Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Ni kweli kwani gwajima anawajibika kwa nani kama c kwa MUNGU kupitia kristo yesu?iweje awe sawa na rais,waziri au mbunge?yeye yule wa MUNGU na wala c wa kaisari basi ni nani aliye mkuu Kati ya kaisari na MUNGU jibu unalo.
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto mgeuzie na la kuume. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.

Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
Jumatatu Njema.
Paskali

Br Pascal,Napenda nikuunge mkono na mguu coz nafanya maombi maalum MUNGU AJIDHIHIRISHE maana wachungaji/manabii wa uongo wamezidi kuwa wengi mno!na waumini cku hizi wanataka kuona MIUJIZA! hamjui hii ni kwa wale wasioamini?(Na hata Shetani ana miujiza pia),TUSOME NENO LA MUNGU NA NENO LIJAE KWETU! ulaghai huu utauvumbua saa 12 Asubuhi yaani mapema tu!Wafuasi wa Yesu walijulikana hata kwa mwendo wao!....Tambua MATUNDA YAO !....Mwembe hauwezi kuzaa Chungwa,......Alichounganisha Mungu ,Mwanadamu hawezi tenganisha,kama Ndoa,Mke wa Mbasha hakuzaa na mumewe wakaachana,mtoto wakagoma kupima DNA,..The Bold nae madhara hayo hayo![Pamoja na matendo mengine ya uchafu, kufanya kitendo cha mapenzi kabla kuoana kumekatazwa katika maandiko (matendo 15:20; warumi 1:29; wakorintho wa kwanza 5:1; 6:13, 7:2; 10;8; wakorintho wa pili 12:21; wagalatia 5:19; waefeso 5:3; wakolosai 3:5; wathesalonike 4:3; yuda7). Biblia inasisitiza kuepuka kitendo hicho kabla ya ndoa.hii ina maana ya kuwa ni dhambi kama ya uzinifu kwa kuwa hujaunganishwa na unayefanya naye kitendo hicho. Mapenzi baina ya mume na mke waliooana ndiyo mapenzi yanayokubalika mbele za Mungu (waebrania 13:4).]na Mke wa mtu ni katazo katika Amri 10 za MUNGU,....
Endeleeni na kudharau utashi(Uwezo wa kutambua jema na baya) mliopewa na Mungu,Mungu ajatukataza kuchunguza Wachungaji na Watumishi wa Mungu ukiogopa hilo utapotea....,Kwani mchungaji kipofu atakupeleka shimoni.
 
Who are we to judge whether Gwajima is truly a servant of God or not. Hayo tumwachie Mungu mwenyewe. Lakini jambo moja lipo wazi kuwa Gwajima amechokozwa na watawala waliokosa hekima. Nilitarajia, Kiongozi wa dini anapotuhumiwa kwa kosa kubwa kama la madawa ya kulevya, basi ushahidi wa 'kufa mtu' uwe umeshakusanywa. Kamanda Sirro anawezaje kukubali maelekezo potofu kama haya? Frankly speaking, this is simply ridiculous.
 
Kaka Paskali, hapo ndipo utajua kuwa vijana wengi wa sasa wameharibikiwa vichwa kwa sababu ya bangi na "unga". Division 0 hapewi cheti, lakini watu wameshindwa kabisa kufikiria jambo dogo kama hilo!.
Umezaliwa lini ? Nina mashaka na elimu yako !

Necta wametoa sana vyeti vya daraja sifuri kwa taarifa yako.
 
a33b3b7ca75cd8516b228acb0569f9fe.jpg

I guess ana matokeo kama haya
Ole sendeka amenyamazishwa kimtindo hahahaha, watu wana data mbaya.
 
Huwezi kucheza na serikali,serikali huwa haitaniwi na mambo ya ajabu ajabu
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto mgeuzie na la kuume. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.

Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
Jumatatu Njema.
Paskali
Mayalla kwa kilugha chetu ni njaa. We bro nimeanza kuamini Rais alikuwa sawa kukuzingua ile siku.
 
Back
Top Bottom