Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Isikilize vizuri hio video,binadamu ni kiumbe kianziacho tumboni,zaid ya raisi maana yake uraisi una ukomo na kazi ya Mungu ni ya kudumu,pia km ni uongo aende mahakamani akamstaki,au akanushe Kwa uthibitisho,kuhusu kumiliki mali hata wwe ukiacha uvivu wa kufikiri ukawa positive thinkers unaweza ukamzid Trump.Gwajima ni great positive thinker anaamini ktk kuweza ni kanuni ya matajiri wengi wa mali za kutafuta sio za kurithi.Siasa ni maisha na ni makosa kumtuhumu mtu Kwa kitu usicho na ushahidi nacho.Na maisha ya kinafiki kuishi kwa kujipendekeza, kuwachongea au kuwaonea wengine huwa yana mwisho mbaya tunayaona mitaani pia.
 
Wazee wa CCM hao ............ Tangu lini ulishaona Mzee wa Kitanzania akija hadharani na kusema maneno na akayasimamia mpaka mwisho!!?

Tena Mzee wa CCM .......................!! Kama akina Mwinyi, Mkapa wanashindwa kusema hadharani bila kuuma wala kumungunya unategemea nani atakayeweza huko CCM!!
Basi hawajui majukumu yao hapa duniani.
 
Maaskofu na wazee ndiyo kazi waliyotumwa na Mungu hapa duniani.
Mkuu wazee wengi sasa wamegawanyika wengi wapo kwa upande wa Gwajma na baadhi kwa makonda kinachotakiwa kwa sasa ni Mh Rais atumbue Jipu watu waachane na story hii maisha yaendelee kama kawaida.
 
Wanabodi,

Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?, Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji Gwajima Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!. Akiwa katika mimbari, madhabahuni, badala ya kuhubiri neno la Mungu lenye kujenga upendo, yeye anahubiri siasa za chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "kiumbe".

Isikilize Clip hii Akisema Uongo Madhabauni, tena mchana kweupe. Mara baada ya Mashekh wa Mkoa wa Dar es Salaam, kumuombea dua, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Gwajima, amemuonea vivu kuwa dua zile zitazidi kumnyooshea mambo yake, hivyo ili kumbomoa, Mchungaji Gwajima, mwenye utajiri wa ajabu (Hammer, Helcopter, na kanisa kubwa), akaamua kuhubiri mahubiri ya kusingizia, kwa kumsingizia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kuwa ni mhalifu wa kosa la jina la kuiba jina la mtu mwingine, na kosa la kughushi kwa vyeti, kwa kudai kuwa eti jina halisi la Paul Makonda, sii jina lake, ni jina la mtu mwingine, Makonda jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite!, na hakuishia hapo, amedai Yeye nini Zaidi ya Rais, kugombea urais ni demotion!. Hivi kwa mtumishi wa Mungu wa kweli, anaweza kusema maneno kama haya madhabahuni kwa Mungu, au Mchungaji huyu, ni wale Manabii wa Uongo, Bwana wetu Yesu Kristu aliotuhusia?.

Msikiliza Mchungaji Gwajima.

Nimeisikiliza hii clip hii ya Mchungaji Gwajima, akimzungumzia Daudi Albert Bashite, A.K.A Paul Christian Makonda, akidai kuwa kilichomponza yeye Mchungaji Gwajima hadi kusingiziwa madawa ya kulevya, ni dhana kuwa anataka kugombea ubunge jimbo la Misungwi, kufuatia kutua kijiji Kolomije kwa Chopa, (Helcopter), hivyo Daudi Bashite, A.K.A Paul Manajipanga kugombea jimbo hilo mwaka 2020!. Mchungaji Gwajima akajitapa Ubunge, Uwaziri hadi Urais kwa Mtumishi wa Mungu aliye hai ni demotion!. "Mtumishi wa Mungu ni zaidi ya Rais wa nchi!". Jee hii ni kweli?.

Akielezea kuhusu Daudi Albert Bashite, na yeye Mchungaji Gwajima, ni watu wa kabila moja na wametokea kijiji kimoja cha Kolomije. Daudi Bashite alisoma Shule Msingi ya Kolomije hadi darasa la tano, akahamia Shule ya Msingi ya Nyanza hadi akamaliza Darasa la 7, hakuchaguliwa. Akajiunga na Shule ya Sekondari Pamba, akiwa anakaa kwa mama Kamese (Gwajima ana simu yake) ambako alipata Divisheni 0, ndipo dada mmoja wa Kihaya kwa jina la Christina (Gwajima ana simu yake) akamuunganishia Daudi Albert Bashite, kwa mdogo wake, Paul Christian, hivyo Daudi Bashite akaanza kutumia cheti cha kaka yake Paul Christian ndipo akajiunga Nyegezi kusomea certificate ya uvuvi kwa jina la Paul Christian Makonda, kisha akajiunga Chuo cha Mbegani Bagamoyo kuchukua diploma ya uvuvi na kumalizia Chuo cha Ushirika kuchukua degree kwa majina ya kughushi ya Paul Christian.

