LGE2024 Mchungaji Msigwa: CHADEMA inajiandaa kuendeleza upotoshaji

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Your browser is not able to display this video.

Kada wa Chama cha Mapinduzi, Mchungaji Peter Msigwa ametahadharisha watanzania juu ya upotoshaji unaotarajiwa kufanywa na vyama vya upinzani nchini kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza na Vyombo vya Habari Disemba 09, Msigwa amesema "kuna vyama vingine vya siasa vinaashiria kutaka kuendeleza upotoshaji...vyama vya upinzani vilikuwa havijajiandaa na uchaguzi naweza nikaisemea CHADEMA kwa sababu nilikuwa huko na nilikuwa Mwenyekiti wa Kanda najua jinsi gani ambavyo vyama havikujiandaa"

Msigwa ameendelea kueleza kuwa wakati vyama vingine hasa CCM inajijenga kujiandaa na uchaguzi CHADEMA ilikuwa iinafanya maandamano hivyo mpaka unafikia uchaguzi haikuwa imejiandaa kufanya uchaguzi.

Aidha ameongeza kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amepoteza ushawishi, dira na nguvu hivyo anatafuta namna ya kuushawishi umma kuwa chama chao kilionewa katika uchaguzi na wapate huruma kutoka kwa jamii.

Chanzo: Jambo TV
 

Gabbage in gabbage out = Msigwa
 
Waleta mada, leteni mada ambazo, kama ni kauli za watu, basi hao watoa kauli wawe ni watu wenye akili timamu.

Msigwa kwa sasa hayupo kwenye utimamu wa akili. Aliyoyategemea yote hayapo, na hiyo nlbila shaka ndiyo iliyomfanya kuwa hivi alivyo!! Huyu sasa ni kumpuuza kama ambavyo tunawapuuza wote ambao hawapo kwenye utimamu wa akili.
 
Duuu!...Siyo Kwa Majungu hayo Brother, Mimi ni CCM lakini simpendi mtu mnafiki kama wewe:
1:Waliweka wagombea wachache sawa, kiliwaogopesha nini Kwa watu hao wachache mpka Mkawaengua?
2:Waliweka wagombea wachache sawa,Mawakala mliwanyima fomu kwanini?
3: Waliweka wagombea wachache sawa,Masanduku ya kura feki yalikuwa ya nini?
4: Waliweka wagombea wachache sawa,Risasi Kwa wagombea wa upinzani za Nini?
5:Yaani Nchimbi mwenyewe aliona CCM wabinya haki na akasema siyo vizuri kuengua wapinzani wewe sijui ulilala ukawa husikii?
6: Warioba kaongea wewe upo TU,hata kama unachuki binafsi na Mbowe,wewe si umeshatoka huko kelele zote hizi za Nini? Si umwache na mambo yake?
 
Huyo mpuuzi mwambie tunashukuru sana kwa Promo, inatosha sasa, afanye sasa kampeni iya Chama chake
 
Sijasikia kigeni alichokisema bwana msigwa.kwamba kama chama hakijajipanga kilichojipanga kiingie na kura zilizopigwa???
 
Kabla ya kucoment kama kuna mtu anayo CV ya Msigwa naomba aiweke hapa kwa sababu tusije tukawa tunapoteza muda kwa mtu asiyejitambua.
 
Hivi mwenzetu ni DAKTARI. Nipe sababu 2 tu, kwanini nikuamini kuwa Msigwa hayupo kwenye utimamu wa AKILI. ....VIPIMO... Vinginevyo ni uzushi tu.
 
Huyu naye angenyamaza tu hata kama umenunuliwa kama huna cha kuongea unanyamaza ni busara kuliko kuongea ya kujishusha zaidi.
 
Sikujua kama msigwa angegeuka chawa na kuharibikiwa hivi. Huko nyuma hakuwa hivi sijui nini kimemuingia.
 

Hivi Mchungaji Mswiga anakazi gani CCM ?
 
Hivi kama Warioba aliona kuna zengwe ktk uchaguzi, Msigwa ni nani hata apinge?

Msigwa anang'ong'wa hata na binti yake. Msigwa akiendelea hivi, atasababisha bintiye asiolewe.
 
Naona bado anaandikiwa vimemo vya kusoma, baada ya Ubongo kuuacha Lumumba kabatini.
 
Napenda kujizima data, (kuahirisha kufikiri kizalendo), ili nijifunze kuwa chawa
 
Msigwa ameshakuwa jini tayari hata kura fake hakuziona na kuenguliwa kwa wapinzani hakukuona kwa kuwa na yeye ameshakuwa kibaka wa haki za wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…