke wake kwa haraka, akidhani kwamba siri yake ingefunikwa milele. Lakini mambo hayakuishia hapo! Chanzo chetu cha kuaminika kinasema kwamba japo alijaribu kuficha, mwishowe ukweli ulijulikana, na familia yake ilipata mapigo mazito. Hadi leo, tukio hilo linaendelea kusimuliwa kila mahali duniani.

Najua unafurahia kusikia habari mbaya, hasa za Watumishi wa Mungu, ndicho kilichokuvuta hapa. Kwani wewe ni mtakatifu? Hesabu dhambi ulizofanya tangu mwaka huu uanze. Si umefanya zaidi ya huyo Mchungaji? Huyo Mchungaji alitubu. Wewe umetubu dhambi zako? Tubu haraka. Kuna mapigo mazito yanaandaliwa kwa ajili ya watu watendao dhambi. Soma Ufunuo wa Yohana.

Kwa habari zaidi za Mchungaji huyo soma 2 Samweli sura yote ya 11 na ya 12.
Pumbavu mie najua udaku wa kweli kumbe story za kuburudisha wajinga
 
Humu ndani tunazidiana akili mjue, ni ngumu kudanganya members wa humu wanaitwa great thinker. Sasa ukiweka picha ya mwanamke kuwa avator yako huku we ni mwanaume na maandiko yako hayaoneshi kuwa ni mwanamke mada unazoleta zitakosa mvuto. Kama we si mwanamke bora uweke picha nyingine au usiweke picha kabisa. Hizi ID/AVATOR zina athiri mada za mhusika positivelly or negativelly kwa wasomaji. Members wengine wanaonekana ni vituko, walevi, wahuni, matapeli, wehu, wacha Mungu, waabudu shetani, akili fyatu, makahaba, wezi, wakora, magaidi, wabishi, wasaliti, mafisadi, watakatifu, walafi, na wengine wengi kutokana na ID/AVATOR zao zinasadifu jinsi walivyo ji brand humu. Ukiandika ujumbe wasomaji wana refer na ku compare na ID/AVATOR yako kama vinaendana na kushabihiana
 
Mi binafsi nimeshindwa kukuelewa lengo lako hasa la kuandika nyuzi zako. Kwanza ni ID mpya humu huenda ni member mpya. Hiyo ID yako na namna unavyoandika humu haviendani na unavyonekana kwenye ID/profile. Picha ni ya kike ila maandiko ni ya kiume, bila shaka we ni mwanaume uandishi wako unaonesha. Bora avator yako uweke kitu kingine, ondoa hiyo picha ya mwanamke we si mwanamke huyo
Comment yako ni dharau ya waziwazi kwa wanawake. Chunga ulimi wako, mkuu.
Mithali 14:21 SRUV
"Amdharauye mwenzake afanya dhambi.."
 
Humu ndani tunazidiana akili mjue, ni ngumu kudanganya members wa humu wanaitwa great thinker. Sasa ukiweka picha ya mwanamke kuwa avator yako huku we ni mwanaume na maandiko yako hayaoneshi kuwa ni mwanamke mada unazoleta zitakosa mvuto. Kama we si mwanamke bora uweke picha nyingine au usiweke picha kabisa. Hizi ID/AVATOR zina athiri mada za mhusika positivelly or negativelly kwa wasomaji. Members wengine wanaonekana ni vituko, walevi, wahuni, matapeli, wehu, wacha Mungu, waabudu shetani, akili fyatu, makahaba, wezi, wakora, magaidi, wabishi, wasaliti, mafisadi, watakatifu, walafi, na wengine wengi kutokana na ID/AVATOR zao zinasadifu jinsi walivyo ji brand humu. Ukiandika ujumbe wasomaji wana refer na ku compare na ID/AVATOR yako kama vinaendana na kushabihiana
Tusiende nje ya uzi, mkuu. Tujadili kisa hicho. Umejifunza nini?
 
Mji wote ulizizima! Mchungaji mashuhuri, anayeheshimika kwa mahubiri yake makali ya utakatifu, alijikuta kwenye kashfa nzito baada ya kufumaniwa na mke wa mtu. Tukio hilo la kushtua lilitokea katika mji mmoja huko Mashariki ya Kati, na chanzo chetu cha kuaminika kimedokeza kuwa Mchungaji huyo alitumia mamlaka yake kumshawishi mke wa mmoja wa waumini wake na hatimaye kuingia katika uhusiano wa siri.

