Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mchungaji Godfrey Malisa amesema; "Bado tuna safari ndefu sana. Demokrasia ya Tanzania inatakiwa kuendelea kuipigania, bado sana. Bado kuna safari ndefu. Kwa sababu kuna wanaotaka demokrasia na kuna wasiotaka demokrasia. Na kwa bahati mbaya, wale wasiotaka demokrasia wana uwezo mkubwa sana wa kuizima demokrasia, ku-manipulate demokrasia iwafaidi wao. Kwa hiyo, bado kuna tatizo kubwa sana la ku-achieve demokrasia kwenye nchi hii.
Hatua ya muhimu kuliko zote ni kuwaamsha Watanzania, hawa raia wa kawaida kabisa ambao wako kwenye usingizi mzito. Watanzania hawajali sana, hata hiki ninachoongea hapa cha demokrasia wataona, "they don't care." Yeye Mtanzania anachojali, leo atakula nini, atalala wapi, kibarua hamna anaenda anafanya chochote kile kinachoweza kumpa pesa, basi. Unazungumza demokrasia anakuambia, "Mimi nitakula demokrasia?" Hajui. Huyu mtu hajui kabisa kwamba yuko vile alivyo kwa sababu hakuna demokrasia.
Wakishtuka, watajua, "Ala, kumbe iko hivi? Kumbe iko hivi?" Watu wengi hawajui haki zao, hawajui kabisa. Hata haki wanazopata kwenye katiba, Watanzania wengi hawajui kwamba kwenye katiba wanaruhusiwa kutoa maoni yako bila kuhojiwa na chombo chochote, hawajui. Kwa hiyo wanaogopa hata kusema. Wale wanaozima demokrasia wamefanikiwa sana kuwatia watu hofu, waogope. Na wamefanikiwa na watu wanaogopa."
Video: Mwananchi Digital