Mchungaji Msigwa ashinda Uenyekiti kanda ya Nyasa

Mchungaji Msigwa ashinda Uenyekiti kanda ya Nyasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Mh Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini , ametetea nafasi yake kwa kumuangusha mpinzani wake Wakili Msomi Boniface Mwambukusi .

Mh Msigwa amepata kura 66 ambazo ni sawa na 62.3 % ya kura zote , wapiga kura walikuwa 108 , ambapo Mwambukusi ameambulia kura 26 sawa na 24.3 % huku Bwana Sadick Malila akijipatia kura 14 ambazo ni sawa na 13.2 %

FB_IMG_1575231085747.jpg

Mungu ibariki Chadema
 
Hahahahaha hawa jamaa sijui wanacheza sinema gani wacha tuone
 
Chadema imetuthibitishia kama wewe huna rekodi yoyote ya kukamatwa na polisi au kufanya purukushani zozote na dola, au hata kutoa maneno ya kashfa na kejeli kwa utawala, basi sahau uwongozi ndani ya chama, wala usithubutu kuchukuwa fomu, utaumbuka.
 
Matokeo sio halali.Kwenye fomu ya matokeo msimamizi wa uchaguzi hajajaza sehemu ile ya wadhifa kuonyesha wadhifa wake Ni Nini?
Mlioshindwa nendeni mahakamani
 
Chadema imetuthibitishia kama wewe huna rekodi yoyote ya kukamatwa na polisi au kufanya purukushani zozote na dola, au hata kutoa maneno ya kashfa na kejeli kwa utawala, basi sahau uwongozi ndani ya chama, wala usithubutu kuchukuwa fomu, utaumbuka.
Ulichoongea kina ukweli ndani yake
 
Chadema imetuthibitishia kama wewe huna rekodi yoyote ya kukamatwa na polisi au kufanya purukushani zozote na dola, au hata kutoa maneno ya kashfa na kejeli kwa utawala, basi sahau uwongozi ndani ya chama, wala usithubutu kuchukuwa fomu, utaumbuka.
Uongo ni aibu
 
Sawa!

Hongera kwake.
Matokeo ya Boniphace Mwambukusi hayapo aliyewekwa hapo ni.boniface Mwabukusi ambaye hakugombea.

Kisheria Ni makosa .Aliyegombea jina la mwisho Anaitwa Boniphace Mwambukusi kwenye fomu ya matokeo wameandika Boniface Mwabukusi.Huyo Boniface Mwabukusi msimamizi wa uchaguzi umemtoa wapi? Mwambukusi wewe Ni wakili iburuze chadema mahakamani kwa kutotoa matokeo ya kura zako sababu huyo Mwabukusi sio wewe.Wewe jina lako Ni.Mwambukusi.Yakatae hayo matokeo Hilo jina kwenye matokeo sio.lako mwanzo Hadi mwisho
 
Back
Top Bottom