Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Heshima kwako mkuu. Nadhani inafahamu kuwa hii sio mara ya kwanza kwa baba askofu Gwajima kujihusisha na mambo ya kisiasa. Licha ya hilo Neno la Mungu linataka mtumishi wake anapotuhumiwa jambo afanye nini? Baada ya kuwa ametimiliza matakwa ya kisheria kwa kuripoti polisi ilimpasa kuendelea kumtumikia Mungu na kumtakia mh Makonda mafanikio katika mapambano yake. Biblia inasema ndiposa hasira ya Mungu itawaka juu ya mtu yule. Tazama His Eminence Pplycarp Cardinal Pengo alivyotenda baada ya kukashifiwa na Askofu Gwajima. Huo ndio mfano mwema wa mtumishi wa Mungu.

Naumia moyo sana naposikia sifa aliyojitwalia sasa baba askofu kwamba "anajua kuchamba. " Ukiona mtumishi wa Mungu amepata mashabiki mpaka kati ya wahalifu huku wakionyesha wazi kile wanachokitaka kwake si kubadili mioyo yao imwelekee Mungu, basi jua mtumishi ameacha njia yake. Ukweli ulipo sasa hivi askofu amegeuka lulu kwa wote wanaotaka kusikia "ubuyu" bila kujali mguso wa kiimani. Kanisa limegeuka nyumba ya mipasho.

Mungu anisamehe kwa kuwa nimeshika kusema hali mimi ni mwanadamu tu.
 
swali la msingi ni kwa nini gwajima amepaniki kuhusu dawa za kulevya???? ajakutwa na ushahidi but lisemwalo lipo

swali la msingi ni kwa nini Bashite amepaniki kuhusu swala la cheti feki???? ajaonyesha ushahidi but lisemwalo lipo
 
Evidence ya Gwajima ya kuuza dawa iko wapi na unamhusisha vipi na mateja Ray C, ChidBenzi etc. kama siyo kujichanganya. waonyeshe evidence kwanza ndiyo watu waongee.
Kusema Gwajima ana panic ni kweli hata ungekuwa wewe unahusishwa na jambo ambalo hujawahi fanya unge react vipi? mlitaka anayamazee ili mseme amekubali kosa au ?
 
Mleta mada hebu acha Unafki , alipokosewa heshima kutangazwa na Makonda kupitia vyombo vya habari mbona hukuwaka ?! Hiyo heshima yake anairudishaje ?!

Viongozi wengi wa dini hao unaowatukuza ni kwa sababu tu ni makada na mameiegemea serikali hata kwa mabaya

Makonda alitakiwa kujuwa athari za kutangaza watu bila ushahidi na bora kazi hiyo angeliiachia police na vyombo vingine vya dola. Siyo yeye kutumia majukwaa ya kisiasa kuchafua watu
 
Kama kuwashika amewashika pabaya...wanatetemeka mbaya
 
Hapa tulipofikia ni hatari kutengeneza "magumashi" itawagharimu watu kazi zao
 
Bwana Lukindo, umeandika "vingi" sana. Lakini ili ueleweke zaidi mwambie tunaomba vyeti vyake na majina ya shule alizosoma mpaka chuo.
Kwanini hao wanaomtuhumu wasitoe uthibitisho kama wanavyodai wanao, ili tuwe na uhalali wa kumhukumu makonda?
 
VIONGOZI WA DINI AINA YA GWAJIMA NI WA KUPUUZWA KABISA

Nakumbuka katika moja ya hotuba zake baba wa taifa hayati JK Nyerere aliwahi kusema kuwa ni kosa kubwa sana kwa kiongozi wa dini kutumia jukwaa la kanisa kuwa jukwaa la kisiasa

Leo hii tunayaona mengi sana yaani askofu mzima wa kiroho katika jukwaa la kanisa lake analigeuza kuwa jukwaa la kisiasa na kuanza kukosoa wateule wa rais wazi wazi.Hili jambo halipaswi kuvumiliwa hata kidogo mamlaka zinazohusika ni wajibu wao sasa kuwachukulia hatua viongozi wa namna hii

Kama kweli mchungaji Gwajima anavyo vyeti vya makonda kwanini alikaa kimya adi juzi baada ya yeye kutajwa katika watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya?
Gwajima amepata wapi hivyo vyeti wakati Necta hawatoi vyeti kwa mtu asiye muhusika?
Necta wameanza lini kutoa vyeti vya mtu aliyepata division zero kidato cha nne?
Hivi Gwajima alikosa mahubiri ya kuwaombea wafuasi wake adi aanze kufanya siasa kanisani.?

