Mchungaji Gwajima amejibu tuhuma za mume wa Flora Mbasha?

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
Mume wa Flora Mbasha katikat ya mwaka huu baada ya kutifuana na mkewe alimnyoshea kidole Mchungaji Gwajima kuhusika na mkasa katika ndoa yake na mkewe Flora. Tuhuma nzito zilielekezwa kwa Mchungaji huyo anayejulikana Tanzania kwa kukusanya umati mkubwa wa watu katika mikutano yake.

Tuhuma nzito zaidi zilizoelekezwa kwake kama nukuru ya barua hiyo hapo chini zinazoonekana kuwa na uzito wa juu ni:

  1. Mchungaji Gwajima kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Flora Mbasha (mke wa mtu).
  2. Mchangaji huyo kuhusishwa tuhuma za biashara ya kuuza unga.
  3. Kumkingia kifua Flora na kutaka kumfungulia mashtaka mume wake anayelalamika kuibiwa mke wake.
Kwa vile mchungaji ni public figure, na kadiri ya maadili ya utume wake alipaswa kutolea ufafanuzi na kujenga utetezi kuwaondolea dukuduku waumini (kondoo) wake na ulimwengu.

Je hilo mchungaji Gwajima amelifanya?


 
Elimu ni ufunguo wa maisha.

Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa.

Ndoa haijengwi na wapambe, haisimami kwa nguvu wala vitisho.

Mbasha na washauri wake, including wewe muandika mada, mngekuwa na elimu ama ya duniani ama ya Mungu, msingeandika barua kama hii kwenye magazeti na kama haitoshi sasa mnaileta jamii forums. Huu ni ujinga.

Laiti kama Mbasha angelikuwa na Mungu, asingefuata ushauri wenu wapambe ambao badala ya kujenga upya mahusiano yake kwa maslahi ya familia, ndiyo mnazidi si kupanua nyufa bali kuangusha kuta kabisa.

Ninajua Ema na Flora walikotoka. Emma anaonyesha uchungu mkubwa sana na kwa barua hii, amekata tamaa na anajiona hana namna kama mfamaji. Laiti kama angelijua, asingewashirikisha ninyi mazandiki mnaozidi kumpa machungu. Ndoa haijengwi kwa shinikizo na wala haijengwi na nguvu zozote za nje ya wawili.

Huwezi kusema unampenda mke wako na unamhitaji arudi kwako kwa manipulations na ku mu embarrass. Hamwezi kujenga ndoa kwa sheria za jamii, lazima ama kuogopa aibu. Mnaanikamambo ya chumbani hadharani inabaki radha ya ndoa tena? Emma ameyakuza mwenyewe kwa kudhani ninyi mazabizabina mnamshauri vizuri!.

Kama mlitaka Mchungaji gwajima ajibu, kwa nini mlipeleka waraka huu gazetini wakati mnapafahamu anakopatikana? Huu ni wehu na ndiyo umewafanya ninyi mvunje ndoa ya Mbasha. Kwanza mnajuaje Gwajima alisoma hayo magazeti yenu au kama anasomaga hapa jamii forum?

Mnajichora ni namna gani hamna elimu ya darasani, hekima ya kurithi na maadili ya asili wala hamna hekima yaa Mungu ndani yenu. Mnaishi kwa mivumo ya kelele za upepo.

Nawapa tahadhari, huko mnakoelekea mnatafuta mauti. Shauri lenu, endeleeni na ujinga wenu.
 
Hivi ile kesi inaendeleaje au imefikia wapi kwa mlio na updates?
 
utajibu vipi mtu unayemchapia mkewe??

umaskini ni soo...
 

Makala kama hizi mnapeleka gazetini.mnatuchosha na maneno mengi point ni moja tu
 

Gwajima nimesema ni public figure, na kama amekuwa na unyofu wa moyo maungamo au kukanusha ni uanaume, lakini kunyamaza ni dalili kisaikolojia kukiri kosa bila kujutia na kuondoa wingu linazofunika ndoa ya wenyewe. Mchungaji kuhusishwa na tuhuma za matatizo ya wanandoa si jambo dogo, hawa ni kondoo wake anaowachunga.
 
Tunapata fursa ya kujifunza hapa,makanisa yanayoibuka kila kukicha ni makao ya shetani,acheni kuwaamin hawa wanaojiita manabii dhid ya wake zenu,hawa n nyoka wnye sumu kali,UKIONA MKE HAKUELEWI MPE GREEN LIGHT MAPEMA AKAOLEWE NA NABII,UBAK NA AMAM ROHONI.
 
Kunyamaza pia neno,huyo Mbasha angenyamaza akamuachia Mungu...........
 