Katika kumuelezea Daudi Bashite, Mchungaji Gwajima amemuita "kiumbe huyu", hili sio neno zuri kwa kiongozi wa dini ya Mungu kweli, kumuita binadamu mwenzako kiumbe!.

Ila pia Mchungaji Gwajima amedai, anavyo vyeti vyote ofisini kwake tangu cha Daudi Albert Bashite alichopata Divisheni 0. hadi cheti cha Paul Christian alichounganishiwa na Christina!, na kudai kuwa ana mshitaki Makonda kwa Ndalichako na kwa Magufuli, na asipochukuliwa hatua zozote, yeye atashangaa sana na atavitoa vyeti hivyo hadharani, umma uvione.

Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Huyu ni mchungaji wa Mungu au mungu. Hili la kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, Jee hii inaweza kuwa kweli?!. Nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kimetoka wapi?. Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo madhabahuni, jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu, au ndio hawa wachungaji wanaomtumikia mungu?!.

Jumatatu Njema.
Paskali

Paskali nilichoelewa mimi, sio kwamba yeye yuko juu ya Rais ila utumishi wa Mungu ni zaidi ya hivyo vyeo vingine.

Nilitaka kukutag kwenye ule uzi mwingine, nilijua itakuuma tu. Pole sana mkuu. Wewe mwambie Makonda ajibu tuhuma kwa vielelezo sio kwa kuombewa na mashehe.

Huyo Gwajima, atajijua yeye mwenyewe na Imani yake. Hivyo ni vitu vya kiroho, haya ya Makonda ni ya hapa na adhabu zake ziko hapa hapa duniani.
 
T
Aisee kumbe wengine mmesoma kw kukariri,kwani akiwa na result slip si ni cheti pia?
Nyinyi mnawajua watumishi wote wanaosali kwa gwajima je kama wamempelekea ushahidi huo wa kuprint hata kama ni document sio cheti?pascally wewe nina wasi wasi utakuwa ni mhanga kama daudi bashite.

Result slip siyo cheti. Tafuta result slip yoyote imeandikwa kuwa siyo cheti, hii ni kwa matokeo yanayotolewa na necta.
 
Wanabodi,

Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?, Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji Gwajima Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!. Akiwa katika mimbari, madhabahuni, badala ya kuhubiri neno la Mungu lenye kujenga upendo, yeye anahubiri siasa za chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "kiumbe".

Isikilize Clip hii Akisema Uongo Madhabauni, tena mchana kweupe. Mara baada ya Mashekh wa Mkoa wa Dar es Salaam, kumuombea dua, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Gwajima, amemuonea vivu kuwa dua zile zitazidi kumnyooshea mambo yake, hivyo ili kumbomoa, Mchungaji Gwajima, mwenye utajiri wa ajabu (Hammer, Helcopter, na kanisa kubwa), akaamua kuhubiri mahubiri ya kusingizia, kwa kumsingizia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kuwa ni mhalifu wa kosa la jina la kuiba jina la mtu mwingine, na kosa la kughushi kwa vyeti, kwa kudai kuwa eti jina halisi la Paul Makonda, sii jina lake, ni jina la mtu mwingine, Makonda jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite!, na hakuishia hapo, amedai Yeye nini Zaidi ya Rais, kugombea urais ni demotion!. Hivi kwa mtumishi wa Mungu wa kweli, anaweza kusema maneno kama haya madhabahuni kwa Mungu, au Mchungaji huyu, ni wale Manabii wa Uongo, Bwana wetu Yesu Kristu aliotuhusia?.

Msikiliza Mchungaji Gwajima.

Nimeisikiliza hii clip hii ya Mchungaji Gwajima, akimzungumzia Daudi Albert Bashite, A.K.A Paul Christian Makonda, akidai kuwa kilichomponza yeye Mchungaji Gwajima hadi kusingiziwa madawa ya kulevya, ni dhana kuwa anataka kugombea ubunge jimbo la Misungwi, kufuatia kutua kijiji Kolomije kwa Chopa, (Helcopter), hivyo Daudi Bashite, A.K.A Paul Manajipanga kugombea jimbo hilo mwaka 2020!. Mchungaji Gwajima akajitapa Ubunge, Uwaziri hadi Urais kwa Mtumishi wa Mungu aliye hai ni demotion!. "Mtumishi wa Mungu ni zaidi ya Rais wa nchi!". Jee hii ni kweli?.