Kuna maswali mengi sana tunapaswa kumuuliza mchungaji Gwajima kuwa kati ya kutumia cheti cha mtu na kuvunja ndoa ya mtu jambo lipi ni dhambi kubwa mbele ya Mungu?
Lazima tujue sasa kuwa lipi ni jambo baya mbele ya mwenyezi Mungu
Huyu mchungaji Gwajima alikuwa na kashfa kubwa sana ya kutembea na kuvunja ndoa ya mwimbaji wa nyimbo za injiri Frola Mbasha na Emanuel Mbasha.Leo hii ndoto za Emanuel Mbasha ya kuwa na ndoa na familia yenye amani imeshafutika na ilifutwa na Gwajima huyu huyu wa leo na hadithi zake za Daudi Bashite

Kweli huyu mtu anapaswa kuaminiwa mbele ya Jamii?.Hivi Mungu wa Gwajima ndio Mungu wetu sisi wengine au ana Mungu wake binafsi?
Hivi kweli Mungu anapenda kuona watoto wa watanzania masikini wanaangamia kwenye ulevi wa madawa ya kulevya? Hivi Mungu anapenda kuona wakina mama wajawazito wanapata tabu wakiwa hospitalini?.Mimi sina hakika kama kweli Mungu wa Gwajima ndio huyu Mungu tunayemuomba sisi mwenye rehema na mwenye kutaka kuona kila mtu anaishi maisha safi na salama

Hivi Gwajima anajua machozi aliyotoa mama yake Rehema chalamila aka Ray C.?
Hivi Gwajima anajua machozi aliyotoa mama yake chidi benzi?.
Hivi anajua machozi aliyotoa mama yake na Tid kuhusu mtoto wake kuwa teja wa madawa ya kulevya.?

Gwajima anajua ni vijana wangapi wa kitanzania wamekamatwa kwenye nchi za nje na wamefungwa maisha kutokana na biashara ya madawa ye kulevya.?
Gwajima anajua ni vijana wangapi wamekuwa mateja wa kudumu kabisa kwa sababu ya hii biashara ya madawa ya kulevya.?

Hivi Mungu anapenda kuona hawa vijana wanakuwa mateja kweli.? Hivi huyu Mungu wa Elia,Mussa na Yakobo ndio huyu huyu Mungu wa Gwajima..?Hapana hapana nadhani Gwajima ana Mungu wake anayemjua yeye na hao wanaomtuma haina ubishi kuwa Gwajima anatumiwa na watu wake lakini watashindwa kwa jina la Mungu wetu sisi sio huyo Mungu wao

Paul Makonda amefanikiwa kujenga wodi ya wazazi tena ya kisasa zaidi ambayo itasaidia wazazi na dada zetu kujifungua kwa usalama zaidi, hivi Gwajima na hao wanaomtuma wamesahau matatizo wanayopata mama zetu huko hospitali?.Hivi Mungu wao hapendi kuona akina mama wanapata huduma bora za afya? Kweli leo hii tumkose makonda kisa makaratasi tu? Wangapi wana vyeti vizuri sana na wengine maprofesa sana lakini wameitia hasara serikali yetu na nchi yetu lakini huyu Gwajima na genge lako hawayaoni hayo?
Gwajima unajua kuwa wabunge wengi wana elimu za kutosha lakini kwenye majimbo yao kuna hali mbaya sana? Gwajima umeshafika jimbo la monduli?
Gwajima umeshafika jimbo la singida mashariki?

Kweli tumkose makonda kisa kikundi cha watu wachache ambao wana maslahi yao binafsi?
Kama Gwajima aliweza kutoa maneno ya ajabu kabisa kwa baba askofu pengo ambaye ni askofu mwenzake na pengo akasema amemsamehee nadhani hii yote ni ile laana ya kumtukana baba askofu pengo
Gwajima waambie hao waliokutuma kuwa wameshindwa vita kabla hawajaanza na Mungu wa Elia naYakobo yupo upande

NDIMI
RAPHAEL LUKINDO
 
Nipigie namba hizi, nikupe vyeti vya guajima

Bashite.Saba.tano.Tano.Mbili.Moja.Bashite.Bashite.Tisa.Bashite
_0755 210 090

Karibu
 
Huyu Baba maneno mengi sana lakini akiitwa mahakamani tu anapatwa na kifafa
 
Naona wachangiaji mada hii wote watoto wa mama mdogo
 
Kumbe alisema Nyerere!!!!

Ni kweli Mungu wa Gwajima sio mungu wako

Kumbuka akuanzae mmalize
 
swali la msingi ni kwa nini gwajima amepaniki kuhusu dawa za kulevya???? ajakutwa na ushahidi but lisemwalo lipo
.... Yaani unichafue Jina langu kwa kupenda kwako misifa halafu nikuache hivi hivi while I can?? Labda niwe sina uwezo au nafasi ya kufanya chochote kama wale mateja...
 
Mlikuwa wapi kuyasema haya mpaka treni imechanganya ndio mnataka kuruka? Hapa issue sio UCHUNGAJI wa Gwajima, hayo yanamhusu mwenyewe na wanaosali kwake...issue ipo
 

Attachments

  • kolomije.jpg
    93.3 KB · Views: 38
Pengo hakulala sero ndugu
 

Njaaa zako zitakuuuaa...bashite alete vyeti hicho tu... Akuanzae mmalize tulifundishwa hivyo..bashite alisema mwenzie anauza dawa...mwenzie kajibu bashite kanunua vyeti....bashite kasepa no vyeti no nn..
Big up askofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…