Mume wa mwanamke huyo, ni mwanajeshi jasiri aliyekuwa mstari wa mbele katika ulinzi wa taifa. Alipotakiwa kwenda vitani, Mchungaji huyo alipata nafasi ya kutimiza tamaa zake za mwili. Lakini kilichofuata ni zaidi ya sinema! Mchungaji alipoona kuwa mambo yameharibika, alihakikisha kuwa mume wa mwanamke huyo anashiriki katika mapambano makali zaidi ya vita, ili afe vitani.

Baada ya kifo cha mwanajeshi huyo, Mchungaji alimuoa mke wake kwa haraka, akidhani kwamba siri yake ingefunikwa milele. Lakini mambo hayakuishia hapo! Chanzo chetu cha kuaminika kinasema kwamba japo alijaribu kuficha, mwishowe ukweli ulijulikana, na familia yake ilipata mapigo mazito. Hadi leo, tukio hilo linaendelea kusimuliwa kila mahali duniani.

Najua unafurahia kusikia habari mbaya, hasa za Watumishi wa Mungu, ndicho kilichokuvuta hapa. Kwani wewe ni mtakatifu? Hesabu dhambi ulizofanya tangu mwaka huu uanze. Si umefanya zaidi ya huyo Mchungaji? Huyo Mchungaji alitubu. Wewe umetubu dhambi zako? Tubu haraka. Kuna mapigo mazito yanaandaliwa kwa ajili ya watu watendao dhambi. Soma Ufunuo wa Yohana.

Kwa habari zaidi za Mchungaji huyo soma 2 Samweli sura yote ya 11 na ya 12.
Hahahha yaan ulivyokuwa unasema nilikuwa na connect na habari za Mchungaji huyoo, na nilitaka niandike bonge la jibu nikushushue hahahha, "lakini hata wachungaji nao ni Binadamu so hutakiwi kumnyoshea mtu kidole" ni sawa na yule mwanamke aliepelekwa kwa kuhani Mkuu kuwa anastahili kupigwa mawe hadi afe kisa amekutwa akizini, yule kuhani akainama chini akisema mwenye ambae anajiona ni mtakatifu awe wa kwanza kurusha jiwe mwisho wakajikuta wako wawili kuhani na yule mwanamke.

Nawachukia watu wanaowasema watu vibaya kwa matendo yao utadhani wametengeneza dunia hii tunayoishi, kila mtu atasimama mbele za Mungu so fanya mambo yako na ukumbuke na ww utahukumiwa.

Na mm nimetoa mchango wangu kwa vijana wa Veta. Kama bado hujajiunga Veta naomba uje inbox na majin yako matatu na mahali ulipo. Nimechoka kuona vijana wa ovyo hahhaha
 
Hana jina na kanisa lake halina jina?

Huu muda umetumia kutumia akili yako kuandika umbeya ulioandika ungetumia kutafuta pesa ungekuwa mbali kimaisha
.tunga wazo la kupata pesa badala ya kutunga story za uongo unamaliza Mb za ubongo wako bure
Ujinga ni mzigo mzito, endapo mjinga hatakuwa tayari kusaidiwa kuondoa ujinga wake.
 
Mi binafsi nimeshindwa kukuelewa lengo lako hasa la kuandika nyuzi zako. Kwanza ni ID mpya humu huenda ni member mpya. Hiyo ID yako na namna unavyoandika humu haviendani na unavyonekana kwenye ID/profile. Picha ni ya kike ila maandiko ni ya kiume, bila shaka we ni mwanaume uandishi wako unaonesha. Bora avator yako uweke kitu kingine, ondoa hiyo picha ya mwanamke we si mwanamke huyo
Shoga la kiume hilo usiumize kichwa
 
Mji wote ulizizima! Mchungaji mashuhuri, anayeheshimika kwa mahubiri yake makali ya utakatifu, alijikuta kwenye kashfa nzito baada ya kufumaniwa na mke wa mtu. Tukio hilo la kushtua lilitokea katika mji mmoja huko Mashariki ya Kati, na chanzo chetu cha kuaminika kimedokeza kuwa Mchungaji huyo alitumia mamlaka yake kumshawishi mke wa mmoja wa waumini wake na hatimaye kuingia katika uhusiano wa siri.

Mume wa mwanamke huyo, ni mwanajeshi jasiri aliyekuwa mstari wa mbele katika ulinzi wa taifa. Alipotakiwa kwenda vitani, Mchungaji huyo alipata nafasi ya kutimiza tamaa zake za mwili. Lakini kilichofuata ni zaidi ya sinema! Mchungaji alipoona kuwa mambo yameharibika, alihakikisha kuwa mume wa mwanamke huyo anashiriki katika mapambano makali zaidi ya vita, ili afe vitani.