Akielezea kuhusu Daudi Albert Bashite, na yeye Mchungaji Gwajima, ni watu wa kabila moja na wametokea kijiji kimoja cha Kolomije. Daudi Bashite alisoma Shule Msingi ya Kolomije hadi darasa la tano, akahamia Shule ya Msingi ya Nyanza hadi akamaliza Darasa la 7, hakuchaguliwa. Akajiunga na Shule ya Sekondari Pamba, akiwa anakaa kwa mama Kamese (Gwajima ana simu yake) ambako alipata Divisheni 0, ndipo dada mmoja wa Kihaya kwa jina la Christina (Gwajima ana simu yake) akamuunganishia Daudi Albert Bashite, kwa mdogo wake, Paul Christian, hivyo Daudi Bashite akaanza kutumia cheti cha kaka yake Paul Christian ndipo akajiunga Nyegezi kusomea certificate ya uvuvi kwa jina la Paul Christian Makonda, kisha akajiunga Chuo cha Mbegani Bagamoyo kuchukua diploma ya uvuvi na kumalizia Chuo cha Ushirika kuchukua degree kwa majina ya kughushi ya Paul Christian.

Katika kumuelezea Daudi Bashite, Mchungaji Gwajima amemuita "kiumbe huyu", hili sio neno zuri kwa kiongozi wa dini ya Mungu kweli, kumuita binadamu mwenzako kiumbe!.

Ila pia Mchungaji Gwajima amedai, anavyo vyeti vyote ofisini kwake tangu cha Daudi Albert Bashite alichopata Divisheni 0. hadi cheti cha Paul Christian alichounganishiwa na Christina!, na kudai kuwa ana mshitaki Makonda kwa Ndalichako na kwa Magufuli, na asipochukuliwa hatua zozote, yeye atashangaa sana na atavitoa vyeti hivyo hadharani, umma uvione.

Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Huyu ni mchungaji wa Mungu au mungu. Hili la kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, Jee hii inaweza kuwa kweli?!. Nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kimetoka wapi?. Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo madhabahuni, jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu, au ndio hawa wachungaji wanaomtumikia mungu?!.

Jumatatu Njema.
Paskali

Paskali. uongo aliousema ni upi?? na wewe unajifanya mtu wa ajabuajabu leo au umehongwa?
 
Tulieni tu dawa iwaingie vizuri jamani, hivi hamshangai kwanini mtuhumiwa kawa mpole hivi?
Mtuhumiwa yupo busy kwa sangoma, kamati za Ufundi toka Nchi mbalimbali na sasa mashehe wa Bakwata wanashinda nae, huku GSM wakitumia pesa kuingila data za baraza za mitihani ili wabariki majina ya Paul makonda yafanane tokea shule ya msingi mpaka alipomaliza, vuteni subra kuna vioja vya mwaka vinaandaliwa mwaka huu tutashuhudia maajabu ya kila aina.
 
Haiwezekani amuite Mkuu wa Mkoa kiumbe...ni kosa kubwa sana
Kosa kwa nani ?
.Ilo jamaa kilaza....Gwajima kampa Siku tatu ....anavitoa vyeti hadharani.... Mmesahau TB Joshua alivyokuja walivyoenda kumpokea airport mpaka ikulu mkwere anajichekesha
 
Kwani humu kuna maraika hadi tujue kuwa Gwajima ni mtumishi wa Mungu au sio?
Kwani mtoa mada wewe unamuonaje Gwajima?
 
Nakuja tena
Hata mimi zamani lilikuwa jambo la kawaida kutumia jina la mtu mwingine
Nawe umerudia yaleyale ya Gwajima, umehukumu. Tafiti, yawezekana Gwajima yupo sahihi. Dunia hii ina jambo moja la ajabu ambalo wengi wetu tunapopanda kimadaraka au kupata fedha tunasahau kwamba kama tunavyowajua wengine ndivyo na wao wanavyotujua. Tulizaliwa na kulelewa huko vijijini na watu wanatujua. Yawezekana madai ya Gwajima yasiwe na mashiko kwa sasa, lakini Paschal, elimu yetu Tanzania hasa hasa kati ya miaka ya 70 na 90 ilijaa magumashi tu, na hili la kutumia majina ya wanafunzi wengine lilikuwa jambo la kawaida. Leo hii ukizungumzia mwenye jina lake halisi kwa waliosoma kipindi hicho utachekwa sana kwa sababu kuchukua majina ya wanafunzi wengine lilikuwa jambo la kawaida, kwa hivyo sishangai kuyasikia haya maana ndo ulikuwa mtindo wakati huo--kukariri madarasa kwa majina ya wanafunzi watoro, wagonjwa nk. Kwa hiyo hili la Makonda kama ni kweli mimi sishangai, na watu wa aina hii wapo wengi tu, iwe serikalini au sekta binafsi. La Makonda linakuzwa tu kwa vile kagusa madawa ya kulevya!!
 
Mkuu wazee wengi sasa wamegawanyika wengi wapo kwa upande wa Gwajma na baadhi kwa makonda kinachotakiwa kwa sasa ni Mh Rais atumbue Jipu watu waachane na story hii maisha yaendelee kama kawaida.
Kazi ya Ukuu wa Mkoa siyo ya kutuma application hata kama hujui kusoma wala kuandika unaweza kupewa hiyo nafasi, kazi hii inataka hekima, busara na maarifa, wazee wanaweza kutumia busara na kumaliza hili bifu kwa amani.
 
Back
Top Bottom