Nadhani sasa ni wakati muafaka kabisa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania afikirie kumpa ama usajili wa muda wa kudumu kabisa Askofu Josephat Gwajima ili tujue moja huu ' upuuzi ' wake tunaoanza kuuchoka sasa.
Najua humu JF kuna Watu wake wengi mnaomuamini na niliweke tu wazi kuwa hata Mimi kuna mahala fulani huwa nakubali michango yake hasa ile yenye uelekeo wa kuijenga Jamii yetu ambayo kimsingi hata yeye anaitegemea kwa ' Sadaka ' zao.
Katika huu ' uzi ' wangu nawaombeni tumwangalie Askofu Gwajima katika dhana nzima ya ' Society Development ' ili tuweze kujua kuwa tunapomkabili hivi Kihoja tunakosea au tupo sahihi na tukisema tukae kimya eti kwa Kigezo cha ni ' Kipenzi ' chetu au chako nadhani tutakuwa hatumsaidii.
Natambua matatizo makubwa yaliyopo sasa nchini Tanzania na pia naitambua kabisa Kazi yake kama Kiongozi wa Kiroho ambaye ana haki ya Kukemea na Kulisemea pale inapobidi ina nadhani sasa Askofu Gwajima ame exaggerate hii kitu na nimeanza sasa kuhisi kuwa pengine kuna ' kamchezo ' fulani ambako anakafanya kupitia Watu maarufu wengine ili kumpaisha na kusudi kila Jumapili Kanisani Kwake kufurike ili azidi kula Pesa za ' wasiojielewa ' wala ' kumshtukia '.
Hivi logically tu Askofu unaweza ukaanza kuhubiri kuanzia Saa 4 hadi Saa 8 na katika hayo mahubiri yako neno la Kimungua au la Kiroho tunalisikia kwa 5% tu lakini maneno ya Kimajungu, Majigambo na Vitisho tunayasikia kwa 95%.
Mimi sijasomea mambo ya ' Theology ' ila nina uhakika kabisa humu humu JF wapo ' wanazuoni ' wazuri wa hiyo Elimu ya Kidini hivyo wajitokeze kutusaidia kuwa je huu ' utoto ' wa Kiimani anaoufanya Askofu Gwajima kila Jumapili ndivyo walivyofundishwa huko Vyuoni Kwao?
Sasa kituko zaidi ni pale jana ambapo Askofu Gwajima kasema kuwa Msanii wa Miziki ya Bongo Fleva Nassib Abdul a.k.a Diamond au Dangote kuwa ni mmoja wa Wafuasi wa lile Kundi linalohisiwa kuwa ni la Kichawi la Freemason na kwamba ana uhakika wote juu ya hilo.
Nadhani Watanzania ama tumejisahau au tumejisahaulisha tu kwa makusudi kuwa huko nyuma kwa miaka kadhaa huyu huyu Askofu Gwajima amekuwa akihusishwa na hilo hilo Kundi la Freemason sasa labda pengine ili tumuamini atuambie je yeye ndiyo alimkaribisha Diamond huko au alipishana nae labda yeye alipoondoka humo?
Sipo hapa wala humu JF kumtetea sijui Diamond au kumachafua Askofu Gwajima ILA vita ambayo siku zote GENTAMYCINE huwa napigana nayo ni ya kutopenda ' Unafiki ' na kuwa ' Mwoga ' kusema ukweli wako na laiti Watanzania wote tungeuchukia huu ugonjwa wa unafiki nina hakika leo nchi yetu ingekuwa mbali mno Kimaendeleo.
Askofu Gwajima nitoe tu RAI Kwako kuwa Wewe ni mmoja kati ya Viongozi wa Dini wenye kuheshimika na jamii kubwa ya Tanzania ( japo nahisi ni ya sisi tu wana Dar es Salaam ) hivyo jaribu sana kutenganisha kati ya Utumishi wa Kiroho na Harakati za Kisiasa kwani nisikufiche siku hizi ' Bifu ' zako zikija kupatiwa ' Ufumbuzi ' wa muda mrefu nadhani hapo Kanisani Kwako utabaki Wewe, Mkeo na hao Walinzi wako na wenye akili wote ' watakukimbia '.
Askofu Gwajima mbona hizi ' harakati ' zako hatuzioni kwa wenzako kama akina Mwingira, Lusekelo, Mwakasege, Kakobe na wengineo ambao nina uhakika kuwa wao wameanza hili ' game ' kabla yako? Kwanini Wewe? Je huyo Mungu wako Wewe kakutuma uwe unaitumia tu Jumapili kwa ' kuwananga ' Watu?
Nimalizie tu kwa kukukumbusha Mkuu japo Wewe unaonekana kuwa ' kimbelembele ' Waganda wanasema ' Lugezigezi ' kwa kutoa ' SIRI ' za ndani kabisa za Wenzako ILA je Askofu Gwajima na Wewe unalikumbuka lile tukio lako la miaka minne ( 4 ) iliyopita ambalo ulilifanya katika Nyumba ya Mtu pande za Mbezi Beach maeneo ya kwa Marehemu Mzee Sykes ambapo ' lilikugharimu ' hadi ikakubidi uruke ' ukuta ' wa ile nyumba baada ya kushtushwa na waliokuonea huruma kisha baada ya hapo ukatumia gharama nyingi mno kulimaliza kupitia kwa ' Msukuma ' mwenzio Erick Shigongo na ' Magazeti ' yake?
Kwa leo naomba niishie tu hapa ila ukiona hayo niliyoyaandika hapa yana tija yachukue na ukiona hayana niachie tu mwenyewe tafadhali ila naamini wenye akili za kutukuka na wanaojitambua watakuwa wamenielewa. Tanzania ya sasa hatuhitaji majungu, fitina, bifu na chuki bali tunahitaji msaada wa kutoka hapa tulipo Kimaendeleo ili tuweze kukimbizana na waliotupita siki nyingi.
Nawasilisha na niwatakieni tu mwanzo mwema wa wiki hii na Pasaka njema nyote.