Baada ya kifo cha mwanajeshi huyo, Mchungaji alimuoa mke wake kwa haraka, akidhani kwamba siri yake ingefunikwa milele. Lakini mambo hayakuishia hapo! Chanzo chetu cha kuaminika kinasema kwamba japo alijaribu kuficha, mwishowe ukweli ulijulikana, na familia yake ilipata mapigo mazito. Hadi leo, tukio hilo linaendelea kusimuliwa kila mahali duniani.

Najua unafurahia kusikia habari mbaya, hasa za Watumishi wa Mungu, ndicho kilichokuvuta hapa. Kwani wewe ni mtakatifu? Hesabu dhambi ulizofanya tangu mwaka huu uanze. Si umefanya zaidi ya huyo Mchungaji? Huyo Mchungaji alitubu. Wewe umetubu dhambi zako? Tubu haraka. Kuna mapigo mazito yanaandaliwa kwa ajili ya watu watendao dhambi. Soma Ufunuo wa Yohana.

Kwa habari zaidi za Mchungaji huyo soma 2 Samweli sura yote ya 11 na ya 12.
walokole wataliwa sana kama wapenda madrasa na mashaik .dini kiwango cha kumfikia wasira uwezo
 
Hahahha yaan ulivyokuwa unasema nilikuwa na connect na habari za Mchungaji huyoo, na nilitaka niandike bonge la jibu nikushushue hahahha,
Duh, bado unaishi enzi za jino kwa jino. Pole sana
"lakini hata wachungaji nao ni Binadamu so hutakiwi kumnyoshea mtu kidole"
Hapo sijamnyoshea mtu kidole. Hiyo habari ni sehemu ya "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki..." 2 Timotheo 3:16-17 SRUV
ni sawa na yule mwanamke aliepelekwa kwa kuhani Mkuu kuwa anastahili kupigwa mawe hadi afe kisa amekutwa akizini, yule kuhani akainama chini akisema mwenye ambae anajiona ni mtakatifu awe wa kwanza kurusha jiwe mwisho wakajikuta wako wawili kuhani na yule mwanamke.
Hata mimi nimemaliza habari hiyo kwa namna hiyo hiyo. Si umeona comments za watu? Inaonekana walikuwa wamejiandaa kumtupia mawe huyo Mchungaji. Lakini nilipowageukia na kuwaambia: "Kwani wewe ni mtakatifu? Hesabu dhambi ulizofanya tangu mwaka huu uanze. Si umefanya zaidi ya huyo Mchungaji? Huyo Mchungaji alitubu. Wewe umetubu dhambi zako? Tubu haraka..."
Wamekimbia na kuniachia matusi 🙂

Nawachukia watu wanaowasema watu vibaya kwa matendo yao utadhani wametengeneza dunia hii tunayoishi, kila mtu atasimama mbele za Mungu so fanya mambo yako na ukumbuke na ww utahukumiwa.
Nimeishakuambia hiyo habari imeandikwa ili iwe fundisho kwetu na kutuonya.
 
Hv mkuu umeolewa? nataman mke mwenye itikad kama yako hakika watoto watakuwa kwenye misingi imara.
Usitafute mke kwenye mitandao, utaangukia pua. Muombe Mungu, atakupa mke anayekufaa.
Mithali 19:14 SRUV
"...mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA."
 
Duh, bado unaishi enzi za jino kwa jino. Pole sana

Hapo sijamnyoshea mtu kidole. Hiyo habari ni sehemu ya "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki..." 2 Timotheo 3:16-17 SRUV

Hata mimi nimemaliza habari hiyo kwa namna hiyo hiyo. Si umeona comments za watu? Inaonekana walikuwa wamejiandaa kumtupia mawe huyo Mchungaji. Lakini nilipowageukia na kuwaambia: "Kwani wewe ni mtakatifu? Hesabu dhambi ulizofanya tangu mwaka huu uanze. Si umefanya zaidi ya huyo Mchungaji? Huyo Mchungaji alitubu. Wewe umetubu dhambi zako? Tubu haraka..."
Wamekimbia na kuniachia matusi 🙂

Nimeishakuambia hiyo habari imeandikwa ili iwe fundisho kwetu na kutuonya.
Yaani sijasema ww unamnyooshea mtu kidole ila kuna watu, nimejaribu tuu kuelezea rafiki yangu ila umeeleza vzr sanaa
 
Back
Top Bottom