Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Steven Kimondo, amefichua kuwa kuendelea kwa matukio ya utekaji wa raia nchini ni mkakati wa makusudi unaoratibiwa ili kuwatia hofu wananchi na kunyamazisha sauti zote zinazojitokeza kudai haki, utulivu, na usawa.
Pia soma > Mchungaji Kimondo: Amani ipo iwapo haki itatendeka
Mchungaji Kimondo ametoa kauli hiyo jana Jumamosi, Julai 4, 2026, jijini Mbeya wakati wa mahojiano maalum na Sasa Live. Amesema vitendo hivyo vimeanza kuonekana kama jambo la kawaida na tabia inayojijenga nchini, jambo ambalo ni hatari na linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila mpenda haki.
"Lengo la watekaji ni nini? Kwa fikra zangu, inawezekana ni mwendelezo wa kutaka kunyamazisha sauti za watu wasiendelee kudai haki zao na kudai watu waishi kwa utulivu. Nadhani viongozi hawataki kusikia sauti nyingine inayosema kinyume na kile wanachotaka wao... Polisi wanakiri kwamba wanaye huyo mtu lakini wamekaa siku kadhaa bila kumpeleka mahakamani. Kama ana hatia sheria ifuate mkondo wake, lakini sio kukaa na mtu kwa kificho," amesema Mchungaji Kimondo.