VIONGOZI WA DINI AINA YA GWAJIMA NI WA KUPUUZWA KABISA
Nakumbuka katika moja ya hotuba zake baba wa taifa hayati JK Nyerere aliwahi kusema kuwa ni kosa kubwa sana kwa kiongozi wa dini kutumia jukwaa la kanisa kuwa jukwaa la kisiasa
Leo hii tunayaona mengi sana yaani askofu mzima wa kiroho katika jukwaa la kanisa lake analigeuza kuwa jukwaa la kisiasa na kuanza kukosoa wateule wa rais wazi wazi.Hili jambo halipaswi kuvumiliwa hata kidogo mamlaka zinazohusika ni wajibu wao sasa kuwachukulia hatua viongozi wa namna hii
Kama kweli mchungaji Gwajima anavyo vyeti vya makonda kwanini alikaa kimya adi juzi baada ya yeye kutajwa katika watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya?
Gwajima amepata wapi hivyo vyeti wakati Necta hawatoi vyeti kwa mtu asiye muhusika?
Necta wameanza lini kutoa vyeti vya mtu aliyepata division zero kidato cha nne?
Hivi Gwajima alikosa mahubiri ya kuwaombea wafuasi wake adi aanze kufanya siasa kanisani.?
Kuna maswali mengi sana tunapaswa kumuuliza mchungaji Gwajima kuwa kati ya kutumia cheti cha mtu na kuvunja ndoa ya mtu jambo lipi ni dhambi kubwa mbele ya Mungu?
Lazima tujue sasa kuwa lipi ni jambo baya mbele ya mwenyezi Mungu
Huyu mchungaji Gwajima alikuwa na kashfa kubwa sana ya kutembea na kuvunja ndoa ya mwimbaji wa nyimbo za injiri Frola Mbasha na Emanuel Mbasha.Leo hii ndoto za Emanuel Mbasha ya kuwa na ndoa na familia yenye amani imeshafutika na ilifutwa na Gwajima huyu huyu wa leo na hadithi zake za Daudi Bashite
Kweli huyu mtu anapaswa kuaminiwa mbele ya Jamii?.Hivi Mungu wa Gwajima ndio Mungu wetu sisi wengine au ana Mungu wake binafsi?
Hivi kweli Mungu anapenda kuona watoto wa watanzania masikini wanaangamia kwenye ulevi wa madawa ya kulevya? Hivi Mungu anapenda kuona wakina mama wajawazito wanapata tabu wakiwa hospitalini?.Mimi sina hakika kama kweli Mungu wa Gwajima ndio huyu Mungu tunayemuomba sisi mwenye rehema na mwenye kutaka kuona kila mtu anaishi maisha safi na salama
Hivi Gwajima anajua machozi aliyotoa mama yake Rehema chalamila aka Ray C.?
Hivi Gwajima anajua machozi aliyotoa mama yake chidi benzi?.
Hivi anajua machozi aliyotoa mama yake na Tid kuhusu mtoto wake kuwa teja wa madawa ya kulevya.?
Gwajima anajua ni vijana wangapi wa kitanzania wamekamatwa kwenye nchi za nje na wamefungwa maisha kutokana na biashara ya madawa ye kulevya.?
Gwajima anajua ni vijana wangapi wamekuwa mateja wa kudumu kabisa kwa sababu ya hii biashara ya madawa ya kulevya.?
Hivi Mungu anapenda kuona hawa vijana wanakuwa mateja kweli.? Hivi huyu Mungu wa Elia,Mussa na Yakobo ndio huyu huyu Mungu wa Gwajima..?Hapana hapana nadhani Gwajima ana Mungu wake anayemjua yeye na hao wanaomtuma haina ubishi kuwa Gwajima anatumiwa na watu wake lakini watashindwa kwa jina la Mungu wetu sisi sio huyo Mungu wao
Paul Makonda amefanikiwa kujenga wodi ya wazazi tena ya kisasa zaidi ambayo itasaidia wazazi na dada zetu kujifungua kwa usalama zaidi, hivi Gwajima na hao wanaomtuma wamesahau matatizo wanayopata mama zetu huko hospitali?.Hivi Mungu wao hapendi kuona akina mama wanapata huduma bora za afya? Kweli leo hii tumkose makonda kisa makaratasi tu? Wangapi wana vyeti vizuri sana na wengine maprofesa sana lakini wameitia hasara serikali yetu na nchi yetu lakini huyu Gwajima na genge lako hawayaoni hayo?
Gwajima unajua kuwa wabunge wengi wana elimu za kutosha lakini kwenye majimbo yao kuna hali mbaya sana? Gwajima umeshafika jimbo la monduli?
Gwajima umeshafika jimbo la singida mashariki?
Kweli tumkose makonda kisa kikundi cha watu wachache ambao wana maslahi yao binafsi?
Kama Gwajima aliweza kutoa maneno ya ajabu kabisa kwa baba askofu pengo ambaye ni askofu mwenzake na pengo akasema amemsamehee nadhani hii yote ni ile laana ya kumtukana baba askofu pengo
Gwajima waambie hao waliokutuma kuwa wameshindwa vita kabla hawajaanza na Mungu wa Elia naYakobo yupo upande
NDIMI
RAPHAEL LUKINDO