Kwa kusoma vitabu vyote vya Mungu kuanzia injili kuna sehemu Yesu aliingia mahekaluni akavunja vunja mali za wayahudi tena akiwa na jazba, Zaburi ya Daudi inakuambia kua Daudi hakua wa michezo! Aliwatandika kweli wapinzani wake kina Goliat, Musa alipambana na jabali La mtu Firaun mpaka tone la mwisho.Mtume Muhammad S.A.W alipigana vita vya uhud huku akiongoza msafara tena akiwa mkali kweli kupambana na maadui zake. Leo upole na uoga wa watumishi wetu hawa uko kwenye vitabu gani?
Hivyo kua na Watumishi wa Mungu wapo wapo tu wanatukanwa wameufyata,Wanaonewa wameufyata hakuna kitu Kama hicho.Hakuna kitabu kinachosema unapoonewa ukae kimya Mungu atakulipa, Hakuna! You should show reactions!
Ndio maana hata kwa kutazama sinema zilizochezwa kuigiza maisha ya Yesu utaona hakuna sehemu alipokua akicheka Cheka hovyo, hakuna sehemu alipokua akimuonea mtu haya,alimwambia Petro kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu! Ni kwa sababu alikua anajua tabia ya Petro.
Nadhani hata Mungu anawapenda sana wapambanaji wake wasiokua wanafki, wasiokua watu wa "ndio mzee" Sidhani kama mtumishi wa Mungu ukasimama kuusema ukweli na ukawa mkali Mungu akakuchukia.
Sheikh Ponda na Gwajima aina ya watumishi wa Mungu waliothubutu. Wako tofauti sana na wengine.