Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Unaumia sana Gwajima kuwa mhubiri? Umemuelewa anamaanisha nini anaposema yupo juu ya Rais?
Hakuna kiongozi wa dini anayejifahamu, anaweza kusema yeye ni zaidi ya Rais. Iko siku atawaambieni yeye ndiye aliyewaumba.

Yaonekana anamfahamu Makonda tangu zamani. Kwa nini kwa utumishi wake wa Mungu, alikaa kimya kwa miaka yote hiyo akiwa mkuu wa Wilaya na sasa akawa mkuu wa Mkoa? Binafsi sijali kwamba amefoji vyeti, hilo ni kosa lake lakini haizuii na yeye kuhisiwa madawa ya kulevya.
Tuliwahi sikia hata polisi waliofoji vyeti, utawazuia kukukamata eti tu wamefoji vyeti? Nonsense!
 
Hii vita ya makonda vs Gwajma imetoa fundisho kubwa kwa watanzania, pia vita hii imetengeneza ajira na Dili kwa Wajanja wachache wanaojua kucheza na Akili za hao wakurupukaji, walimtuma makonda akurupuke na yy akakurupuka pasipo kutafakari sasa hao hao na wengineo wanakula pesa zake kwa kisingizio cha kumsaidia kupoza pressure ya akina Manji, mbowe, wema, Gwajma na wengineo, na yy Makonda sasa anapata pesa nyingi toka Hazina kwa amri ya mkulu akidai ni pesa ya kumsaidia kupambana na vita iliyopo mbele yake, sasa kuna biashara mpya imeibuka Wajanja wanapiga pesa kinyama huku watanzania wakiendelea kujadiliana tu, hii ndiyo Tanzania Nchi ya fursa na vioja vingi.
 
a33b3b7ca75cd8516b228acb0569f9fe.jpg

I guess ana matokeo kama haya
It seems being that broo
 
Pascal nadhani keshapewa cha juu, kama mnakumbuka ndo aliyeleta awali hizi tuhuma akizitoa kwenye page ya Mange Kinambi leo anasema ni uzushi, kwa mantiki hiyo Pascal ndo mzushi namba moja
 
Safari hii mliopewa hela mmsafishe Makonda mtaumbuka sana.
Gwajima huwa anapiga panapouma siku zote na aliyepigwa huwa haachi kuweweseka
Mako anawachora tu...muongee mmalize ...alafu anakuja kuwachapa na vyeti vyake....let the fools talk first...let wait and see who will lough last
 
Hajasema ana matokeo, amesema ana vyeti mezani kwake, hivi kweli kuna cheti cha divisheni 0 ya miaka hiyo?.

Paskali
Ndio,Zaman walikuwa wanatoa na Results Slip Pia
Pasco inachukua dakika ngapi kwa Daudi kuja na Vyeti vyake kum prove wrong Gwajima
 
Hakuna kiongozi wa dini anayejifahamu, anaweza kusema yeye ni zaidi ya Rais. Iko siku atawaambieni yeye ndiye aliyewaumba.

Yaonekana anamfahamu Makonda tangu zamani. Kwa nini kwa utumishi wake wa Mungu, alikaa kimya kwa miaka yote hiyo akiwa mkuu wa Wilaya na sasa akawa mkuu wa Mkoa? Binafsi sijali kwamba amefoji vyeti, hilo ni kosa lake lakini haizuii na yeye kuhisiwa madawa ya kulevya.
Tuliwahi sikia hata polisi waliofoji vyeti, utawazuia kukukamata eti tu wamefoji vyeti? Nonsense!
ww unamiliki cheti feki ndiyo maana unatetea vyeti feki, Tambua kuwa Gwajma kaamua kumchunguza makonda baada ya jaribio la kutaka kumbambikia kesi, na kila mtu huamua kumchunguza mtu pindi akiamua kukufanyia ubaya, Kabla makonda hajamfanyia Unyama Gwajma hakuwa akijua history yake, anapaswa umwambie boss wako Daud Albert kuwa hakuna aliyekuwa akijua kuwa ni muumni wa vyeti feki mpaka alipoamua kuwakomoa watu ndipo siri zote zimeanza kuvuja baada ya watu kutumwa kumchunguza.
 
Mako anawachora tu...muongee mmalize ...alafu anakuja kuwachapa na vyeti vyake....let the fools talk first...let wait and see who will lough last
Mkuu hongera sana naona umekula Tenda ya bilion kuingia Necta kufuta data zote na kuingiza Upya ( kufa kufaana) tumieni fursa hiyo kula pesa za GSM .
 
