Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Kada wa Chama cha Mapinduzi, Mchungaji Peter Msigwa ametahadharisha watanzania juu ya upotoshaji unaotarajiwa kufanywa na vyama vya upinzani nchini kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika Novemba 27, 2024.
Akizungumza na Vyombo vya Habari Disemba 09, Msigwa amesema "kuna vyama vingine vya siasa vinaashiria kutaka kuendeleza upotoshaji...vyama vya upinzani vilikuwa havijajiandaa na uchaguzi naweza nikaisemea CHADEMA kwa sababu nilikuwa huko na nilikuwa Mwenyekiti wa Kanda najua jinsi gani ambavyo vyama havikujiandaa"
Msigwa ameendelea kueleza kuwa wakati vyama vingine hasa CCM inajijenga kujiandaa na uchaguzi CHADEMA ilikuwa iinafanya maandamano hivyo mpaka unafikia uchaguzi haikuwa imejiandaa kufanya uchaguzi.
Aidha ameongeza kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amepoteza ushawishi, dira na nguvu hivyo anatafuta namna ya kuushawishi umma kuwa chama chao kilionewa katika uchaguzi na wapate huruma kutoka kwa jamii.
Chanzo: Jambo TV