Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Viongozi wote wakienda kwenye ibada hupiga magoti kuomba mungu.
 
Tatizo taifa letu linawazee na viongozi wa dini waoga sana, kazi za wazee na viongozi wa dini ni kuwaonya vijana.
 
ikumbukwe kuwa makonda amewafanyia wengi mabaya na wale wote ambao wameonewa na makonda kwa namna zote ndiyo hao hao wameamua kumchimba kwa undani zaidi japo makonda na yy kaingiza pesa nyingi kuwanunua wale wote ambao wametajwa na Gwajma, kuna vioja vinakuja yaani ile ile style ya Steven nyerere, watu wote watapewa pesa na Dalali watakuwa pasco na Steven nyerere watachukuliwa watapelekwa kuongea na vyombo vya habari watakanusha kila kitu ndipo utajua kuwa pesa ni Adui wa Ukweli pia ni kikwazo cha vita juu ya vyeti feki.
 

Baba na Mama walikuwa kwenye mahojiano Clouds last week, haikuwekwa vizuri issue hii. Miaka wanayosema amesoma Pamba Sekondari, Mkuu wake wa shule namfahamu sana, and she used to be a very good friend.....Hata mimi nautafuta huu ukweli, kwa hiyo navuta waya muda si mrefu.
 
Kuita kiumbe kwani wewe siyo kiumbe? Hili nalo ni shida kwani? Makonda aka Bashite ni kiumbe yule. Au unadhani mwanadamu ni mungu? Maana hata malaika ni viumbe. Hebu hapo rekebisha Paskally. Pia sijaona pungufu lolote kwa yeye kutaja historia ya Bashite ambaye alihama Kolomije kwenda Mwanza na akadunda la saba.
 
Kama Makonda angemjua ni mtumishi wa Mungu asingemhusisha na kashfa hii kubwa ya madawa ya kulevya na asimkute na ushahidi wowote.Mwacheni aongee apate ahueni wa fikra.Hiyo kashfa siyo ya kitoto
 
Nawewe hii kitu umeiandika kishabiki, huoni kwamba huyu ni whistleblower mzuri sana katika kipindi hiki cha vyeti feki? cha kufanya vyombo vinavyohusika vifanyie kazi hii taarifa kama ni ya kweli makonda awajibishwe kama ni uongo Gwajima awajibishwe, suala la kwamba ni uongo au ukweli hutakiwi kulizungumzia wewe hapa, mimi ninafahamu mtu akipata zero hupewa Result slip sasa sijui gwajima angetumia jina gani rahisi la kiswahili la result slip. Na ishu aliyosema kwamba yeye kugombea urais au ubunge ni demotion kwake anaweza kua sahihi kabisa kwasababu amezungumza kiroho zaidi ndiyo maana Rais akiingia ibadani anakua mnyenyekevu sana anaweza kushikwa mpaka sharubu na mtumishi wa Mungu katika mchakato wa kumuombea.
 

Kiutendaji ni kweli kabisa mchungaji ni zaidi ya Watawala,kwa maana kwamba wanafanya kazi ya Mungu.Ni kiimani zaidi kuliko kisiasa
 

Hapana Mkuu. Issue ya vyeti haiko vile. Ni ngumu sana kufuta nyayo zake. Hata ukifunika kiana, watakuja watu watathibitisha kwamba hukuwahi kusoma katika darasa lile. Ni ngumu sana kufunika hii kitu, labda watu waamue tu makusudi kutochukua hatua..
 
Mkuu hawa wote ni viongozi mmoja wa kiroho na mwingine wa umma na wote wapo Dsm hivyo siyo busara kugombana waziwazi, busara za wazee zitumike, hawa wazee wakina Warioba, Paul Bomani, Mangula ndiyo kazi zao hizi.
Wazee wa CCM hao ............ Tangu lini ulishaona Mzee wa Kitanzania akija hadharani na kusema maneno na akayasimamia mpaka mwisho!!?

Tena Mzee wa CCM .......................!! Kama akina Mwinyi, Mkapa wanashindwa kusema hadharani bila kuuma wala kumungunya unategemea nani atakayeweza huko CCM!!
 
Kama Makonda angemjua ni mtumishi wa Mungu asingemhusisha na kashfa hii kubwa ya madawa ya kulevya na asimkute na ushahidi wowote.Mwacheni aongee apate ahueni wa fikra.Hiyo kashfa siyo ya kitoto
Gwajma anayo haki ya kujihami kwa 100% ndiyo maana wengi wanamuunga mkono, lakini pia amewasaidia watanzania kujua mengi juu ya wajibu wa mkuu wa mkoa pia vita juu ya vyeti feki ilivyokuwa ngumu hasa kwa wateuliwa wa mkulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…