Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Mchungaji Richard Hananja amesema changamoto zinazojitokeza katika jamii zinapaswa kutatuliwa kwa mazungumzo na maridhiano badala ya migogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Juni 18, 2026, amesema historia inaonesha kuwa hata uhuru wa Tanzania ulipatikana kupitia mazungumzo.
Hananja amesisitiza kuwa amani ni tunu muhimu inayopaswa kulindwa na kila Mtanzania, akionya kuwa kuvunjika kwake huwaathiri zaidi watoto na wazee.
Aidha, ametoa wito wa kutafuta suluhu za tofauti kwa ustaarabu huku akieleza kuwa kujenga amani ni kazi ngumu lakini kuiharibu ni jambo la muda mfupi.