Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Haiwezekani amuite Mkuu wa Mkoa kiumbe...ni kosa kubwa sana
Hapa huwa hakuna middle ground, Kama wewe si muumba basi ni kiumbe. Sasa naomba nikuulize, mkuu wa mkoa ambaye unasema kumuita kiumbe ni kosa sasa yeye ni nani?! Ni muumba?! Ukishajua anafiti wapi basi ndio utajua kuwa ulikomenti kwa kuongozwa na mihemko.
 
Kwe

Kweli ndugu hata mfalme Daudi alimchukiza Mungu kwa kumchukua mke wa Jemedari wake
Ni kweli Mfalme Daudi alitenda dhambi nyingi na nyingine kubwa. kwanza alisema uongo kumdangaya jemedari wake Uria kumshawishi kwenda vitani, (amri ya 7: "usiseme uongo). Pia kwa kumtamani mke wa mtu mwingine (amri ya 9, usitamani mke wa mtu mwingine").

Kisha akumuua jemedari wake Uria ili amtwae mke wake(amri 5."Usiue").
Kisha kumtwaa mke wa uria, Berth-Sheba na kuzini nae kwa kumbaka (amri ya 6:"usizini").

Licha ya dhambi hizi zote, sometimes Mungu huwaacha watumishi wake watende dhambi kwa lengo la kuwaacha ili kuuonyesha utukufu wake ujidhihiri, hivyo hizo dhambi za Mfalme Daudi, ziliachwa na uzao wa Daudi na Berth-Sheba ni Mfalme Suleiman.

Hivyo katika bandiko hili zijazungumzia dhambi za kiuzinifu za watu wa Mungu.

Paskali.
 
Unaweza vipi kutenganisha dini na siasa? Wewe siyo mzima kichwani.

Papa ni Rais wa Vatican unawezaje kumzuia kufanya siasa? Iran huwezi kuwa Rais mpaka upate Approval ya Ayatollah cleric leader, jinga kabisa wewe.
 
Tutahudhuria bila kukosa, ila kinachofanywa hapa ni kazi ya Mungu?.
P.
 
Hawa wanapaswa kuwa watumishi wa Mungu na kufanya kazi ya Mungu kuhubiri Injili, sasa hiki anachokwenda kufanya mtumishi huyu ndio kazi ya Mungu?!.

Usiniambie kuwa, kuna watu na akili zao timamu, siku hiyo, watatoka majumbani mwao, kwenda kulishwa neno la Bwana kumhusu Bashite!.

Wakijitokeza kwa wingi, nitashangaa!.

P.
 
Nabii Issa, ndio nani huyu!!?

Sent from my TECNO-J8 using Tapatalk
Nabii Issa ni Nabii wa Mungu, jina lake halisi ni Issa Bin Mariyam kwa Kiislsmu kwa Kikisto ni Yesu Kristo.

Mungu ni mmoja, na sheria ya Mungu ni moja tuu, ile ile sheria ya Musa. Kitabu cha sheria ndani ya Quran ni Tourat, ndani.ya Biblia ni Kumbukumbu la Torati.

Adam na Eva ndio Adam na Hawa.

Nabii Ibrahim ndio Abrahamu.

Watoto wake, Ishamel na Isaka ndio Ismaili na Isihaka. Yakobo ndio Yakub, Mtoto wa Yakobo Joseph ndio Yusufu alioeapeleke wana wa Israel, utumwani Misri, na Moses ndie Musa!.

Wakristu na Waislamu ni watoto wa baba mmoja na Mungu mmoja ila majina tofauti!.

P.
 
Mkuu watu wengi kwenye dini wanaingiza ushabiki. Maelezo yako wengi hawatakuelewa kwasababu moja tu ya Ushabiki! Walichosahau ni kuwa dini si kitu cha ushabiki kama mpira. Hakuna mshindi wala mshindwa hapa duniani kwenye suala la dini. Mshindi na mshindwa ni baada ya kifo siku ya kiama kwa wanaoamini kwamba kipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nabii Issa wa kwenye quran na yesu kristo wa kwenye biblia ni watu wawili tofauti kabisa soma historia zao vizuri kwenye hivyo vitabu(kuanzia kuzaliwa kwao hadi kuondoka kwao hapa duniani).Ingawa kwa vitu vichache wanafanana kama uponyaji wa vipofu na viziwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,

Umekurupuka kijana, hii inatokana na chuki uliyonayo dhidi ya mtu fulani! Unapotumia maandiko matakatifu /Bible unatakiwa kuambatanisha vifungu ambayo itaonyesho maandiko hayo umeyapata wapi!! Sasa kwa wewe maandiko yako yote yahusuyo bible si ya kweli!
 
Ni haki yako kushangaa...you're what you know.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…