Hakuna kiongozi wa dini anayejifahamu, anaweza kusema yeye ni zaidi ya Rais. Iko siku atawaambieni yeye ndiye aliyewaumba.

Yaonekana anamfahamu Makonda tangu zamani. Kwa nini kwa utumishi wake wa Mungu, alikaa kimya kwa miaka yote hiyo akiwa mkuu wa Wilaya na sasa akawa mkuu wa Mkoa? Binafsi sijali kwamba amefoji vyeti, hilo ni kosa lake lakini haizuii na yeye kuhisiwa madawa ya kulevya.
Tuliwahi sikia hata polisi waliofoji vyeti, utawazuia kukukamata eti tu wamefoji vyeti? Nonsense!
Hoja zako ni za kitoto sana sawa na kumwambia Makonda alikuwa wapi kusema siku zote kuwa Gwajima anatumia madawa mana alikuwa kiongozi wa UVCCM akawa DC alikuwa na uwezo wa kulisaidia jeshi la polisi na si kulopoka ovyo sasa mtu wamemkamata wamempima hamna kitu wameamua wamuachie mana kama angekuwa navyo angebaki kizuizini au angepandishwa mahakamani.
 
Wanabodi,

Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?, Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji Gwajima Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!. Akiwa katika mimbari, madhabahuni, badala ya kuhubiri neno la Mungu lenye kujenga upendo, yeye anahubiri siasa za chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "kiumbe".

Isikilize Clip hii Akisema Uongo Madhabauni, tena mchana kweupe. Mara baada ya Mashekh wa Mkoa wa Dar es Salaam, kumuombea dua, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Gwajima, amemuonea vivu kuwa dua zile zitazidi kumnyooshea mambo yake, hivyo ili kumbomoa, Mchungaji Gwajima, mwenye utajiri wa ajabu (Hammer, Helcopter, na kanisa kubwa), akaamua kuhubiri mahubiri ya kusingizia, kwa kumsingizia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kuwa ni mhalifu wa kosa la jina la kuiba jina la mtu mwingine, na kosa la kughushi kwa vyeti, kwa kudai kuwa eti jina halisi la Paul Makonda, sii jina lake, ni jina la mtu mwingine, Makonda jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite!, na hakuishia hapo, amedai Yeye nini Zaidi ya Rais, kugombea urais ni demotion!. Hivi kwa mtumishi wa Mungu wa kweli, anaweza kusema maneno kama haya madhabahuni kwa Mungu, au Mchungaji huyu, ni wale Manabii wa Uongo, Bwana wetu Yesu Kristu aliotuhusia?.

Msikiliza Mchungaji Gwajima.


Nimeisikiliza hii clip hii ya Mchungaji Gwajima, akimzungumzia Daudi Albert Bashite, A.K.A Paul Christian Makonda, akidai kuwa kilichomponza yeye Mchungaji Gwajima hadi kusingiziwa madawa ya kulevya, ni dhana kuwa anataka kugombea ubunge jimbo la Misungwi, kufuatia kutua kijiji Kolomije kwa Chopa, (Helcopter), hivyo Daudi Bashite, A.K.A Paul Manajipanga kugombea jimbo hilo mwaka 2020!. Mchungaji Gwajima akajitapa Ubunge, Uwaziri hadi Urais kwa Mtumishi wa Mungu aliye hai ni demotion!. "Mtumishi wa Mungu ni zaidi ya Rais wa nchi!". Jee hii ni kweli?.

Akielezea kuhusu Daudi Albert Bashite, na yeye Mchungaji Gwajima, ni watu wa kabila moja na wametokea kijiji kimoja cha Kolomije. Daudi Bashite alisoma Shule Msingi ya Kolomije hadi darasa la tano, akahamia Shule ya Msingi ya Nyanza hadi akamaliza Darasa la 7, hakuchaguliwa. Akajiunga na Shule ya Sekondari Pamba, akiwa anakaa kwa mama Kamese (Gwajima ana simu yake) ambako alipata Divisheni 0, ndipo dada mmoja wa Kihaya kwa jina la Christina (Gwajima ana simu yake) akamuunganishia Daudi Albert Bashite, kwa mdogo wake, Paul Christian, hivyo Daudi Bashite akaanza kutumia cheti cha kaka yake Paul Christian ndipo akajiunga Nyegezi kusomea certificate ya uvuvi kwa jina la Paul Christian Makonda, kisha akajiunga Chuo cha Mbegani Bagamoyo kuchukua diploma ya uvuvi na kumalizia Chuo cha Ushirika kuchukua degree kwa majina ya kughushi ya Paul Christian.