Kunyamaza pia neno,huyo Mbasha angenyamaza akamuachia Mungu...........

Ndugu kukaa kimya kwa mambo ya namna hii ni kujiua polepole,ni bora aseme kuinusuru nafsi yake,then napata taabu zaidi na ukimya wa mchungaji Gwajima!!!kwa maelezo ya Emma nadhani Kuna elements za ukweli!!!
 
Ndugu kukaa kimya kwa mambo ya namna hii ni kujiua polepole,ni bora aseme kuinusuru nafsi yake,then napata taabu zaidi na ukimya wa mchungaji Gwajima!!!kwa maelezo ya Emma nadhani Kuna elements za ukweli!!!
sijui kwakeeli lakini ningekua mimi ningenyamaza tuu na chozi la mwenye kuonewa mwenye mungu hulipokea na ukizingatia ni mkewe hali wa ndoa,kama kweli ameonewa huyo Gwajima na mkewe hawato fumba jicho bila ukweli kujulikana........
 
Sasa hapa una mend ndoa ya Ema au unapigana na Gwajima? Maana hueleweki.

Gwajima hataki kuitikia mchezo wa kijinga unaotaka kumchezesha. Ana akili za kuu kuliko ninyi, kanyamaza kwa kuwa anaona kujibishan na watu wenye akili kama zenu ni kujidharirisha. Na ndoa ya Emma ndiyo hiyo mnazidi kuizika,kwa kudhani mnatumia akili kumbe ni makamasi.

Sasa mnafanya nini?? Acheni wehu!.

Hata kama ni mimi ningekuwa Gwajima, nisingejibizana na watu wenye kiwango cha chini kama chenu. Mnafanya fujo kama vibaka wa mahusiano? Mmekosa elimu hata ushauri wa wenye hekima hamna? Acheni upuuzi wenu huu.

Endeleeni kudanganyana, mwisho wake mtajutia nakwambia. Ninyi ndiio mmekuwa mawakala wa uharibifu kuliko kitu chochote.

MWAMBIENI EMA AWAELEZE, TATIZO LAKE NA FLORA LIMEANZA BAADA YA FLORA KWENDA KUSALI KWA GWAJIMA? MSITAKE KUMFANYA GWAJIMA MBUZI WA SHUGHULI, MKADHANI WOTE NI WAJINGA.



 
Mnalalamika Flora kwa nini apewe fedha na utajiri wa ghafla. Millioni 20 ni utajiri?

Kwa hiyo bila hizo fedha ndoa yao ingekuwa imara?

Tatizo ni pesa, ndoa ama Gwajima?

Msktake kutafuta sababu, tatizo la ndoa yao si la leo. Flora aliolewa na Ema akijua ni mtoto wa maskini hana kitu. Kama angelikuwa anatafuta pesa, kwa nini hakutafuta wenye nazo?

Gwajima alarundikiwa mzigo kwa kumpa financial confidence (kama ni kweli), Flora kitu ambacho nakiona kwe Emmanuel ni utashi (kama yalivyo madume mengi) kwa kulazimisha wanawake wakae kwenyehimaya yao kwa sababu ya economic dependency wala si mapenzi.

Mnataka kusema Flora kukaa na Mbasha bia mapenzi ila ni kwa kuwa hana namna ya kuishi, ndio uimara wa ndoa?

Acheni huo ujinga. Mmemharibia Emma ndoa yake kwa kumshauri vibaya na sasa itabidi mlinywe. Angepata washauri wazuri, pengine alikuwa na uwezo wa kumend uhusiano wao badala ya kusingizia matokeo kuwa ndiyo sababu.

Wehu!


 
Sasa hiyo mbasha anashindwa hata kumanage mkewe mpaka apeleke shituma magazetini .Kama mwanaume kweli siande mwenyewe kwa Gwajima na kumwonya kuhusu mahusiano yake na mkewe badala ya Kuna kuyaongelea huku mitandaoni.Naanza kuwa na wasiwasi na uanaume wake kama kichwa cha familia
 

Usiombe yakukute ya mwenye nguvu kushindana na mlalahoi. Mfalme Daud alimtamani mke wa Uria Mhiti, alipomwita na kuonja tu utamu wake, akaamuru Uria Mhiti vitani awekwe mbele eneo lenye wapiganaji wakali auawe. Alifanikiwa na kisha kumtia kiulaini mke wa Uria Mhiti kuwa mke wake. Historia ni mwalimu, hayo niongeleayo ni kutoka Biblia.
 
Jamani hii move bado inaendelea?
 
Mungu atamlipia mke anauma hasa akichukuliwa na mwenye nazo unabak kutazama tu machoz yk yataleta majibu cku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…