Mchungaji Mashimo: Simba hawajanipa sadaka nimewalaani

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
MCHUNGAJI MASHIMO ATOA TAMKO BAADA YA AHMED ALLY KUMKATIA SIMU

"Nimeona watu wa simba wanajisifu wapo juu wamesahau kuna mtu aliewafanya wawepo hapo juu, wamesahau kwamba mimi ndio nlisema simba SC kuwa itafanya vizuri Msimu huu na tayari wamechukua ngao ya jamii

Nimempigia simu msemaji wa simba Ahmed ally awaambie viongozi watoe sadaka yao kabla mchezo wa Super League Dhidi ya Al Ahly lakini hajapokea simu Yangu ameikata !

Mwambieni ikifika hadi jioni saa 10 hawajatoa sadaka Basi watapata laana watafungwa magoli mengi na Al Ahly, sitaki mashabiki watoe sadaka zao hii wanatakiwa kutoa viongozi wa simba sio mashabiki

Yanga niliwaambia watoe fungu la Kumi Wakadharau, laana Ambayo nimeishusha kwao ni Kushika Nafasi ya Tatu kwenye Ligi kuu Hadi watakapoleta Ile sadaka iliyobakia ya msimu uliopita, na wasipotoa hawatafika Popote wataishia Makundi" Amefunguka Mchungaji wa Taifa Pastor Daniel Mashimo

LuoBoy Media
1697794039965.jpg
 
Mbona ameizungumzia Yanga, sio simba kama ulivyosema?
"Nimempigia simu msemaji wa simba Ahmed ally awaambie viongozi watoe sadaka yao kabla mchezo wa Super League Dhidi ya Al Ahly lakini hajapokea simu Yangu ameikata !

Mwambieni ikifika hadi jioni saa 10 hawajatoa sadaka Basi watapata laana watafungwa magoli mengi na Al Ahly, sitaki mashabiki watoe sadaka zao hii wanatakiwa kutoa viongozi wa simba sio mashabiki"
 
Unabii huwa hauuzwi huyo mashimo Nabii ni pepo

Sadaka huwa hailazimishwi hata siku moja haya mapepo ndio yanaharibu sifa za Ukristo.Toka lini sadaka ikalazimishwa?

2 Kor 9:7-8​

Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema
 
Ushetani mtupu

Kwenye Ukristo sadaka huwa haidaiwi kwa nguvu wala kulazimisha

Tapeli mkubwa huyo Mashimo .SIMU ZAKE wasipokee na viongozi wa Kikristo wamfuate Mashimo wamkemee mipepo yake ya kutapeli.imtoke kwa Jina la Yesu

Toka lini sadaka ikalazimishwa kutolewa? Pepo mkubwa na shetani huyo Mashimo
 
Unabii huwa hauuzwi huyo mashimo Nabii ni pepo

Sadaka huwa hailazimishwi hata siku moja haya mapepo ndio yanaharibu sifa za Ukristo.Toka lini sadaka ikalazimishwa?

2 Kor 9:7-8​

Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema
Don't judge a book by looking cover
 
Ushetani mtupu

Kwenye Ukristo sadaka huwa haidaiwi kwa nguvu wala kulazimisha

Tapeli mkubwa huyo Mashimo .SIMU ZAKE wasipokee ba viongozi wa Kikristo wanfuate mashimo wamkemee nipepi yake ya kutapeli.imtoke kwa Jina la Yesu

Toka lini sadaka ikalazimishwa kutolewa? Pepo mkubwa na shetani huyo Mashimo
[emoji23][emoji23][emoji1666]
 
Don't judge a book by looking cover
Pepo hilo

Biblia ndio kipimo cha kupima kila kitu cha ki Mungu

Sadaka halizamishwi hata siku moja kwa mujibu wa Biblia

Mashimo ni tapeli

Na utapeli wake wazi analaximisha apewe sadaka na kutishia kulaani watu wasiotoa sadaka hiyo kwake pepo mkubwa atokomee kuzimu kwa jina la Yesu na kila akifanyacho kisifanikiwe kwa jina Yesu sababu anatukanisha na kudhalilisha Ukristo mbele ya mataifa kwa kulazimisha wampe sadaka kwa lazima na vitisho bila kujali ni waumini wa Kristo au la.Pepo Mashimo ashindwe kwa Jina la Yesu
 
Unabii huwa hauuzwi huyo mashimo Nabii ni pepo

Sadaka huwa hailazimishwi hata siku moja haya mapepo ndio yanaharibu sifa za Ukristo.Toka lini sadaka ikalazimishwa?

2 Kor 9:7-8​

Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema
Walio karibu na huyu mchungaji naomba wamsaidie!! Hajiharibii yeye tu bali anaupaka matope ukristo wote!! Nadhani anafanya mzaha, lakini si kitu kizuri kutumia nafasi ya uchungaji iliyo ya heshima kubwa kufanya mzaha!! Wakristo hatujaitiwa kulaani bali kubariki!!
 
Kabisa anaharibu sifa ya Ukristo tena wasioongee naye kwa upole Wamfokee hasa
 
Back
Top Bottom