Katika kumuelezea Daudi Bashite, Mchungaji Gwajima amemuita "kiumbe huyu", hili sio neno zuri kwa kiongozi wa dini ya Mungu kweli, kumuita binadamu mwenzako kiumbe!.

Ila pia Mchungaji Gwajima amedai, anavyo vyeti vyote ofisini kwake tangu cha Daudi Albert Bashite alichopata Divisheni 0. hadi cheti cha Paul Christian alichounganishiwa na Christina!, na kudai kuwa ana mshitaki Makonda kwa Ndalichako na kwa Magufuli, na asipochukuliwa hatua zozote, yeye atashangaa sana na atavitoa vyeti hivyo hadharani, umma uvione.

Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Huyu ni mchungaji wa Mungu au mungu. Hili la kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, Jee hii inaweza kuwa kweli?!. Nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kimetoka wapi?. Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo madhabahuni, jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu, au ndio hawa wachungaji wanaomtumikia mungu?!.

Jumatatu Njema.
Paskali

Hapa ana jaribu kukwambia kuhusu usafi wa kiumbe
 
YANI UMAJITAHIDI KABISA SIJUI KWA KUSUDI GANI KUTETEA VITU USIVYOKUWA NA USHAHIDI NAVYO. KAMA GWAJIMA ANASEMA UONGO WAKAMSHTAKI. HAYO YA UNABII WA UONGO MI HAYANIHUSU MAANA SIJAAMBIWA NIMEAMBIWA NISIHUKUMU.
Ndugu yangu uandishi ya Paskal unahitaji utulivu wa akili ndipo umweelewe,wewe unaweza ukafikiri kwanda anamponda Gwajima lakini kumbe sio hivyo.
 
Ndio,Zaman walikuwa wanatoa na Results Slip Pia
Pasco inachukua dakika ngapi kwa Daudi kuja na Vyeti vyake kum prove wrong Gwajima
Zitakuwa dakika milion 500 maana kuwasaka watu wote wanunuliwe kupoteza ushahidi itachukua madakika mengi sana.
 
Nawe umerudia yaleyale ya Gwajima, umehukumu. Tafiti, yawezekana Gwajima yupo sahihi. Dunia hii ina jambo moja la ajabu ambalo wengi wetu tunapopanda kimadaraka au kupata fedha tunasahau kwamba kama tunavyowajua wengine ndivyo na wao wanavyotujua. Tulizaliwa na kulelewa huko vijijini na watu wanatujua. Yawezekana madai ya Gwajima yasiwe na mashiko kwa sasa, lakini Paschal, elimu yetu Tanzania hasa hasa kati ya miaka ya 70 na 90 ilijaa magumashi tu, na hili la kutumia majina ya wanafunzi wengine lilikuwa jambo la kawaida. Leo hii ukizungumzia mwenye jina lake halisi kwa waliosoma kipindi hicho utachekwa sana kwa sababu kuchukua majina ya wanafunzi wengine lilikuwa jambo la kawaida, kwa hivyo sishangai kuyasikia haya maana ndo ulikuwa mtindo wakati huo--kukariri madarasa kwa majina ya wanafunzi watoro, wagonjwa nk. Kwa hiyo hili la Makonda kama ni kweli mimi sishangai, na watu wa aina hii wapo wengi tu, iwe serikalini au sekta binafsi. La Makonda linakuzwa tu kwa vile kagusa madawa ya kulevya!!
We nahisi ukulisikia tangazo kutoka kwa mama Joyce ndalichako
 
Mako anawachora tu...muongee mmalize ...alafu anakuja kuwachapa na vyeti vyake....let the fools talk first...let wait and see who will lough last
We unafiki hakuna ambae hawezi kucheza michezo ambayo Makonda anacheza cheti kukibadilisha ni pesa yako na ushawishi tu lakini ukweli pekee ndo huwezi kuubadilisha mana kama tumesoma na wewe na tunajua uliitaga halafu leo uonyeshe cheti umefaulu haitakujenga bali itakudidimiza tu.
Mpaka sasa Paul halisi kashatolewa kituo cha kazi yupo jijini wanaandaa cheti original wanachokijua wao lakini ni too late
 
Back
Top Bottom